Juzi kati, nilisafiri toka Kyela kwenda Zanzibar via Dar, ulikuwa usafiri maalum, abiria sio zaidi ya 30.
Baada ya Konyagi kadhaa, huku safari ikiendelea mjadala wa siasa ukaanza! Zaidi ulikuwa ukilinganisha awamu ya tano na ya sita.
Wengi wa abiria walisimama na hoja ya kuwa awamu ya tano yapo ilikuwa fupi ilikuwa ni bora zaidi kuliko awamu zote.
Binafsi nikahoji ni ubora gani ambao wana zungumzia. Wengi wao wakaanza kutaja miuondo mbinu kadha wa kadha na wengine wakasema juu ya kudhibitiwa kwa ufisadi na rushwa.... uwajibikaki wa watendaji serikali na mengi kama hayo....
Nikauliza katika miradi hiyo ya kimkakati ni upi uliokwama ama kufutwa kabisa? Sikupata jibu la moja kwa moja, zaidi ya kusema pengine sasa ingekuwa imekwisha kamilika. Nikahoji juu ya ufahamu wao katika eneo hili, sikupata jibu sahihi au la moja kwa moja zaidi ya walivyosema awali.
Nikauliza tena juu ya ufisadi na rushwa. Je kuna ufisadi gani unaoendelea sasa na vipi kiwango cha rushwa katika awamu hii? Hapakuwa na jibu la moja kwa moja, zaidi ya kelele kwamba watu sasa wanafisadi zaidi kuliko awamu iliyopita. Nikawakumbusha kuwa tukiwa njiani kwenda Kyela na tulipofika Iringa tuliamriwa kulala hapo kwani muda wa kusafiri ulikuwa umekwisha. Ni hao hao walioanza kuwashawishi Polisi waturuhusu kwani tuna safari muhimu na maalum. Wengine wakapiga hata simu makao makuu ya jeshi la Polisi ili tu tuweze kuendelea na safari yetu!
Je hiyo haikuwa kutaka rushwa? Kwanini hatukutaka kufuata taratibu na sheria ya usafiri wakati wa usiku...! Sikupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kelele tu! Huyu hatoboi 2025! Kwa nini hapana jibu!