Rais Samia anaongelea matiti, tena ya Wanawake wenzake?

Rais Samia anaongelea matiti, tena ya Wanawake wenzake?

Kweli..? Ndo Kasema hivyo.!! ..Ila kama yupo Sahihi wengi nikiwacheki hao Mabinti Wanafanana na hiyo description ya Mama.....! Kawadhalilishaje Sasa?
Sasa ndo aombe wasaidiwe kisa hawavutii wanaume? Angeomba mamlaka ziwasaidie kwa sababu wameleta sifa kwa taifa. Hapa angekuwa sahihi.
Ila na sisi wanaume tunapenda msambwanda na vifua kujaa eti?
 
Yeye anaamini msichana asipoolewa kama utu..
Mentality ya kipwani na kiislamu zaidi
She is wrong maana anaongoza watanzania wenye mitazamo tofauti na tamaduni tofauti, tena hakuna sheria inayomlazimu mwanamke kuolewa
 
ILA MIMI NIMETOKEA KUMPENDA SANA MAMA. MUNGU TU AMTANGULIEAMLINDE AMPE AFYA, BUSARA NA MAISHA MAREFU.

MAMA SAMIA NA NDUGU MOHAMODOU BUHARI WA NIGERIA NDIO MARAIS AMBAO AFRIKA HUNIAMBII KITU!
unaleta ushabiki wa Simba na Yanga
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ,Ikulu Jafari Haniu naamini wewe ni mwandishi wa habari na umefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari, katika tasnia ya habari kuna kitu kinaitwa "Off Records" katika mambo anayoongea Rais sio kila jambo lazima liende kwa wananchi kuna mengine personal advice ambayo yanaweza kulenga sana maisha ya watu ,mtu au kitu fulani , sasa Rais anapoongea na Umma kupitia vyombo vya habari, jitahidi sana kuchuja kipi kiende kwa jamii na kipi ni cha ndani tu.

Hii inafanywa hivi kwa lengo la kuzuia negatives perception za watu , kama ni live ni swala la kukiambia kituo cha TV hapo weka "off records" kama ni recorded basi waambie kuwa maneno fulani na fulani hayo ni off records msiyatumie popote , nasema kwasababu hivi karibuni Rais alitoa ushauri kuhusiana na muonekano wa wadada wa timu ya mpira wa miguu "Taifa Quenss" kwa jinsi wanavyoonekana na nini future ya maisha yao wakimaliza kucheza mpira.

Maneno hayo yameleta sintofahamu nyingi sana , ikidaiwa kuwa wadada hao wamedharirishwa kijinsia , imefikia hatua mpaka vyombo mbalimbali vya habari vikilaumu juu ya maneno hayo japo ushauri wa Rais ulikuwa mzuri sana lakini mahali na njia iliyotumika kushauri ilikuwa open sana kiasi kwamba jamii nyingine imechukulia negative.

Hivyo Jafari kontrol media kipi kitoke na kipi kisitoke , kauli au maneno ya Rais yananguvu sana na kufuatiliwa na ulimwengu mzima na utajua hivyo pindi Rais akiongea jambo la kushangaza.

Aksante.
 
Katika mambo anayoongea Rais sio kila jambo lazima liende kwa wananchi kuna mengine personal advice ambayo yanaweza kulenga sana maisha ya watu ,mtu au kitu fulani , sasa Rais anapoongea na Umma kupitia vyombo vya habari, jitahidi sana kuchuja kipi kiende kwa jamii na kipi ni cha ndani tu. [emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1548]
 
Hapana mkuu. Maza hana shida. Shida waliomzunguka na mama anawaonea aibu. Najua waziri wetu mkuu Freeman mbowe kuwa ndani inamuuma sana maza. Mama ni mama tuu
Mkuu naona unajumlisha 5 unatoa 5 unabaki na 0. Kwani nini azungukwe na watu wenye shida,kwa nini awaonee aibu. Basi na yeye ana shida
 
Hii speech si aliandikiwa sasa hawa waandaaji ndo wamemuingiza chaka.
Dah naona Aljazeera naona wamereport hii kitu pia
 
Timu za soka za wanaume hazijawahi kufanya lolote la maana, halafu timu ya wanawake toka imeanzishwa imekuwa inafanya vizuri sana hadi kuna wakati nikasema, labda sisi wanaume tutajifunza kitu kutoka kwa hawa kina dada.

Halafu anakuja kiongozi mkubwa kama huyu na kutoa maneno kama haya ya kuwazodoa na kuwakatisha tamaa.

Sitashangaa kwa akili za viongozi wetu, wataanza kusema hawa wachezaji wanapromoti ushoga! Naona msingi wa kauli yake ulikuwa unaelekea huko.
 
Kwa mfano ile ya askofu Gwajima ku!kataa kiti na mic haikupaswa kupelekwa kwa public.

Inaonyesha taswira ya ushirikina kwenye muhimili!
 
Back
Top Bottom