Rais Samia analivusha mwaka Taifa likiwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu

Rais Samia analivusha mwaka Taifa likiwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Ni kwa Mara nyingine Tena tukiwa tunaelekea kuumaliza Mwaka tunashuhudia Rais wetu mpendwa mama wa Shoka, Jasiri, shupavu, imara, madhubuti, mwenye msimamo usiyoyumba,mcha Mungu, mzalendo, mpenda nchi yake, na mwenye maono ya Mbali Mama Samia Suluhu Hassan akilibeba Taifa letu katika mabega yake huku likiwa limetamalaki na amani, utulivu, mshikamano, upendo, kuvumiliana na umoja wa kitaifa.

Rais Samia Analivusha Taifa likiwa limetawaliwa na furaha na amani mioyoni mwa watanzania,Hakuna anayelia na kububujikwa machozi kwa kuonewa na serikali ya Rais Samia,Hakuna anayevuka mwaka akiwa magerezani kwa uonevu au kuonewa na Serikali ya Rais Samia.

Hakuna watoto wanaolia machozi majumbani kwa baba yao au mama Yao kuonewa,Hakuna anayeilaani serikali hii ya Rais Samia kwa uonevu au ukandamizaji au unyanyasaji au kusigina haki za binadamu.

Rais Samia kafanikiwa kuliunganisha Taifa letu kwa maneno na matendo, Maneno yake na matendo yake yamekuwa mfano wa kuigwa kwa wasaidizi wake na wateule wake. Husikii mteule wa Rais akisimama mahali kudhalilisha mtu au watu kwa maneno pasipo sababu.

Kila mmoja anatambua mipaka yake na wajibu wake,kila mtu anatambua kuwa kila mtu Anastahili kuheshimiwa utu wake, Ni amani kila mahali, Ni furaha kila eneo, Ni utulivu kila Kona, Ni Haki kila sehemu, Ni Upendo kila walipo watanzania, Nimaelewano miongoni mwa watanzania.

Rais Samia Ni mshindi katika kila eneo,Hakika ameshinda,watanzania Tumeshinda Na Taifa letu limeshinda,Sasa sote Tunazungumza lugha moja,Tunaelewana vyema,Tunasikilizana, tunabishana kwa hoja,Tunashirikiana katika misiba,sherehe na matukio ya kijamii pasipo kujari itikadi zetu za kisiasa.

Kauli za Rais Samia Ni Faraja kwa watanzania na Mfariji wa Taifa,ndio sababu watanzania wameendelea kuwa na Imani na upendo mkubwa Sana kwa Rais Samia,Mama yetu na kiongozi wetu mama Samia anatambua uzito wa kauli zake Kama mkuu wa nchii.

Anatambua kauli zake zinaweza kujenga umoja wakitaifa au kubomoa Taifa, Anatambua kauli zake na ulimi wake unaweza kuvutia wawekezaji na watalii au kuwafukuza.

Anatambua kauli na maneno yake yanaweza ponya mioyo ya watu au kuwa bubujisha machozi, anatambua kauli zake zinaweza Lituliza Taifa au kulitikisa Taifa, anatambua kauli zake zinaweza wafanya watanzania wakaishi kwa kushirikiana au kubaguana.

Hii ndio sababu Rais wetu amekuwa akitoa maneno yenye upendo na kujenga Taifa letu,Amekuwa Mfariji mkuu wa Taifa letu na ngao ya umoja wetu na msingi wa utulivu wa Taifa letu.

Watanzania Tunasema Asante mama yetu kwa upendo wako na uzalendo wako kwa Taifa letu katika kututumikia kwa moyo wako wote,Hakika Keki ya Taifa itamfikia kila mtanzania kupitia juhudi zako za kulijenga Taifa letu kwa nguvu zako zote pasipo kuchoka.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Umoja na mshikamano sawaa, ila ufisadi umerudi kwa kasi ya 5g!.
 
Hongera! Huu waraka umeuandika ukiwa Tz au nje ya hii nchi iliyojaa manung'uniko?
 
Karibu Sana ndugu yangu na mtani wangu Erythrocyte,wewe sinaga Tatizo na wewe japo upo chadema na Mimi nipo CCM lakini wewe Ni muungwana katika uchangiaji was hojaa na huwa hutumii maneno ya matusi,Wala kumdhalilisha mtu. Katika Hilo nakupongeza sana mwana nyanda za juu kusini mwenzangu.
 
[emoji41]
JamiiForums-28130319.jpg
 
Ila SAMIA kweli kiboko! Hajakupa tu ulaji mpaka leo!!!???
Ulaji aliyotupatia watanzania ninkazi zake ambazo amekuwa akizifanya usiku na mchana ambazo zinagusa maisha yetu watanzania,Mfano sis wakulima tunamshukuru Rais wetu kwa kutupatia mbolea za Ruzuku Hakika hapa Ni Kama Rais wetu alitupatia hewa Safi maana kwetu sisi kilimo ndio pumzi yetu Katika kuendesha maisha yetu
 
Ila katupandishia bei ya maharage, amekosea sana.
 
Back
Top Bottom