Tundu Lissu kasema kuwa, Rais Samia katika filamu ya Royal Tour, akubali kuwa Rais Magufuli alikufa kwa UVIKO-19.
Lissu kayasema hayo akiwa katika mazungumzo na Maria Sarungi.
Yasikilizeni mazungumzo hayo. Ni marefu kidogo. Ila nawarahisishia. Pale ambapo anamzungumzia Samia kukiri kilichomuua Magufuli, ni kuanzia dakika ya 35 hadi 39.
Kwa manufaa ya uwazi, mimi binafsi sijaiangalia hiyo filamu.
Hapa naleta tu kile alichokidai Lissu, ambaye kwa mujibu wake yeye mwenyewe, kaiangalia hiyo filamu.
Lakini pia, ikumbukwe, ni Lissu huyu huyu aliwahi kudai kuwa yule mlinzi wa Magufuli; huyu hapa chini kwenye picha, kwamba naye alikufa kwa UVIKO-19, ilhali wakati Lissu anadai hivyo, jamaa alikuwa bado yu hai na ni matumaini yangu kuwa bado yu hai.
Ni huyo aliye kulia kwa Magufuli na kavaa kiraia.
View attachment 2204968
Hivyo, maneno ya Lissu ni muhimu kuyasikiliza kwa umakini na si kuyabeba yote kama yalivyo bila kuushirikisha ubongo wako.
Na kama ni kweli Samia kakubali kuwa Magufuli alikufa kwa ugonjwa huo, basi hili nalo linazua masuala mengi sana.
Je, kukiri kwake huko ni Freudian Slip?
Je, wahariri wa Kitanzania wa hiyo filamu, kama wapo, waliona na kusikia alichokikubali Samia na wakakiacha kiwepo kwa makusudi au hata hawakukiona na kukisikia?
Kama ni kweli Samia kakiri, kwa nini sasa alitudanganya kuwa Magufuli kafa kutokana na ugonjwa wa moyo?
Ni nani atakuja kumuuliza kuhusu mkanganyiko huu?
Maana hata huyo Tundu Lissu mwenyewe mpaka leo hii bado hajaulizwa kuhusu huo uzushi wake wa kifo cha mlinzi wa Magufuli ambaye wote tulimwona akishiriki kwenye mazishi ya mlindwa wake.
Kwa ambao mmeiangalia hiyo filamu, hebu tujuzeni.
Ni kweli Samia alikubaliana na huyo Peter aliposema kuwa Magufuli alikufa kwa UVIKO-19?