Rais Samia Analipeleka na kuliongoza Taifa katika Njia Sahihi na yenye kuleta Matumaini kwa Mamilioni ya Watanzania

Maana ya Jina Lucas asiliyake ni latin uangavu au nuru ya mwanga lakini nachelea kusema na unisamehe kama nitakukwaza unaelekea kuwa giza!!. Mimi namuombea sana Mama Samia apate ufunuo kwamba anatakiwa akabidhi kijiti kwa mtu mwingine, kwa sababu atateseka sana akiamua kung'angania kipindi kingine hali si shwali deni la Taifa limeongezeka mno sisi tunaona sawa anafanya vitu lakini pesa ya kukopa inapashwa iingizwe kwenye uzalishaji na siyo matumizi. chawa wengi kama wewe wala hawampendi wanapambana abaki ili waendelee kupiga, sasa hivi matabaka ndani ya Muda mfupi yameibuka walio navyo na wanyonge, hali vijijini siyo shwali hiyo pesa yenyewe haionekani sasa hivi watu hawana furha kabisa hali ni ngumu. Mama umeongoza miaka 6 kama makamu wa Rais na miaka Mine kama Rais una nafasi sawa sawa na maraisi waliokutangulia katika haki zote usijichoshe kwa maslahi ya watu wengine wasioitakia Mema Tanzania.
 
Naona upo gizani tena katika giza tororo kabisa.

Napenda kujibu andiko lako kama ifuatavyo. Kuhusu Deni la Taifa kuwa kubwa ningependa kukupinga kuwa umedanganya na kupotosha pengine kutokana na kukosa uwelewa wamabo haya ya kiuchumi. Hapa majuzi tu imetoka ripoti ya kuzitaja nchi kumi zenye madeni makubwa,ambapo Tanzania haipo katika nchi hizo zilizotajwa.lakini nchi kama ya kenya ipo. Hii maana yake ni kuwa deni letu Ni himilivu na ndio maana ripoti mbalimbali zimeeleza na kutuhibitisha jambo hilo.

Pili kukopa siyo dhambi na wala siyo jinai na wala siyo jambo la ajabu. Kinachoangaiwa ni aina ya mkopo wako,Riba ya mkopo au masharti ya mkopo. Muda wa kuanza kurejesha mkopo na mahali unakokwenda kuweka mkopo wako. Vitu hivi vyote na vingine vimekuwa vikizingatiwa na serikali ya Rais Samia kwa kuchukua mikopo yenye masharti nafuu kabisa.

Suala la furaha kwa watanzania nalo ningependa kusema umedanganya kwa kuwa ripoti zinaonyesha kuwa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia imeendelea kupanda zaidi katika viwango vya furaha kwa wananchi wake. Kwa kuwa vitu vinavyochochea furaha vimeendelea kuimarika.mfano uwepo wa amana ,utulivu na usalama wa kutosha, demokrasia nzuri,uhuru wawatu kuzungumza, kutamalaki kwa hakika nchini,kuimarika kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa zima kwa ujumla,kuboreshwa kwa huduma mbalimbali za kijamii nazilizo karibu kabisa ya mwananchi na mambo mengine mengi sana.

Ukineda vijijini ambako wananchi wengi ni waulima wmunauta watu wakiwa na furaha na kuunga mkono uongozi wa Rais Samia ,kwa kuwa umechochea kasi ya maendeleo yao kwa kuwapa pembejeo za kilimo hususan mbolea kwa wakati,bei nzuri na uhakika wa soko kwa mazao yao na mengine mengi.
 
Chawa mmoja wewe
 
Ilaaaa ...wakukumbuke aseee sio Kwa uchawa huu ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…