Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ,Ikulu Jafari Haniu naamini wewe ni mwandishi wa habari na umefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari, katika tasnia ya habari kuna kitu kinaitwa "Off Records" katika mambo anayoongea Rais sio kila jambo lazima liende kwa wananchi kuna mengine personal advice ambayo yanaweza kulenga sana maisha ya watu ,mtu au kitu fulani , sasa Rais anapoongea na Umma kupitia vyombo vya habari, jitahidi sana kuchuja kipi kiende kwa jamii na kipi ni cha ndani tu.
Hii inafanywa hivi kwa lengo la kuzuia negatives perception za watu , kama ni live ni swala la kukiambia kituo cha TV hapo weka "off records" kama ni recorded basi waambie kuwa maneno fulani na fulani hayo ni off records msiyatumie popote , nasema kwasababu hivi karibuni Rais alitoa ushauri kuhusiana na muonekano wa wadada wa timu ya mpira wa miguu "Taifa Quenss" kwa jinsi wanavyoonekana na nini future ya maisha yao wakimaliza kucheza mpira.
Maneno hayo yameleta sintofahamu nyingi sana , ikidaiwa kuwa wadada hao wamedharirishwa kijinsia , imefikia hatua mpaka vyombo mbalimbali vya habari vikilaumu juu ya maneno hayo japo ushauri wa Rais ulikuwa mzuri sana lakini mahali na njia iliyotumika kushauri ilikuwa open sana kiasi kwamba jamii nyingine imechukulia negative.
Hivyo Jafari kontrol media kipi kitoke na kipi kisitoke , kauli au maneno ya Rais yananguvu sana na kufuatiliwa na ulimwengu mzima na utajua hivyo pindi Rais akiongea jambo kushangaza.
Aksante.