Rais Samia anakubali kuwa Rais Magufuli aliambukizwa UVIKO-19?

Nimekiangalia kipande anachokizungumzia Lissu.

Huenda Samia hakujua maana ya neno ‘contract’ as in ‘he contracted COVID’.

🤣.
 
Nimekiangalia kipande anachokizungumzia Lissu.

Huenda Samia hakujua maana ya neno ‘contract’ as in ‘he contracted COVID’.

🤣.
Dakika ya ngapi?

Watanzania wengi wakiwa na wazungu, wazungu wakiwa wanaongea Kiingereza, Watanzania wasiojua Kiingereza vizuri wanakosa kujiamini na wanaishia kukubali tu.

Kuna mchizi mmoja alikuwa anasema mademu wa kibongo ukiwatongoza Kiingereza wanakubali kirahisi sana.

Labda na huyu kapigwa kimombo, kakubali mpaka asiyoyaelewa.
 
It's confusing....

..Rais wa Marekani, Waziri Mkuu, na Malkia wa Uingereza wote aliambukizwa Covid.

..Hivi kuna ajabu gani kuwa Jpm naye aliambukizwa Covid?

..Na kama Ssh hakumaanisha hicho alichosema basi Ikulu ilitakiwa ikanushe.

..Hii filamu imerushwa New York, Los Angeles, na Arusha, kwa hiyo muda wa kurekebisha kauli hiyo ulikuwepo.

..Kwamba hawajakanusha ina maana gani?
 
Hiyo hapo!

Msikilize….
 
Ni ujinga tu wa mataga na sukumagangs... Dalili zilikuwa wazi kabisa
 
Msitafute wafu miongoni mwa wazima...
 
..tatizo waliingiza siasa kwenye masuala ya kisayansi.
Waliendekeza siasa za kishirikina...
Tuliwaambia na bado tunawaambia Covid-19 ni janga la kisayansi... linahitaji reactions za kisayansi!
 
Hiyo hapo!

Msikilize….
Wakati mzungu yupo katika "who contracted Covid", Rais Samia alikuwa bado anatafsiri maneno yaliyopita kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, kwa hivyo anajibu "Yeah" kwenye habari ya "He was a Chemist" bado.

Ndiyo yale yale niliyoandika hapo juu kwamba saikolojia ya Watanzania wengi ukiwaongelea Kiingereza, hususan ukiwa mzungu, inakwenda kwenye kukubali mambo by default.

Haya mambo mengine Rais inabidi akae na wataalam wamfundishe kwamba maswali mengine inabidi kuchukua sekunde kadhaa kwanza kufikiri kabla ya kujibu.

Yani, ni bora uonekane uko slow kujibu kama Obama, halafu unajibu kitu chenye kueleweka, kuliko kujifanya unawez akujibu haraka haraka, halafu unajibu kituko.

Rais Samia anahitaji team ya wataalam wa mawasiliano wamfundishe mambo mengi sana.

Sifikiri kwamba alitaka kujibu Magufuli kafa kwa Covid. Ni ushamba tu wa mawasiliano, hususan katika Kiingereza.
 
Usikute hakuelewa alichokuwa anaulizwa, aliitikia tu ila kwa kuwa ni kiongozi wa CCM sitashangaa kwa yeye kuwa kigeugeu. Mwanzoni mwaka jana alinikuliwa kwa kusema Magufuli alikufa kutokana na hitilafu ya umeme moyoni, sasa anaitikia kuwa alikufa kwa Covid. Hivi kwanini hatuna viongozi wanaojitambua, tutafika kweli huko tuendako jamani?
 
Kiingereza kinampiga chenga mleta mada

Hajui tofauti kati ya contacted COVID na died of covid
Sasa wewe nafuu yako ipo wapi kuanza kumcheka mwenzio?

Hiyo "contacted" inaeleza kitu gani hapo? Na najua utabisha, kwa sababu huoni kosa ni lipi hapo.
 
Kwahiyo wanakubalikirahisi sana mpaka unampeleka chumbani unamvua bado kingereza tu kinamchanganya?🤣🤣
 
Madaktari wanasema mtu akiwa namaradhi sugu kama moyo au kisukari ni rahisi sana kupata compications. So Alichotagaza Rais kinaweza kuwa sawa 100%

Mtu mwenye covid-19 anaweza kufa kwa kisukari auHeart Attack au vyote viwili.
 
Sasa kwa nini hawakulishughulikia hilo wakati wa editing na/ au previewing?

Kauli za Rais zina uzito usio sawa na kauli za viongozi wengine katika nchi.

Au hawakuwa [team Samia] na say so yoyote ile kwenye hiyo documentary?

Najua utakuwa unajua kuwa huku [US] kiongozi akiwa kwenye mahojiano na chombo cha habari, handlers wake wanakuwa hawapo mbali na mara nyingine huingilia kati kama wakiona mtu wao kaulizwa swali lisilo au katoa jibu lisilo.

Na mara nyingine hutoa hata statement ya ufafanuzi.

Ila sitashangaa endapo handlers wa Samia ni watu wa aina yake [kiuwezo], hivyo hata wao huenda hawakuona tatizo lolote lile katika jibu alilotoa mtu wao.

Kwa kawaida, mtu makini huchagua watu makini wa kumsaidia.

Wasaidizi wa Samia wanaakisi tu vile na yeye alivyo….
 
Kuna yule Mama aliyemtoa BBC, Zuhura Yunus.

Wote ni wale wale tu the blind leading the blind.
 
Kuna yule Mama aliyemtoa BBC, Zuhura Yunus.

Wote ni wale wale tu the blind leading the blind.
Kwa hiyo ukweli ufichwe

Huwezi kuficha ukweli, Uwongo una muda wake na hupotea kwa muda sana lakini ukweli huchelewa lakini unadumu

Issue ya Korona kuhusu Mzee ilisemwa sana na kukanushwa na Mamlaka lakini karma inafanya kazi Mama automatic kaongea na watu wameelewa


Nchi hii usanii na uwongo ni mwingi sana, Hata mambo ya jamii yanafanywa Siri, Rais ni public figure, Raia wanapaswa kuambiwa hali ya kiongozi wao

Mbona Uingereza hakuna siri ya viongozi, Wanasema live Malikia amelazwa hali sio nzuri, Waziri mkuu anaumwa hali ni tete, Ni kawaida tu uingereza
 

Sijasema popote ukweli ufichwe, nimesema Rais afundishwe jinsi ya kuongea, asije kukoseakosea kwenye mambo mengi mengine tu kwa kimbelembele cha kujibu harakaharaka.

Jua kusoma kwa ufahamu.
 
Acha wivu
 
Kwahiyo Rais alipatia kingereza chote walichoongea ila unataka kuaminisha watu kwamba eneo la covid-19 tu ndio hakuelewa kingereza?

🤣🤣🤣wacha nicheke tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…