Rais Samia analala nje ya Ikulu?

Rais Samia analala nje ya Ikulu?

Nadhani hapa kosa ni kuonekana kwa msafara, angeweza kuja na msafara wake bila kurekodiwa akaingia chumba maalum cha kusubiria wageni then anaingia ukumbini na kukuta wageni wote walishafika wala huu mjadala usingekuwepo
 
Nadhani huo ni ukumbi wa mikutano Ikulu maana Ikulu si kama nyumba binafsi kwamba utamkuta Rais sebureni na Ikumbukwe maeneo yake ni mapana sasa kujua analala eneo gani ni jambo lingine.
Maswali mengine ni vioja kuuliza Rais analala wapi.Mbwembwe pia zakuonyesha msafara wa mkuu akiwa ndani ya himaya yake zipungunge,ndio zinajenga maswali yakipuuzipuuzi.
 
Rais anakaa Ikulu na ukumbi wa mikutano wa Ikulu upo mbali lakini humohumo Ikulu hivyo ina mlazimu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine ndani ya ikulu kwa msafara. Ikulu ya Dodoma ni kubwa sana.

Ni kama Udom, kutoka college moja kwenda college nyingine.
Ikulu ya Chamwino sio sawa na Dar,hii ni kubwa kama Kijiji kizima
 
Hizo ni sherehe za kitaifa mkuu, zinazingatia protocol.
Sasa hapo ni ikulu, ni ofisini.
Hao walikuwa wageni wake kama ilivyokuwa kwa peter alimpokea akiwa ikulu.

Kusema ukweli kitendo cha kuja baada ya akina mbowe kufika, niliwaza mengi.
Je, angekuta wameteka ofisi? Au wamejiapisha? Angewahi tu, wakamkuta.
Hata JP alipotembelewa na nnape, alimkuta ofisini (ikulu)
Toka umezaliwa umewahi kuona boss anatangulia kusubiria wananchi? Au bwana harusi anatangulia ukumbini?
 
Square kilometres 64 ni kama 8km. Ni muhimu kujua kuwa kilometa za mraba sio urefu bali ni eneo
Samahan naomba kufahamu hii sentensi inanichanganya ya square metre.
Nifafanulie kiufupi.

Nikisema square metre moja ni 15000 ina maana gani? Na urefu ni wa metre 20. Kwahiyo hapa napaswa nizidishe 15000×20 ndio nitapata jibu lá kila square metre moja?

Au ni sawa tu metre yenye urefu wa centimetres 100?
 
Kwanza naomba mnielewe ili ni swali tu nimeuliza, hivyo naomba mnieleweshe maana mi ufahamu wangu umekomea hapo,

Rais samia hii nimeona ni mara ya pili, mara ya kwanza alipofatwa kuhojiwa ikulu na Tido, niliona anakuja na msafara, jana pia hivyo hivyo wameenda ikulu wadau wa CHADEMA wakaingia ndani kisha yeye ndio akaja na msafara,

Anakua anakuja na msafara wa magari akitokea wapi?

View attachment 2232926


Mbali na hilo pia naomba nichomekee kidogo, Sijafurahishwa na uteuzi wa mwalimu wake wa form two, hii inaonyesha hayupo serious na hii nchi aisee, tunapeana shukrani au tunajenga nchi?
Unataka ujue anapolala!! Swali mlako halitaishia hapo!!
 
Back
Top Bottom