Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

SSH anaweza kuchukiwa kwa sababu ya jinsia yake lakini hana tofauti na JPM tena yeye anakwenda mbali zaidi kwa kuwa karibu na dunia nzima kwa ujumla.

Huku Dar wale wapangaji wa kwenye majengo ya Masaki na maeneo mengine wameshaanza kurudi maana yake upo mzunguko wa pesa kwa sasa.

Hao kina mama wa vijijini wenye nongwa za yule jamaa yao aliyekuwa akichanganya lugha majukwaani na wanamuelewa na kucheka wanajitafutia tu maumivu ya mioyo na kununa kusiko na sababu.
hivi wewe si ulikuwaga mfuasi wa ibilisi meko wewe???
 
Mzee upo Tanzania hiihii au ndio kujitoa ufahamu kwasababu unatumia Phillipo Bukililo unaamini kabisa kwamba jina lako litaonekana somewhere!?

Maana nashindwa kukuelewa!!??...Jamaa ameongea point zilizopo kabisa na mtaani hali halisi ndio hiyo au mwenzetu sio mtz?!?.

Ni kweli kabisa Samia kuna mambo mazuri kafanya(anafanya) na anajitahidi kwa kiasi chake ila kwa sababu zilizotajwa na muanzisha thread ni kweli kabisa zinamfanya achukiwe.

Njoo mtaani huku uone watu wanavyomuongelea kiufupi hawamuelewi kabisa nenda hata facebook upate maoni ya raia kiukweli watu wamekataa kabisa kumuelewa na yeye anajua hilo pamoja na kwamba kajenga madarasa na blahblah kibao ila watu HAWAMUELEWI
huyu ni mrundi asikupe shida, huwa anashinda ziwa tanganyika sana maeneo ya kibirizi
 
Ssh angekuwa anasikiliza critics hakika angepata Mo Ibrahim award tena sababu ni mwanamke ingekuwa rahisi na angeweka landmark kwa wanawake wengine wataokaobarikiwa kukamata dola kwa uchaguzi .

Katibu mkuu mstaafu Marten Lumbanga amenukuliwa akisema " Katiba mpya haikwepeki" wanaweza wakaikwepa lakini mabadiliko yanayoendelea duniani na haswa kwa sababu ya midororo ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi, na mabadiliko ya serikali zinazoshinda chaguzi nchi mbalimbali wahisani. Legacy kubwa mama ataiacha ni Katiba. Maana shule hizi hata zikijengwa hazitakuja kutosha, ajira ndio kabisa
 
Kuna watu ukisema ukwel wana mind kinoma ila iko waz mama hakubariki fact mbili
1:magu aliaminisha wananchi wa chini(mtetezi wa wanyonge) mama Katoa justice kaleta equality hivyo wanyonge wanaona wanaonewa tozo Nyingi
2: mwanamke apa kakosa kula za wamama
 
Hakuna mwanaCCM anayetamani upinzani uingie madarakani!

Wapo wanaotamani mwanaCCM mwenzao ashinde uchaguzi kupitia upinzani kama ilivyokuwa kwa mamvi
 
Chawa watu walishaamka muda mrefu, au unadhani matumizi ya vyombo vya dola yataendelea kuwa upande wenu kila siku? Machafuko tu ndio yatawaondoa madarakani nyie majizi ya kura.
Hakuna wakuleta machafuko nchi hii, maana watanzania Wana Imani na matumaini makubwa Sana na serikali ya CCM, ndio maana unaona hata Lisu aliposema muandamane hata wewe mwenyewe ulimpuuza na Kuendelea na shughuli zako za kukupatia kipato,maana unayo Imani na CCM na unatambua wazi kuwa Lisu Ni mbabaishaji tu
 
Watanzania wote tumeona maendeleo makubwa aliyoleta Rais Samia Suluhu kwa kipindi cha siku 567 kwaiyo 2025 mama hana haja ya kufanya ata campaign maana matendo yake yanajieleza tupo nae mpaka 2030
"Watanzania wote", hilo tu linaonyesha huna kitu kichwani. Sijui kwa nini unapoteza muda hapa JF.

Nashangaa sana umeamua kuelekeza akili yako mbovu kunijibu mimi.

Usihangaike, huwa sina muda wa kupoteza kujibishana na watu wa aina yako.
 
Kabisa umepoteza na mda na wino wako kuandika huu ushuzi? Yani 2025 samia asiwe Rais? Hamjifunzi tu jamani
 
Acha uongo na upotoshaji wako hapa wakuleta uchonganishi na kujipa faraja ambayo kwa Sasa mmekosa baada ya kuwa mmepuuzwa na watanzania
Juzi tu hapa Geita alipokuja Kinana walimwambiaa kabisa Samia hapendwi, mwanzoni kabisa mwa mwaka huu alikuja Shaka akasema Samia mitano tena wananzengo tena akina mama wa CCM wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Ilngo
 
EeeenHeeee!

Hiyo awamu ya nne yenyewe hao wapinzani walioingia bungeni ilikuwa ni kwa jasho na damu, au hukumbuki?
Democracy kwenye Nchi iliyozowea kuendeshwa na Chama kimoja tena cha kikomusti inatakiwa struglle kwelikweli.

Hata wakati huo Kinana na Nape walipambana na sisi kweli kweli.
 
Juzi kati, nilisafiri toka Kyela kwenda Zanzibar via Dar, ulikuwa usafiri maalum, abiria sio zaidi ya 30.

Baada ya Konyagi kadhaa, huku safari ikiendelea mjadala wa siasa ukaanza! Zaidi ulikuwa ukilinganisha awamu ya tano na ya sita.

Wengi wa abiria walisimama na hoja ya kuwa awamu ya tano yapo ilikuwa fupi ilikuwa ni bora zaidi kuliko awamu zote.

Binafsi nikahoji ni ubora gani ambao wana zungumzia. Wengi wao wakaanza kutaja miuondo mbinu kadha wa kadha na wengine wakasema juu ya kudhibitiwa kwa ufisadi na rushwa.... uwajibikaki wa watendaji serikali na mengi kama hayo....

Nikauliza katika miradi hiyo ya kimkakati ni upi uliokwama ama kufutwa kabisa? Sikupata jibu la moja kwa moja, zaidi ya kusema pengine sasa ingekuwa imekwisha kamilika. Nikahoji juu ya ufahamu wao katika eneo hili, sikupata jibu sahihi au la moja kwa moja zaidi ya walivyosema awali.

Nikauliza tena juu ya ufisadi na rushwa. Je kuna ufisadi gani unaoendelea sasa na vipi kiwango cha rushwa katika awamu hii? Hapakuwa na jibu la moja kwa moja, zaidi ya kelele kwamba watu sasa wanafisadi zaidi kuliko awamu iliyopita. Nikawakumbusha kuwa tukiwa njiani kwenda Kyela na tulipofika Iringa tuliamriwa kulala hapo kwani muda wa kusafiri ulikuwa umekwisha. Ni hao hao walioanza kuwashawishi Polisi waturuhusu kwani tuna safari muhimu na maalum. Wengine wakapiga hata simu makao makuu ya jeshi la Polisi ili tu tuweze kuendelea na safari yetu!
Je hiyo haikuwa kutaka rushwa? Kwanini hatukutaka kufuata taratibu na sheria ya usafiri wakati wa usiku...! Sikupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kelele tu! Huyu hatoboi 2025! Kwa nini hapana jibu!
Ndugu yangu usihangaike na Watanzania sababu aijulikani wanataka nini
 
5. Jinsia yake.

Hili nalo ni kujitetea tu, Jinsia Wala ht Si tatizo.

Pale Ethiopia ni JINSIA hiyo hiyo, mbona Yeye hakukimbilia Seat ya dirishani???

Alionyesha msimamo wote tumemkubali...
Rais wa Ethiopia siyo mkuu wa serikali kikatiba bali ni mkuu wa nchi asiye na madaraka ya kuteua au kuunda serikali.

Huwezi kulinganisha rais wa Ethipia na Tanzania maana kimamlaka hawashabihiani kabisa
 
Democracy kwenye Nchi iliyozowea kuendeshwa na Chama kimoja tena cha kikomusti inatakiwa struglle kwelikweli.

Hata wakati huo Kinana na Nape walipambana na sisi kweli kweli.
Sasa Kinana huyo huyo eshajuwa njia nzuri zaidi za kuwabana wapinzani, nafuu hiyo ya kupata wabunge wengi itatoka wapi?

Nitakuelewa vyema ukigeuza mawazo yako kuelekea kwenye mbinu mpya. Badala ya kuwaponda vichwa, sasa Samia atakuwa nawapoza kwa maneno hao wapinzani, halafu wanalala usingizi. Mbuge mmoja au wawili, bahati yao sana.
 
Kwani hiyo katiba ndiyo itatoa ajira kwa vijana? Kwani wewe kwa akili yako na upeo wako huoni mh Rais Samia anavyoweka mazingira mazuri kisera na kisheria yaliyosababisha kuongeza wawekezaji ndani ya kipindi kifupi? Huoni ajira zitaongezeka kupitia uwekezaji? Huoni namna secta binafsi ambavyo imeimarika kipindi hiki? Unazani Ni ajira ngapi zimezalishwa na zitazalishwa kupitia kuimarika kwa secta binafsi? Watanzania wanachohitaji Ni maendeleo tu siyo hizo blaa blaa zenu hapa,

kwanza nyie si mlikimbiaga kwenye bunge la katiba? Mlizani mtaitwa kubembelezwa? Au mlikuwa ninyi Ni special Sana? Watanzania wamewapuuza na Wala hawana habari na nyie na kwa Sasa wapo bega kwa bega na mh Rais wetu mpendwa mama Samia
Ssh angekuwa anasikiliza critics hakika angepata Mo Ibrahim award tena sababu ni mwanamke ingekuwa rahisi na angeweka landmark kwa wanawake wengine wataokaobarikiwa kukamata dola kwa uchaguzi .

Katibu mkuu mstaafu Marten Lumbanga amenukuliwa akisema " Katiba mpya haikwepeki" wanaweza wakaikwepa lakini mabadiliko yanayoendelea duniani na haswa kwa sababu ya midororo ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi, na mabadiliko ya serikali zinazoshinda chaguzi nchi mbalimbali wahisani. Legacy kubwa mama ataiacha ni Katiba. Maana shule hizi hata zikijengwa hazitakuja kutosha, ajira ndio kabisa
 
Badili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoani.

Nasikitika kukwambia kwamba hao wanaopata madarasa mapya hawasomi uzi kama wa kwako. Hawa wanaopata umeme huko vijijini ndani ya muda huu hawana muda wa siasa za maji taka kama hizi.

Kuna watu wanaguswa moja kwa moja maisha yao, hao hawana muda wa kusoma ulichoandika achilia mbali kuwa na muda wa kukitafsiri kwa kina.
Naona mtoa mada anajifariji tu
 
Back
Top Bottom