Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Ipo tofauti nimeiona ndani ya miezi saba tangu JPM aage dunia na Rais Samia apewe nchi. Tofauti ya uwezo wa kusikiliza na kufanya maamuzi yenye mizania sahihi. JPM hakubarikiwa busara za utatuzi wa matatizo mengi ya kiutekelezaji japokuwa alikuwa na sifa ya utatuzi huo. Hayati JPM alipenda kuamua suala pale pale jukwaani yaani muda ule ule alipokuwa ndio kwanza kalifahamu.

Rais Samia anaukwepa huu mzigo wa lawama ya wananchi. Hana pupa ya maamuzi na hutumia busara ya kusema 'mimi na wasaidizi wangu hili tunalichukua na tunakwenda kulifanyia kazi'. JPM aliamua muda ule ule, matokeo yake baada ya siku kadhaa kupita yale maamuzi yanakuwa yakifahamika kuwapendelea baadhi ya watu na kuwaumiza wengine. Baada ya siku kadhaa kupita inakuja kujulikana kuwa maamuzi yameegemea upande mmoja badala ya kuwa ni ya haki. Hulka hii ilisababisha baadhi ya watendaji serikalini kumuogopa Hayati JPM.

Na wengine hawakumuogopa bali walianzisha tabia ya kuharibu kazi makusudi ili wamuachie ofisi ateue watu wengine anaoona wanafaa kupewa ofisi. Rais Samia anakubali kutumia muda mrefu kupata utatuzi wa matatizo akijiridhisha na maamuzi yatakayofikiwa baada ya kulitazama suala husika kwa pande zote mbili. Unaweza kudhan ni udhaifu kumbe ni sifa ya uongozi, kuepuka kuleta mifarakano miongoni mwa watu wako wa karibu.

Kwani udhaifu wa tabia ya maamuzi ya jukwaani ni kiongozi kuwa wapendwa zaidi wanaoaminiwa na yeye na wapendwa wa kawaida tu. Watu wasioogopa wala kuona aibu ya kuwaharibia wenzao walio wengi kwa sifa ya muda mfupi tu.

Rais Samia ameonyesha utulivu wa kufanya maamuzi. Hajaonyesha pupa wala hasira pale anapochokozwa, mfano alichokifanya Baba Mchungaji Gwajima kingeweza kabisa kuiamsha hasira ya Samia lakini akatulia kama hakuna linalotokea. Aliweza kuonyesha ukomavu wa kiuongozi kwa kuweza kuistahimili misukosuko ya kisiasa kwa utulivu mkubwa.

Hayati JPM alipendwa kwa kusimamia haki za wananchi lakini upande mwingine wa sifa hiyo ulimpatia maadui haswa miongoni mwa wale waliokwazwa. Rais Samia ameweza kueleweka pale anaposema 'hili tunalichukua'. Hataki kufanya maamuzi halafu yakaleta msingi mbaya (precedent) wa siku zijazo.
 
Kuna hasara nyingi sana za kuhukumu hapo hapo endapo tu jambo hilo halina haja na ulazima wa kuhukumu hapo hapo.

Kuhukumu hapo hapo kuna madhara makubwa kwa sababu mara nyingi mtu anahukumu kwa utashi na kufurahisha kundi fulani na pengine ukamkosesha haki mtu mwingine.

Mama samia alipojibu hoja ya chato kuwa mkoa alijibu kwa hekima sana kwamba vitaangaliwa vigezo kama vitakidhi basi chato utakuwa mkoa.

Hekima iliyoje kwa mama yule,pale alijua fika kwamba akijibu moja kwa moja chato kwamba itakuwa mkoa atawafurahisha sana wana chato msibani na angewafariji zaidi,lakini jibu halikuwa na ulazima wa kutolewa pale pale kwa sababu baadae utakuja kuonekana muongo.

Hivyo mama yetu raisi haoni haja ya kuhukumu hapo hapo kwa sababu kwanza kesi nyingi ambazo zinahukumiwa hapo hapo hazina ulazima wa kuhukumiwa,lakini pia zinakuwa na hukumu za mihemko mara nyingi hivyo mama anaona bora ajiepushe nazo.

Hekima na kufikiria kwanza kisha ndipo unajibu.
 
Uongozi ni kuamua tu kuchukua njia unayopita, unapita unaenda zako bila ya kujali kelele za kutoridhika au vigelegele vya kuridhika.....,miaka yenyewe mingapi ya uongozi ya kuridhisha wote!!

Maamuzi ya papo kwa papo yana uwezekano mkubwa wa kukosea kunakotokana na kukosa taarifa sahihi na mwisho wa siku mtu anaonewa (nina uhakika katika kila maamuzi natano ya papo kwa papo, mawili yanakuwa sivyo). Faida ya hii ni kuwa watu ni kweli wanakuogopa na hujitahidi kuwa 'sio wao' ili kubaki salama

Style ya mama ya 'kulichukua' ina uwezekano wa kutenda haki lakini ina shida ya kuchelewa na......nchi ni kubwa sana yatachukuliwa mangapi miaka yenyewe mitano au 10 tu!

Suluhisho: nenda tu na unachoamini ni sahihi!
 
Hili la tutalichukua hata mimi nililipenda manake suala la kusikia hapohapo ukatoa uamuzi unaweza kuingizwa chaka.

Kiongozi analichukua anaenda kuketi na wasaidizi wake, wanalichakata kisha anafanya kitu Wamatumbi wanaita informed decision. Ukifanya papo kwa papo kunakuwa na information asymmetry na matokeo yake uamuzi unakuwa biased.

Nakumbuka mama mmoja aliwahi kulia mbele ya JPM na JPM akatoa maamuzi fulani ikiwa ni pamoja na mama kupewa ulinzi ila baadaye ikajajulikana kwamba yule mama ni tapeli; angelichukua na kulichakata angejua mama alitaka kumuingiza King!

Mama anajipa muda kabla hajafanya maamuzi; wengine wanaweza kusema hafanyi maamuzi lakini si sawa kwa kuwa ili ufanye maamuzi mazuri unatakiwa kuwa na information toshelevu.

Maamuzi ya Rais ni hatari hayafai kufanyika kidharura kwani yanaweza kujeruhi vibaya.

Mama yachukue yachakate, rudisha feedback na itakuwa vyema hiyo feedback ikiwa public.
 
Uongozi ni kuamua tu kuchukua njia unayopita, unapita unaenda zako bila ya kujali kelele za kutoridhika au vigelegele vya kuridhika.....,miaka yenyewe mingapi ya uongozi ya kuridhisha wote!!

Maamuzi ya papo kwa papo yana uwezekano mkubwa wa kukosea kunakotokana na kukosa taarifa sahihi na mwisho wa siku mtu anaonewa (nina uhakika katika kila maamuzi natano ya papo kwa papo, mawili yanakuwa sivyo). Faida ya hii ni kuwa watu ni kweli wanakuogopa na hujitahidi kuwa 'sio wao' ili kubaki salama

Style ya mama ya 'kulichukua' ina uwezekano wa kutenda haki lakini ina shida ya kuchelewa na......nchi ni kubwa sana yatachukuliwa mangapi miaka yenyewe mitano au 10 tu!

Suluhisho: nenda tu na unachoamini ni sahihi!
Suluhisho lenye manufaa ni sulihisho sahihi si suluhisho lililowahi.
 
Wote wanaweza kuwa sawa..
Wote wanaweza wasiwe sawa..
Mmoja anaweza kuwa sawa na mwingine hapa.

Taifa la Tanzania na watu wake kuna mahala linamtaka Marehemu JPM na hulka yake ileile..
Hii nchi kuna baadhi ya watu wajinga sana, narudia tena wajinga sana na ndio wanasababisha hii nchi iwe hapa kwa sasa..

Wakati huu Taifa linahitaji mtu kama marehemu atuvuruge sana na tukija kukaa sawa miaka mingi mbele ndio waje viongozi aina hii ya Mama , pamoja na JK... Style ya uongozi wa mipango na kuamini watu inafaa sana kwenye mataifa yaliyoendelea tayari lakini sio kwa Taifa kama hili lenye baadhi ya watu primitive na wajinga...
 
Taifa hili linawatu wajinga tena sio wajinga kidogo, ukiwaminya watalia na kutoa vilio kila mahala lakini ukiwaacha watakudharau na kukuimbia kila aina ya nyimbo za kukukebehi...

Jk alijitahidi kuaacha mambo loose ili watu wanyanyuke kiuchumi na maendeleo yafike kwa kila mtu lakini maajabu ya Musa, watu walewale waliotajirika kwa mgongo wa JK kwa wizi ndio hao hao wakaanza kumletea dharau na kumuumdia mipango ya kumuangusha au kuhakikisha chama kinamfia na kumhujumu kwa kila namna lakini ni JK huyu huyu aliyewapa utajiri....
 
Wote wanaweza kuwa sawa..
Wote wanaweza wasiwe sawa..
Mmoja anaweza kuwa sawa na mwingine hapa.

Taifa la Tanzania na watu wake kuna mahala linamtaka Marehemu JPM na hulka yake ileile..
Hii nchi kuna baadhi ya watu wajinga sana, narudia tena wajinga sana na ndio wanasababisha hii nchi iwe hapa kwa sasa..

Wakati huu Taifa linahitaji mtu kama marehemu atuvuruge sana na tukija kukaa sawa miaka mingi mbele ndio waje viongozi aina hii ya Mama , pamoja na JK... Style ya uongozi wa mipango na kuamini watu inafaa sana kwenye mataifa yaliyoendelea tayari lakini sio kwa Taifa kama hili lenye baadhi ya watu primitive na wajinga...
So linahitaji Rais wa kuuliza wananchi nitumbue au nisitumbueeee
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hauko serious au wew ni walewale
 
Bado hii nchi iko kwenye stage ya wapumbavu hivi kufa, wengine kupotezwa na wengine kwenda magerezani, hiyo ndio stage tuliyopo kwa sasa ili kuwe na discipline baina ya mtu na mtu na baina ya watu na dola.

Mifano iko mingi na mingine tayari imeshaanza kuonekana....Leo hii wauza mafuta tayari wanaitisha serikali na kupandisha bei za mafuta hovyo hovyo, ukiwakemea wanakutishia kugoma au kuficha mafuta ili uwapigie magoti, lakini watu hawahawa ukiwa mtemi kwao wanapiga kimya na kuendelea kufanya biashara.

Bei za vifurushi vya simu mama kasema vishuke lakini watu wamekaza kijeuri na wenye mamlaka wako kimya mambo yanaendelea.

Sijui watu kama wanaona hii hali ya mtandao wa internet kuwa chini karibu mitandao yoote kiasi cha kuchukua muda mrefu kufungua page au kutuma kitu, hapo mwananchi anaibiwa tayari kwa kutumia bundle kubwa kwenye kuload watu wako kimya.
 
Back
Top Bottom