Rais Samia analala nje ya Ikulu?

Rais Samia analala nje ya Ikulu?

Mkuu ikulu ya chamwino ni 64km za mraba yaani ni kama kutoka chalinze hadi kibaigwa, ila hela noma, yaani pamekuwa na msitu kama kazimzumbwi
Hivi kibaigwa na chalinze unapafahamu kweli mkuu?
 
Kwanza naomba mnielewe ili ni swali tu nimeuliza, hivyo naomba mnieleweshe maana mi ufahamu wangu umekomea hapo,

Rais samia hii nimeona ni mara ya pili, mara ya kwanza alipofatwa kuhojiwa ikulu na Tido, niliona anakuja na msafara, jana pia hivyo hivyo wameenda ikulu wadau wa CHADEMA wakaingia ndani kisha yeye ndio akaja na msafara,

Anakua anakuja na msafara wa magari akitokea wapi?

View attachment 2232926

Mbali na hilo pia naomba nichomekee kidogo, Sijafurahishwa na uteuzi wa mwalimu wake wa form two, hii inaonyesha hayupo serious na hii nchi aisee, tunapeana shukrani au tunajenga nchi?
Nahisi analala anapostahili kulala pia umefurahishwa na uteuzi wa nani sasa
 
Ndio atembee maana ni within the premises za ikulu.

And after all Rais ni binadamu kama sisi, analia ana cheka, ana kaa analala ana tembea anakimbia. Kwahiyo hakuna kosa lolote kusema Rais atembee.

Mungu pia alitembea. Soma kitabu cha mwanzo utaona wakati wa ijioni Mungu alipokua akitembea tembea katika bustani ya edeni ila hakumuona Adam na Hawa kwakua walikua wamejificha.

Hivyo kwakua kutembea ni jambo la kawaida sana.

Hakuna kosa lolote kusema Rais atembee. Tena ikiwezekana akimbie kabisa maana mazoezi ni afya.

Punguza kujipendekeza mkuu.
Protocol za kiusalama zinaruhusu hilo ?
 
Rais anaishi humo ikulu ila kwa kupenda kwake misafara ya magari mgeni akifika yeye hutoka na kwenda kuanzia safari yake mbali ili aingie kwa msafara.
Kwa hiyo mkuu unataka kusema huyu nae ana kaugonjwa kake kama mtangulizi wake au? Yaani nae anapenda sifa kidizaini flani hivi
 
Chalinze Hadi Kibaigwa. Ukipitia shortcut gani hiyo Mkuu ikupe km64?!
Injiniiiiiaa sooomaaaa hiyo. In Aggrey Mwanri's voice
Me nikadhani ni mimi tu sijamuelewa huyo jamaa kumbe hata nyinyi, maana siyo kwa kutudanganya huko! Km 200+ leo mtu aseme ni sawa na km64
 
Rais anaishi humo ikulu ila kwa kupenda kwake misafara ya magari mgeni akifika yeye hutoka na kwenda kuanzia safari yake mbali ili aingie kwa msafara.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daah!
 
Rais anakaa Ikulu na ukumbi wa mikutano wa Ikulu upo mbali lakini humohumo Ikulu hivyo ina mlazimu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine ndani ya ikulu kwa msafara. Ikulu ya Dodoma ni kubwa sana.

Ni kama Udom, kutoka college moja kwenda college nyingine.
Kwakuwa yeye ni mwenyeji kwanini asifike ukumbini kabla ya wageni wake [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Umeandika shortcut, Chalinze, kibaigwa. Sentensi hiyo inahusiana na urefu wakati 64 km za mraba ni eneo (ref. Post #46)
Hata hivyo, sina sababu yoyote kubishana kijinga, tuelimishane na kurekebishana kwa nia njema yenye staha.
Ndiyo nimeulizia huenda kuna shortcut watu hupita na kuipata hiyo 64kms,
Siyo lazima iwe barabara ya lami,
Mfano zamani wenyeji wa Morogoro, walienda Kibiti Kwa kupitia short cut ya Kisaki Selous,hawakuhitaji kuzunguka Chalinze Dar Mkuranga,
Songea Ifakara via Malinyi Selous Namtumbo, hawahitaji kuzunguka Iringa Njombe Songea.
Tanga walikatiza Turiani Handeni!

Sibishani natafuta short cut kama IPO tuambiane, mafuta yamepanda bei!
 
Hivi huyo mwalimu wake alimfundisha level ya f2 na3 kama elimu rasmi au alikuwa anajiendeleza ?.Maana naona mwalimu anaonekana ni kijana kuliko mwanafunzi wake
 
Ndiyo nimeulizia huenda kuna shortcut watu hupita na kuipata hiyo 64kms,
Siyo lazima iwe barabara ya lami,
Mfano zamani wenyeji wa Morogoro, walienda Kibiti Kwa kupitia short cut ya Kisaki Selous,hawakuhitaji kuzunguka Chalinze Dar Mkuranga,
Songea Ifakara via Malinyi Selous Namtumbo, hawahitaji kuzunguka Iringa Njombe Songea.
Tanga walikatiza Turiani Handeni!

Sibishani natafuta short cut kama IPO tuambiane, mafuta yamepanda bei!
Dodoma pia kuna kijiji kinaitwa Chalinze kipo kilomita chache kutoka Chamwino uelekeo wa kwenda Kibaigwa maarufu kwa jina la Chalinze nyama zamani kulikuwa kunauzwa sana nyama za mbuzi
 
Ndiyo nimeulizia huenda kuna shortcut watu hupita na kuipata hiyo 64kms,
Siyo lazima iwe barabara ya lami,
Mfano zamani wenyeji wa Morogoro, walienda Kibiti Kwa kupitia short cut ya Kisaki Selous,hawakuhitaji kuzunguka Chalinze Dar Mkuranga,
Songea Ifakara via Malinyi Selous Namtumbo, hawahitaji kuzunguka Iringa Njombe Songea.
Tanga walikatiza Turiani Handeni!

Sibishani natafuta short cut kama IPO tuambiane, mafuta yamepanda bei!
Narudia tena, 64km za mraba ni eneo.
 
Ndiyo hakai ikulu kapangisha kwenye nyumba ya mjomba wangu huku Nkuhungu
 
Back
Top Bottom