Kwa aina ya watu tulionao kwenye utumishi wa umma, sekta binafsi zenye kushikilia kiuchumi, na wananchi wa kada nyingi tulihitaji uongozi wakariba ya Hayati JPM watu wetu wengi tunawaongoza wanahitaji kusukumwa kwa nguvu ukiwapa nafasi ya kujisimamia wanaujinga mwingi kuliko unavyo weza kufikiria. Mtu ambaye anatoa malalamiko kuhusu aina ya uongozi wa JPM hajawahi kuongoza... sisi ambao ambao tumeongoza taasisi na makundi makubwa ya watu tunajua namna watu wetu waliovyo.. ukilegeza kamba kidogo jiandae kulaumiwa..
Watu wanawaza wizi na utajiri wa kupindukia wanawaza rushwa kwa makusudi, hawana mipango ya kufanikisha malengo ya taasisi, wanasababisha urasmu ili kuweka mazingira ya kupewa kitu, angali taasisi za uma zenye mamlaka ya utoaji leseni, vibali mbali mbali wanavyo tekeleza majukumu yao kuna mambo hayapo sawa ni watendaji wachache sana wenye kusimamia haki. Angali mahakama, polisi, uhamiaji na vyombo vingine vinavyo simamia sheria, ukiwa ni mtu ambae umehudumiwa na makundi haya kwa haki bila usumbufu au mazingira ya rushwa una haki ya kukataa aina ya uongozi wa JPM.
Kwa eneo kubwa mama ni mtu laini sana kuweza kusimamia nchi yenye watu wa aina yetu, hakuna kitakacho fanyika kwa kizingatia muda na gharama halisi ( Inflation kila kona) , kila siku ataishia kutueleza yeye ni mpole asiye fokea watu nk. Si mlaumu maana mazingira alikotokea na aina ya maisha aliyopitia hii kwake ni zali la mentali..... Lakini watamwangusha sana kwa hilo ninauhakika kwa kuwa nayashuudia kila siku.
Wafanyabiashara duniani kote ni watu wanaobanwa kulipa kodi na kudhitiwa kwenye mfumuko wa bei, ukiwaachia wanakuchezesha maana mstari kati ya wahalifu wa wafanyabiashara ni mwembamba sana. Swali la kujiuliza ni kwa hawa wamachinga wanaolalamikiwa kukwepa kodi..(Kuchafua mazingira naliacha kwanza) Je machinga ni nani ... trade dealer, peddler au mchuuzi yaani ni mtu anaeuza end products to be used with last consumer.. Sio Distributor, sio whole seller sio muagizaji, kama hivyo ndivyo serikali inashindwaje kukusana kodi yake? Maana yake wafanyabiashara wakubwa wana watumia machinga kukwepa kodi... sasa leo Dar wameanza kuwaondoa ngoja tuone makusanyo kama yataongezeka! Petrolium products zinapanda kila kukicha, bidhaa za chuma kila siku juu, mafuta ya kula nk Bila kuwa na mtu wa kuwafinya wafanyabiashara wananchi wa kawaida ndio wana beba mizigo yote na mwisho umasikini kuisha kwao ni ndoto ya alinacha.