Rais Samia anaiongoza Afrika kwa sasa, tumpatie sapoti kubwa

Rais Samia anaiongoza Afrika kwa sasa, tumpatie sapoti kubwa

Samia sio wa Nchi hii,imagine mwaka huu kaongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka bil 290 hadi bil.750,na sehemu kubwa inaenda kwenye Umwagiliaji..

Aisee ni si nouma Sana.
Hata nyongeza ya 23,3% uliwahi kuisikia kwenye awamu ipi na nchi ipi ya Afrika? Kuna jitu lilikaa miaka 5 bila kuongeza mtu hata 0.5% halafu analazimishwa awahi kazini na kuchapa kazi kwa bidii.
 
Hiyo pesa imetoka?
Samia sio mwizi, hana tegemezi maskini sana waliomzunguuka kama Marais waliomtangulia. Ukichagua rais maskini sana mtapata shida sana ya kuibiwa na ulimbukeni wa pesa. Anatembea na hela hata kwenye soksi zake za viatu
 
Ukute mtoa mada hata hajui siku inaishaje leo.
Yaani huyo sijui kaokotwa wapi na sitashangaa nikiambiwa ni product ya mikesha ya mwenge. CCM imewalemaza akili Watanzania mpaka wakati mwingine unajiuliza maswali usipate jibu.
kavulata said:
Rais Samia na Rais Sarif ndio litmas test kwa wanawake wote barani Afrika kuona kama wanawake wanaweza kuwa marais au hapana.
kavulata, je unamjua huyu mshindi wa Nobel Peace Prize (2011)

1652799927783.png
...........................................................
1652800238206.png


Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia 2006 – 2018
​
List of Female African Presidents...
  1. Slyvie Kiningi, Acting President of Burundi (February – October 1993)​
  2. Ivy Matsepe-Cassaburi, Acting President of South Africa (September 2005)
  3. Ellen Johnson Sirleaf, President of Liberia ( January 2006 – January 2018)
  4. Rose Francine Rogombe, Interim President of Gabon (June 2009 – October 2009)
  5. Agnes Monique Ohsan Bellepeau, Acting President of Mauritius (March – July 2012 and May – June 2015)
  6. Joyce Hilda Banda, President of Malawi (April 2012 – May 2014)
  7. Catherine Samba, Acting President of Central African Republic (January 2014 – March 2016)
  8. Ameenah Gurib-Fakim, President of Mauritius (June 2015 – March 2018)
  9. Sahle-Work Zewde, President of Ethiopia ( October 2018 – Present)​
  10. Samia Suluhu Hassan, Ptesident of Tanzania (March 2020 - Present)​

​
 
Tumeanza na kuangalia jinsia ya mtu ?

Vipi suala la uwezo nalo lipo au tuhakikishe tu 50/50 no matter kama wanawake wanaoweza ni 80% wakishafika 50 tuseme basi...
 
Yaani huyo sijui kaokotwa wapi na sitashangaa nikiambiwa ni product ya mikesha ya mwenge. CCM imewalemaza akili Watanzania mpaka wakati mwingine unajiuliza maswali usipate jibu...
​
Samia sio tuj atapata hiyo bali atanyakua hata tuzo ya Mo Ibrahim.
 
Really? Yaani huyu huyu aliyekuwa msaidizi mkuu wa jiwe kwa miaka mitano hadi COVID-19 ikasema hapana, imetosha!
Kuwa msaidizi wa Jiwe inahusikaje na yeye kunyakua hizo tuzo?

Jiwe ni Jiwe na Samia ni Samia,ameshanyakua tuzo ya haki za binadamu na uhuru plus tuzo ya kuendeleza Infrastructure na Afdb
 
Zenji imenufaika sana na mgao wa mikopo ulioenda shule!! Wanachekea tumboni kuogopa wasiwakwaze wat*ng*nyik*!!
 
Labda Africa ya hapo Mwanakwerekwe
Afrika iko kwenye kipindi cha mpito kutoka kuwa na marais wanaume kwenda Marais wanawake. Baada ya Mama Sarif wa Liberia sasa ni Mama Samia wa Tanzania. Rais Samia na Rais Sarif ndio litmas test kwa wanawake wote barani Afrika kuona kama wanawake wanaweza kuwa marais au hapana...
 
Haya nakubali lakini nipe sababu
Vita ni process hadi kuanza, unataka kusema mama anazidi utashi wa viongozi wa juu wa nchi hizo? Mama mwenyewe anatamani akae walau na biden hata nusu saa apige nae picha tu; akipewa ushauri juu ya uongozi wa nchi kutoka kwa biden nadhan atashukuru milele 😁 nchi haiongozwi kwa maneno tu we hujui vita ya uchumi baki kuwa omba omba tu. Yale ni mataifa makubwa ambayo mama huyu hastahili hata kuwa balozi.
 
Yaani huyo sijui kaokotwa wapi na sitashangaa nikiambiwa ni product ya mikesha ya mwenge. CCM imewalemaza akili Watanzania mpaka wakati mwingine unajiuliza maswali usipate jibu...
Mbona unaongelea habari za acting, acting na seremonial presidents kama yule wa Ethiopia? Joyce Banda na Ellen Sirlif hawakutia moyo waafrika wawaone wanawake kuwa wanaweza kiviiilee kama vile Magreth Thatcher na Angel Merkel walivyofanya kwao. Huyu Samia wetu ni Rais kamili mwanamke na anaonekana kuyaziba matundu yaliyoachwa na watangulizi.
 
Tumeanza na kuangalia jinsia ya mtu ?

Vipi suala la uwezo nalo lipo au tuhakikishe tu 50/50 no matter kama wanawake wanaoweza ni 80% wakishafika 50 tuseme basi...
Hakuna hamsini kwa hamsini bali anaeweza apewe bila kujali jinsia yake wako wangapi. Ila mwanamke mwenye uwezo ni Bora kuliko mwanaume mwenye chuki, mwizi, asiyejali wengine wanajisijiaje.
 
Mbona unaongelea habari za acting, acting na seremonial presidents kama yule wa Ethiopia? Joyce Banda na Ellen Sirlif hawakutia moyo waafrika wawaone wanawake kuwa wanaweza kiviiilee kama vile Magreth Thatcher na Angel Merkel walivyofanya kwao. Huyu Samia wetu ni Rais kamili mwanamke na anaonekana kuyaziba matundu yaliyoachwa na watangulizi.
Nilifikiri namjibu mtu mwenye akili ...pole na kwaheri.
 
Nilifikiri namjibu mtu mwenye akili ...pole na kwaheri.
Bora asiye na akili unaweza kumuelewesha kuliko yule anayetumia akili zake kupindisha mambo ili basi tu kuendeleza propaganda... (mbaya zaidi upindishaji huo ukiwa sio based on facts wala logic basi tu kuungenisha maneno ili ku-make a sentence)

Ingawa kila mtu yupo entitled to their own opinions naona watu wanadhani kwamba they can make their own facts....

Sad times indeed kwa watu tunaopenda constructive arguments based on logic and facts... Hoja za Nguvu ndio zimekuwa Rungu hapa JF....

Yaani kuna saa unaona mtu kaandika kitu ambacho unasema ngoja tuendeleze mjadala ila ukiangalia down the line majibu atakayokupa inabidi tu ujifanye haujaona
 
Huyu mama yetu LAZIMA ataonyesha nini maana ya kuwa Rais wa nchi, hata sisiminzi hatapotea wala kung'olewa kucha kijinga kama Marekana, Urusi, Ukraine na ulaya kungekuwa na rais hata mmoja tu mwanamke; mazungumzo yangetosha kuepusha vita.
Hiyo ni bahati imetokea sio kwa juhudi zake
 
Bora asiye na akili unaweza kumuelewesha kuliko yule anayetumia akili zake kupindisha mambo ili basi tu kuendeleza propaganda... (mbaya zaidi upindishaji huo ukiwa sio based on facts wala logic basi tu kuungenisha maneno ili ku-make a sentence)...
Shida yako na wenzio mna disregard all efforts being made by mama Samia for your own reasons. Majority including myself had ill thinking about her when she sworn to take the position. Lakini Sasa nimegeuka na kujisuta nafasi.

Kiukweli mama hakukuta kitu hazina bali madeni ya ndani na nje na biashara zilizobondekabondeka.
 
Afrika iko kwenye kipindi cha mpito kutoka kuwa na marais wanaume kwenda Marais wanawake. Baada ya Mama Sarif wa Liberia sasa ni Mama Samia wa Tanzania. Rais Samia na Rais Sarif ndio litmas test kwa wanawake wote barani Afrika kuona kama wanawake wanaweza kuwa marais au hapana.

Kenya kuwa na mgombea mwenza wa Raila Odinga ambae ni mwanamke ni dalili ya kwanza kuwa Mama Samia anafanya vizuri Tanzania na bado hajawaangusha wanawake wenzake East Africa na Afrika pia. Tusimchukulie poa huyu mama tumpe kila msaada anaouhitaji.

Kule ujerumani wameshaanza kuiona tofauti kati ya Rais Angel Meckel na Rais Scholz, Tayari Scholz kashaanza kuuvuruga uchumi wa Ujerumani kijinga kabisa. Ona hapa tanzania pia mama samia anapata shida ya kurekebisha ujinga uliofanywa na watangulizi wake.
Kenya Wamemchagua mgombea Mwenza wa Odinga mwanamama huku wakimtaka SSH kama mfano
 
Yaani mkikosa cha kuandika mnashindwa kukaa kimya. Vidole vinawawasha na hivyo hamchajiwi kitu JF basi mnaposti tu ujinga
Halafu hata historia halijui linakusanya tu maneno linaweka linafikiri linajua. Mwisho wa siku inaonekana wanaomtetea Mama ni ma tabulraza tu!
 
Back
Top Bottom