Nadhani ulikuwa humfahamu Magu vizuri wewe,ile style yake ndio inafaa zaidi na yenye matokeo kwenye taifa linalokuwa kama hili.
Kwanza mpe heshima yake kama kiongozi mwenye ujasiri wa kusimama popote pale hasa vijiji vya njiani kusikiliza kero za wananchi na mkutano kwenda live Tanzania nzima ambapo shida za kijiji hicho inaweza kuwakilisha matatizo ya vijiji kama 10000 Tanzania hii.
Na ambalo hulikuwa hulijui ni kuwa huyu mzee alikuwa anatembea na viongozi wa ngazi zote kuanzia mkoa mpaka kijiji na kabla ajatoa hukumu alikuwa anaitisha viongozi wote ambao walipaswa kuwajibika kwenye hiyo kadhia.
Nenda youtube kapitie kesi moja ya kisima cha maji huko wilaya ya kongwa Dosoma ya mheshimiwa aweso uone jinsi viongozi wenye dhamana walivyo wazembe mpaka ikamlazimu mheshimiwa waziri atoe hukumu pale pale mbele ya wananchi maana inatia hasira ukiangalia jinsi wananchi wanavyokosa huduma ya msingi kwa uzembe wa kipumbavu wa watu wachache waliokabidhiwa dhamana hiyo.
Mwisho najua umeandika hili kuwafurahisha mabwana zako kumendea teuzi ila sijapenda kumlinganisha hayati Magufuli hapa,nikukumbushe kusimama kusikiliza,na kutatua kero za watu ambao sio hata ndugu zako huo ni wito sio kila binadamu au kiongozi anazaliwa nao,usikute hata wewe mtoa mada kukaa na ndugu zako kusikiliza shida zao pasi na kuwasaidia kifedha hata kuwapa ushauri tu mawazo courage hiyo huna sasa tukikupa uongozi utaruhusu watu wapenye ofisini kwako waje walie shida zako.
Kama hukunufaika na uongozi wa Magufuli basi kuna maskini na wanyonge huko ndani ndani walipitiwa na baraka zake mpaka leo ndio hao wanamkumbuka na kumuombea huko aliko kwa sasa sema tu uwezo wa kuingia hapa Jf na kutoa ushuhuda hawana.
Uongozi wa kusikiliza na kutatua shida za wananchi wanyonge ni wito,na huu wito ni inborn character mtu anazaliwa nao.