KateMiddleton
JF-Expert Member
- Mar 15, 2021
- 3,883
- 4,676
Sikiliza sekunde ya 19-20Aliekuwa anamhoji Samia baada ya kuuliza kama Magufuli alikuwa contracted na covid na kujibiwa ndiyo alimalizia kuwa:......"na wewe ndiyo ukaupata urais".Unaelewa maana ya hii sentensi?!
Dah!...hii nchi ina mengi sana sirini.Na hiyo ilikuwa mbinu ya deep state jengo jeupe mithiri ya meli ambalo ukijichanganya ukaenda ijumaa unaweza toka Jumatatu,,, pale wanaitana chief hawatajani majina … unapoenda pale aga Kabisa nyumbani maana na simu wanakabidhi mapokezi
Cc Pascal Mayalla
Na ile timu yake je, wote walikuwa na pacemaker ?!Sikiliza tena mara tatu utaelewa swali na jibu lake, take it easy don't rush! Halafu uwe a dictionary karibu, au Google - kila neno utafute maana yake, utaelewa! Hasa neno contracted! Compare that word na haya - died of, sucurm to!
Hata mimi naona kajibu kwa wenge, chezea yai wewe unaweza tamka 'yes' hata kama umeambiwa tunataka kukuchinja saa hizi........yai weka mbali na watoto....Kaingia Wenge tu chezea mombo wewe
Tatizo lugha, huyo journalist alichomeka bila mama kujua naye kaitikia yes yes kibongo kibongo. Lakini ingekuwa kiswahili asingejibu hivyo.
Maana Mama anajua JPM alikufa kwa sababu ya pacemaker ya moyo na siyo Corona ndo maana wenza wao hawakupa hata mafua, japo ni umafya wa hali ya juu ulitumika kuwaondoa hao watu, katibu mkuu wake, kaimu katibu mkuu wake, barozi maiga, etc. Ingekuwa ni Corona Samia naye angepata, mke wake etc.
Kwahiyo pale walikuwa wakiongea kizaramo?Kiingereza kinampiga chenga mleta mada
Hajui tofauti kati ya contacted COVID na died of covid
Kwa hiyo Mafuguli alipata kwanza Covid ndio akafa au alikufa kwanza ndio akapata covid?Hakuna sehemu kwenye clip yako amesema amekufa kwa covid ila kakubali kuwa alipata covid.
ile corona ilinipata mmNi uwongo yule mzee tulimnywesha sumu ya panya
Unadhani Kijazi na wale marehemu wengine wawili waliokuwa wakikaa karibu sana na Magufuli hasa wakati wa kuapisha nao walikufa kwa tatizo la umeme wa moyo?Tundu Lissu kasema kuwa, Rais Samia katika filamu ya Royal Tour, akubali kuwa Rais Magufuli alikufa kwa UVIKO-19.
Lissu kayasema hayo akiwa katika mazungumzo na Maria Sarungi.
Yasikilizeni mazungumzo hayo. Ni marefu kidogo. Ila nawarahisishia. Pale ambapo anamzungumzia Samia kukiri kilichomuua Magufuli, ni kuanzia dakika ya 35 hadi 39.
Kwa manufaa ya uwazi, mimi binafsi sijaiangalia hiyo filamu.
Hapa naleta tu kile alichokidai Lissu, ambaye kwa mujibu wake yeye mwenyewe, kaiangalia hiyo filamu.
Lakini pia, ikumbukwe, ni Lissu huyu huyu aliwahi kudai kuwa yule mlinzi wa Magufuli; huyu hapa chini kwenye picha, kwamba naye alikufa kwa UVIKO-19, ilhali wakati Lissu anadai hivyo, jamaa alikuwa bado yu hai na ni matumaini yangu kuwa bado yu hai.
Ni huyo aliye kulia kwa Magufuli na kavaa kiraia.
View attachment 2204968
Hivyo, maneno ya Lissu ni muhimu kuyasikiliza kwa umakini na si kuyabeba yote kama yalivyo bila kuushirikisha ubongo wako.
Na kama ni kweli Samia kakubali kuwa Magufuli alikufa kwa ugonjwa huo, basi hili nalo linazua masuala mengi sana.
Je, kukiri kwake huko ni Freudian Slip?
Je, wahariri wa Kitanzania wa hiyo filamu, kama wapo, waliona na kusikia alichokikubali Samia na wakakiacha kiwepo kwa makusudi au hata hawakukiona na kukisikia?
Kama ni kweli Samia kakiri, kwa nini sasa alitudanganya kuwa Magufuli kafa kutokana na ugonjwa wa moyo?
Ni nani atakuja kumuuliza kuhusu mkanganyiko huu?
Maana hata huyo Tundu Lissu mwenyewe mpaka leo hii bado hajaulizwa kuhusu huo uzushi wake wa kifo cha mlinzi wa Magufuli ambaye wote tulimwona akishiriki kwenye mazishi ya mlindwa wake.
Kwa ambao mmeiangalia hiyo filamu, hebu tujuzeni.
Ni kweli Samia alikubaliana na huyo Peter aliposema kuwa Magufuli alikufa kwa UVIKO-19?