Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Tunawapa madini wanachimba badala ya kuacha tuje kuyachimba wenyewe hata ikija kuwa Ni baada ya miaka 500.
Tuwatoe wamasai ili kujichanganya na waarabu.
Ni kweli ilikuwa muda huo wa kizamani Ila saivi tuko nyakati za kijanja na za kimaendeleo.


Tuko nyuma vibaya mno kwa nchi za Asia ambazo tulikuwa nazo sawa miaka iyo 50-60s.


Ngoja tujipendekeze kuendana na utandawazi
Typical JPM mindset
 
Mama piga kazi kanyaga twende tumecheleweshwa kama taifa.
 
Badili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoani.

Nasikitika kukwambia kwamba hao wanaopata madarasa mapya hawasomi uzi kama wa kwako. Hawa wanaopata umeme huko vijijini ndani ya muda huu hawana muda wa siasa za maji taka kama hizi.

Kuna watu wanaguswa moja kwa moja maisha yao, hao hawana muda wa kusoma ulichoandika achilia mbali kuwa na muda wa kukitafsiri kwa kina.
Ndioooooo
 
CDM watagombea 2024 katika mazingira yoyote yale, utakuja kuyakana haya maneno yako.
The stakes are too high
CDM haitoshiriki Uchaguzi wowote, amueni kukubali Takwa la KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi,

Au tukubali kulala saa 12, maana tutakuwa tumekataa wenyewe kuheshimu matakwa na Utaratibu tuliojiwekea.

Policeee mnaowaaminia na wajeda ni ndugu, kaka na dada zetu, WATAKATAA kuwatii na hamtoamini.

Ameeeen.
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu au mapungu haya ni pamoja na haya na kukithiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Rais Samia Suluhu 2025 hana mpinzani watanzania tunamkubali sana haya yote uliyoandika ni mambo ya kufikilika tu na sio kweli ukiingia mtaani ndio utajua mama anakubalika kinoma kwasababu ndani yasiku 567
Rais Samia Suluhu amefanikiwa kupunguza gharama za kilimo pia ameboresha sekta ya elimu pia sekta ya afya ameimarisha mpaka vijijini ule ugonjwa wa fistula uliokua unatibiwa ccbrt tu sasa unatibika katika mikoa yote Tanzania Rais Samia Suluhu ameupiga mwingi sana aisee
 
Mzee upo Tanzania hiihii au ndio kujitoa ufahamu kwasababu unatumia Phillipo Bukililo unaamini kabisa kwamba jina lako litaonekana somewhere!?

Maana nashindwa kukuelewa!!??...Jamaa ameongea point zilizopo kabisa na mtaani hali halisi ndio hiyo au mwenzetu sio mtz?!?.

Ni kweli kabisa Samia kuna mambo mazuri kafanya(anafanya) na anajitahidi kwa kiasi chake ila kwa sababu zilizotajwa na muanzisha thread ni kweli kabisa zinamfanya achukiwe.

Njoo mtaani huku uone watu wanavyomuongelea kiufupi hawamuelewi kabisa nenda hata facebook upate maoni ya raia kiukweli watu wamekataa kabisa kumuelewa na yeye anajua hilo pamoja na kwamba kajenga madarasa na blahblah kibao ila watu HAWAMUELEWI
Watanzania tunamuelewa sana Rais Samia Suluhu uku mtaani tunaona maendeleo mengi aliyoyafanya maji safi na salama mpaka vijijini umeme sasa unapatikana mpka vijijini pia mikopo yenye mashart nafuu inapatikana
Ikiwa na lengo la kumuinua kijana kiuchumi tutake nini tena jaman
 
Happy kwenye utafiti, ni kwamba watanzania wengi wanataka mabadiliko anzia kipindi Cha Mrema wa NCCR.

Watu wengi wa CCM hakipendi hicho chama kwa sababu walishagundua wamegawanjwa kimakundi. Kuna kundi la high table hili ni kwa ajili ya uongozi, kundi la wapambe na kundi la mavazi. Hili kundi la vitenge, kofia, kanga na matisheti ndio ukiongea utapata ukweli kuwa wapo ili kubahatisha bahati lakini chama hakipo rohoni.

Samia ni ngumu kutoboa kwa sababu malengo yao yanafeli wakati wengine wananeemeka.
Sio weli Rais Samia Suluhu yeye anafanya haki always
 
Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Hayo mengine yote ya huko juu sikuyasoma.

Nimesoma kichwa cha mada na huu mstari wa mwisho, nikaona kwamba umetumia muda wako mwingi kuandika uliyoweka hapo juu kwa hasara kwa sababu mstari huu wa mwisho tayari umekwishafuta yote uliyoandika huko juu.

Hakuna cha "wapinzani kujipanga vizuri" kwa lolote bila ya kuwepo kwa mabadiliko katika kuendesha chaguzi.

Tayari unawaona CCM wanavyojipanga toka ngazi ya mtaa hadi juu, kuhakikisha hali haibadiliki, lakini bado watu makini kama wewe wanaimba wimbo wa matumaini?

Hayo matumaini yatatoka wapi?
 
Hayo mengine yote ya huko juu sikuyasoma.

Nimesoma kichwa cha mada na huu mstari wa mwisho, nikaona kwamba umetumia muda wako mwingi kuandika uliyoweka hapo juu kwa hasara kwa sababu mstari huu wa mwisho tayari umekwishafuta yote uliyoandika huko juu.

Hakuna cha "wapinzani kujipanga vizuri" kwa lolote bila ya kuwepo kwa mabadiliko katika kuendesha chaguzi.

Tayari unawaona CCM wanavyojipanga toka ngazi ya mtaa hadi juu, kuhakikisha hali haibadiliki, lakini bado watu makini kama wewe wanaimba wimbo wa matumaini?

Hayo matumaini yatatoka wapi?
Watanzania wote tumeona maendeleo makubwa aliyoleta Rais Samia Suluhu kwa kipindi cha siku 567 kwaiyo 2025 mama hana haja ya kufanya ata campaign maana matendo yake yanajieleza tupo nae mpaka 2030
 
Swali zuri sana, Upinzani upo Upingaji na Uanaharakati usiojua unataka nini upo pia.
Wapinzani wa atanzania wanajua kukosea kila kitu ndio upinzania hata kama ni maendeleo watapinga tu lakini Rais Samia Suluhu anawaziba midomo a kuwanyima content kwa kufanikiwa kufanya maendeleo katika sekta muhimu zinazowalenga direct wananchi
 
mama hana haja ya kufanya ata campaign
Usimdanganye.
umad.png
weweee!!😁

Watanzania tumeathirika sana na Stockholm syndrome ya Magufuli.

Na kuna sumu inasambazwa kitaa acha kabisa.

Mama ajifunge kibwebwe na kwasababu kamrudisha Kinana ambae ni gwiji la siasa za kistaarabu.

Mama atarudi 2025 kwa mbinde.
 
Amridhi = amrithi, kukidhiri = kukithiri. Nakukumbusha tu kwama Mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ndo kateua wafuatao na anaweza akawapiga chini pia wakimzingua;
1. Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi.
2. Mkurugenzi wa uchaguzi.
3. Wakurugenzi wa wilaya (DED) ambao ndo wasimamizi wakuu wa uchaguzi kwenye wilaya.
4. IGP
5. Mkuu wa majeshi
6. Kamishna wa takukuru.
7. Gavana
8. Mkuu wa usalama wa taifa
9. Mkuu wa jeshi la magereza

Jiulize mpinzani atapenya vipi kwa hiyo nguvu ya kikatiba aliyo nayo mwenyekiti wa CCM? Penda usipende mgombea wa CCM hata angekuwa Gigy Money kushinda ni lazima.

Sio kushinda ni lazima, sema kutangazwa mshindi ni lazima. Kushinda ni jambo lililoko kwa wananchi, ila kutangaza mshindi ni jambo ambalo rais ana uwezo wa kuingilia na kuamua matokeo atakavyo.
 
Acheni kujifariji na kutafuta faraja kwa watu ambao walishawapuuza nyie wapinzani mliokosa Sera na ajenda na kubakisha ubabaishaji tu na kudandia vimatukio tu vya mpito Kama ukungu wa asubuhi, Nani mwenye Akili Timamu wakuweza kuwafikiria au kuwapigia kura nyie? Nani wakuwaunga mkono nyie upinzani? Kwa Sera na ajenda zipi mlizonazo? Kwa ushawishi gani mlio nao kwa watanzania? Hamuoni kuwa watanzania walishawapuuza na kuwadharau kwa Sasa? Hamuoni kuwa watanzania walishawatupa mkono? Hamuoni kuwa watanzania hawataki kuwasikiliza kwa lolote? Hamuoni hata namna ambavyo hamsikilizwi Wala kutiliwa maanani na watanzania kwa lolote mtakalo ongea na kuzungumza?

Nani awape nchi wasaliti wakubwa Kama nyie? Nani awaamini vigeu geu Kama nyie? Unazani watanzania wamesahau akili zenu za 2015? Nani awaamini watu Kama nyie wa upinzani mliokosa dira na muelekeo? Nani awape Imani watu Kama nyie ambao hamueleweki hata mnachosimamia? Nani awaamini nyie mliokosa mizizi ya kila kitu? Nani awaamini nyie mliokosa hata safu Bora ya uongozi wa kueleweka? Nani awaamini nyie ambao hata kuandaa mtu wa kugombea Urais mnasubili atoke kwetu CCM? Nani awaamini nyie mnaokosa hata uwezo wa kujiongoza na kujisimamia wenyewe?

Kwa Taarifa yako Ni kuwa Rais Samia Ndio chaguo la mamilioni ya watanzania, Ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo, Rais Samia Ndio kiongozi aliyebeba Imani ya watanzania, Raisi Samia Ndio kiongozi anayekubalika na kuaminika na watanzania kwa matendo na kauli zake, Hakuna wa kumtikisa Wala kumyumbisha Rais Samia,

Naona mmeanza kupata kiwewe baada ya kuona Kiwango Cha kukubalika kwa Rais Samia kinazidi kuongezeka Zaid, mmepata kiwewe baada ya kugundua kuwa makundi yote yanamkubali na kumuunga mkono Rais Samia, mnataka kujaribu kutuchonganisha CCM ili mpate kupumua, lakini kwa Taarifa yenu Ni kuwa CCM Ni moja, wanaccm ni wamoja, wanachama Ni wamoja na sote tupo pamoja chini ya Mwenyekiti wetu na Rais wetu mh mama Samia suluhu Hassani

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

Chawa watu walishaamka muda mrefu, au unadhani matumizi ya vyombo vya dola yataendelea kuwa upande wenu kila siku? Machafuko tu ndio yatawaondoa madarakani nyie majizi ya kura.
 
Back
Top Bottom