Haswa.Kwa hiyo mkuy unataka kusema huyu nae ana kaugonjwa kake kama mtangulizi wake au? Yaani nae anapenda sifa kidizaini flani hivi
Maswali mengine ni vioja kuuliza Rais analala wapi.Mbwembwe pia zakuonyesha msafara wa mkuu akiwa ndani ya himaya yake zipungunge,ndio zinajenga maswali yakipuuzipuuzi.Nadhani huo ni ukumbi wa mikutano Ikulu maana Ikulu si kama nyumba binafsi kwamba utamkuta Rais sebureni na Ikumbukwe maeneo yake ni mapana sasa kujua analala eneo gani ni jambo lingine.
Ikulu ya Chamwino sio sawa na Dar,hii ni kubwa kama Kijiji kizimaRais anakaa Ikulu na ukumbi wa mikutano wa Ikulu upo mbali lakini humohumo Ikulu hivyo ina mlazimu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine ndani ya ikulu kwa msafara. Ikulu ya Dodoma ni kubwa sana.
Ni kama Udom, kutoka college moja kwenda college nyingine.
Toka umezaliwa umewahi kuona boss anatangulia kusubiria wananchi? Au bwana harusi anatangulia ukumbini?Hizo ni sherehe za kitaifa mkuu, zinazingatia protocol.
Sasa hapo ni ikulu, ni ofisini.
Hao walikuwa wageni wake kama ilivyokuwa kwa peter alimpokea akiwa ikulu.
Kusema ukweli kitendo cha kuja baada ya akina mbowe kufika, niliwaza mengi.
Je, angekuta wameteka ofisi? Au wamejiapisha? Angewahi tu, wakamkuta.
Hata JP alipotembelewa na nnape, alimkuta ofisini (ikulu)
Samahan naomba kufahamu hii sentensi inanichanganya ya square metre.Square kilometres 64 ni kama 8km. Ni muhimu kujua kuwa kilometa za mraba sio urefu bali ni eneo
Unataka ujue anapolala!! Swali mlako halitaishia hapo!!Kwanza naomba mnielewe ili ni swali tu nimeuliza, hivyo naomba mnieleweshe maana mi ufahamu wangu umekomea hapo,
Rais samia hii nimeona ni mara ya pili, mara ya kwanza alipofatwa kuhojiwa ikulu na Tido, niliona anakuja na msafara, jana pia hivyo hivyo wameenda ikulu wadau wa CHADEMA wakaingia ndani kisha yeye ndio akaja na msafara,
Anakua anakuja na msafara wa magari akitokea wapi?
View attachment 2232926
Mbali na hilo pia naomba nichomekee kidogo, Sijafurahishwa na uteuzi wa mwalimu wake wa form two, hii inaonyesha hayupo serious na hii nchi aisee, tunapeana shukrani au tunajenga nchi?
Usijitoe ufahamu umeelewa Sana kilichoandikwaSasa ndio umeandika nini hiki.