Siyo kweli kuwa JPM alikuwa anakurupuka kutoa uamuzi bali alikuwa anatembelea sehemu akiwa na data za kutosha kuhusu sehemu anayotembelea. Kwa mfano alipompandisha Mbuge kutoka Kanali hadi kuwa Brigadier general papo kwa papo alishailiongelea jambo hilo na CDF, na ndiyo maana CDF akamvika Mbuge nyota zile siku hiyo hiyo kwani alikuwa anajua. Alipomfukuza DAS wa Kisarawe, alikuwa ana taarifa zote na alisema aliwahi kumuonya mara kadhaa. Hata hivyo wanachi walipoomba barabara ya kwenda Kibaha, hakutoa amri ya papo kwa papo bali aliwaambia hilo analibeba na atalifanyia kazi.
Alipomfukuza yule marehemu mkurugenzi aliyechongewa na Makonda, alishakuwa na taarifa zaidi juu ya ubadhirifu ulikokuwa unafanywa naye hata kabla ya Makonda kuzungumza, na ni kutokana na msukumo wa kutaka maelezo ya taarifa hizo za ubadhilifu ndipo Makonda akatoa lawama hizo. Alipoamuru ATCL iwe ina mmbeba Mapunda na mke wake bure, ni swala ambalo lililkuwa limeshaongelewa na bodi ya wakurugenzi wa ATCL na ndiyo maana siku hiyo Mapunda akawa amepewa kiti pale high table.
Kudhani kuwa alikuwa anakurupuka kutoa maamuzi siyo sahihi, alikuwa anafanya homewrok yake kabla ya kwenda ziaranai na alipokuwa huko alikuwa data za kutosha sana. Ni mtu aliyekuwa na uwezo wa kujua idadi ya samaki kwenye ziwa asingeshindwa kujua matukio ya kwenye sehemu alizokuwa anatembelea kabla hajafika.