Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

We ingia kwenye inbox yangu tuma location yako uone Basha anatinga hapo muda huu huu. Uandae na vyombo vya dola kabisa maana ndio nguzo yenu.
Mimi kazi yangu ni kutoa huduma, wewe unahitaji huduma hivyo ni jukumu lako kunitafuta. Na nakuahidi nitakulipa
 
Mimi kazi yangu ni kutoa huduma, wewe unahitaji huduma hivyo ni jukumu lako kunitafuta. Na nakuahidi nitakulipa

Mtoto wa mama toa location ujue kama una ujanja wa mjini au ulikuja mkubwa.
 
Kikubwa zaidi ni kukithiri kwa ugumu wa maisha. Huku mtaani hali ni ngumu mno, bidhaa muhimu zinapanda bei kila kukicha na wakati huohuo zinaibuka tozo zisizo na kichwa wala miguu ilimradi kuwakandamiza wananchi tu!
 
Watakuwa ni Wabunge machachari sana hili Bunge la Chama kimoko limezubaa sana.
Samahani sana, sina madhumuni ya kuuendeleza huu mjadala, lakini niseme tu wazi: kama Samia kwa njia zilizozoeleka ataendelea baada ya 2025, siioni tena CHADEMA ya "machachari" unayoiwazia wewe.
Kwanza tayari imekwishakabwa tokea sasa, sijui huo umachachari utatokea wapi?

Nitakubaliana nawe kama kitaundwa chama kingine cha siasa, na hao machachari unaowasema hapa.

Lakini ndiyo hivyo tena, siku zinayoyoma na 2025 ni keshokutwa tu!
 
Iweje SA mwenye mamlaka madogo akafanya makubwa zaidi ya mwenye mamlaka makubwa.

Rudia tena kujenga Hoja!!!
Kimamlaka, Waziri Mkuu wa Ethiopia ndiye Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu maana yake ndiye anayeunda serikali na kuisimamia.

Rais wa Ethiopia ni kivuli tu kama alivyo Mfalme Charles III.

Sasa huwezi linganisha rais wa Tz na wa Ethiopia. Labda ulinganishe Waziri Mkuu wa Ethopia na Rais wa Tanzania
 
Tatizo la hii nchi ni ujinga CCM hata wakisimamisha tofali litachaguliwa.
 
Ni wale wale wenye roho nyeusi na wasio na hoja zenye kuingia akilini. SSH anapoendeleza kumalizia miradi aliyoachiwa na hayati JPM anazidi kujiweka karibu na mwananchi wa kawaida.

Anazidi kupewa tuzo za kimataifa huko nje, wenye kujitambua wanaelewa anafanya nin lakini wale wale wenye akili mgando wanaendelea kuwa na fikra zile zile za miaka yote.
 
Kujiaminisha 2025 tutakua na mgombea mwingne tofauti na samia ni kunidanganya
Usisahau Mtoa PUMZI ni Mungu. Angalia usijejikuta unamgombanisha Bure.

Mungu akipenda Sa100 atagombea 2025 kama UCHAGUZI utakuwepo😃😃
 
Hakuna aliyekamilika hapa duniani kila mtu anakuja na mazuri yake na mabaya yake lakini yule aliyepita mhhh.
 
Juzi tu hapa Geita alipokuja Kinana walimwambiaa kabisa Samia hapendwi, mwanzoni kabisa mwa mwaka huu alikuja Shaka akasema Samia mitano tena wananzengo tena akina mama wa CCM wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Siyo kweli ndoho ndiyo nini. Subiri 2025 mama anapeta na kazi inaendelea.
 
Bro
Unamanisha kweli unachosema. Au na wewe umeshaingia kwenye orodha ya chawa. Nenda mtaani zungumza na wananchi. U don't need anya research methodology. Amka nenda mtaa wowote uliopo ongea na hao wanachi. Ukitoka hapo kamwambie mama ukweli!
 
Hakuna aliyekamilika hapa duniani kila mtu anakuja na mazuri yake na mabaya yake lakini yule aliyepita mhhh.

Huyu jamaa Salary Slip muongo huyu.
Awamu iliyopita alikuwa akisema hivi hivi. Kama unafikiri nadanganya fuatilia post zake. Huyu jamaa kazi yake ni kukosoa tuu. Yaani ingekuwa yeye ndiye aliyetuumba tungekoma na kushika adabu. Ingekuwa ni mwendo wa kukosoa halafu bakora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…