Rais Samia anakubali kuwa Rais Magufuli aliambukizwa UVIKO-19?

Duh!
" President John Magufuli who denied COVID-19 existed"

huu mstari mmoja umetumiwa na vianzo vikubwa vya habari duniani.

Binafsi sijaona lini au wapi amesema ' hakuna COVID-19'. Kwa uelewa wangu COVID-19 ni kirusi.
Niliyowahi kusikia, ni pale aliposema "...kinaweza kufa na joto..." Najiuliza, imekuwaje waandishi wa habari hawakuona au kusikia hayo?

Kwanini walitumia maneno hayo wakijuwa kwamba siyo kweli alikataa uwepo wa Kirusi?

Huyo muuliza maswali aidha kwa makusudi au la, Je aliamini yaliyoenea mitandaoni na baadae kwenye vyombo vikubwa vya habari ni ya kweli?

Sina majibu, ila ninachojua na alichokataa ni uwepo wa "Pandemic" na sio uwepo wa kirusi. Nina uhakika hatukuwa na vigezo vya kutamka kuwa Tanzania tuna Pandemic.

....mategemeo yangu yalikuwa Mh Raisi angeweza kutatua kinzani hiyo lakini nilichopata ni "yeah"
I am disappointed.
 
Mimi sijaona shida yeyote hapo. Rais hajasema wala muuliza swalinhajauliza kuwa Mzee alikufa kwa Covid bali 'kupatwa' (contract). Ilw pia kila mtu apaswa kujua kuwa, kuww chemist haikufanyi wewe kutopata maambukizi. Na ndio maana madaktari wakubwa nao huambukizwa. Kwa hiyo huyo jamaa aliuliza kwa namna ya kushangaa sio kwa namna ya kuhitaji jibu toka kwa Mh. Rais. Ndio maana Mama alijibu tu simply yeah..ili aendelee kama kuna jambo zaidi. Contextually huwezi kuchukulia kuwa that was a confirmation. Kutingisha kichwa au matumizi ya maneno yeah au okay okay..ktk oral communication hayamaanishi muda wote kuwa unakubali anachosema 100 100 bali nibkuonesha tu sapoti ktk mazungumzo.
 
Hapo sioni tatizo,maana kama ni kweli yeye hakuwa kiongozi wa Kwanza kuambukizwa covid.wapo viongozi wengi akiwemo waziri mkuu wa uingereza
 
Ukiangalia sura ya Raisi anaonekana ana wasi wasi hatari,ubongo na mdomo havipo kwenye sincronization,kapigwa swali,kapewa comment kabla ya ubongo hauja dadavua na kuchakata,mdomo ukasema ndio,imeisha hiyo!!!!,"he was chemist who contracted COVID"?
Hapa angekuwa ana komand nzuri ya kizungu Ili bidi afunguke amwage point kadhaa na bla blaa nyingi!!lakini wapi!
Akaingia mkenge,hakutegemea kusema ndio,basi lilimponyoka tu,
Kwa watu ambao hawajuhi jinsi Raisi anatakiwa awe na ajibu,waangalie wakati Mkapa anahojiwa na Jeff koinage kule Kenya,waone comand ya kizungu ilivyo muhimu
 
Sijasema popote ukweli ufichwe, nimesema Rais afundishwe jinsi ya kuongea, asije kukoseakosea kwenye mambo mengi mengine tu kwa kimbelembele cha kujibu harakaharaka.

Jua kusoma kwa ufahamu.
Wewe ni mpumbavu unayetaka kila mtu awaze na afikirie kila unachoandika wewe ni sahihi

Umekosa maarifa na ufahamu wa mambo, Unachokifahamu wewe tambua Wengine walianza kukitambua kabla yako na kuweka kwenye maandishi

Rais ni mamlaka, Na kwa Tanzania lazima ufahamu umpende au Usipende Rais ndie Sheria, Kanuni na taratibu

Kwa mfumo wa Tanzania wa sasa hakuna mwenye nguvu ya kumsema na kumkosoa Rais hiyo ndio Tanzania

Sheria ya kumuweka mtu Kizuizini bado Rais anayo na haijafutwa Tanzania, Anaweza kukupeleka jela daima

Sasa wewe unataka wasaidizi wake wamwambie Rais Jamaa hakupata corona wakati Yeye alikuwepo kama Makamu wake wa Rais

Hakuna Rais alipokosea kuwa Jamaa alipata korona

Thibitisha hapa kwa vyeti kuwa hakuwa na korona

Je wewe una akili?
 
Haya mambo mengine Rais inabidi akae na wataalam wamfundishe kwamba maswali mengine inabidi kuchukua sekunde kadhaa kwanza kufikiri kabla ya kujibu.
Ubongo huo anao? Kwa ufupi motheri ni slow learner anayetaka kutuaminisha kwamba naye ni genius!
 
Sisi tunaojua ukweli kuwa mlimuua sasa mmekuwa mnaangaika kuficha ukweli ila sasa mnaanza kuweweseka kwa kauli mbili mbili ukweli utajulikana tu.kuhusu kovidi kila mtz aliugua hata sa100 na kikwete waliugua na kuugua covid ndiyo kinga yenyewe tuliyo opata watz. KUUGUA COVID SIYO KUFA KWA COVID JPM ALIKUWA MGONJWA HATA KABLA YA KUWA RAIS ILA SISI TUNAJUA ALIMALIZIWA KITANDANI ILI KUSINGIZIA UGONJWA
 
Lisu alisema wakamuwakia sasa wabishie amri majeshi mkuu tuone
 
Kabisa kabisa, kwakua Mh. Rais ataambiwa alilidanganya taifa. Hawa wasaidizi buana sijui kwanini wana mpotosha Rais hivi!
 
..kilitakiwa kihakikiwe ile kisitoke public, na huo ni wajibu wa Dr.Abbas, Msigwa, na Zuhura Yunus.

..suala la Jpm kuambukizwa Covid lilitakiwa libakie kuwa SIRI ya wakubwa huko serikalini.
Mbona juzi hapa tumeambiwa makomo wa Rais wa USA kaambukizwa? Hakuna siri ktk hili. Swala la kafa na nini hiki ni kingine na ishasemwa alikuwa na issue ya umeme wa moyo JPM.
 
You nailed...tuna kihelehele sana kwa wazungu...! Na wao wanajua tu wajinga..wanatusanifu sana.
 
Rais ni mamlaka, Na kwa Tanzania lazima ufahamu umpende au Usipende Rais ndie Sheria, Kanuni na taratibu

Kwa mfumo wa Tanzania wa sasa hakuna mwenye nguvu ya kumsema na kumkosoa Rais hiyo ndio Tanzania
Duuuh! Unahorojoka mwenyewe kama katapila linalovuja oil.

Huna hata wasiwasi masikini!
 

Huko waliko jifungia kulitokea nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…