Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Viongozi wengi dhaifu kuamua mambo magumu majukwaani.
Magufuli alikuwa dhaifu
Asante mungu umemuondoa haraka
 
USA Kwenyewe wanainua manage itakuwa bongo?
Bongolala wewe
 
Haya
USA Kwenyewe wanainua manage itakuwa bongo?
Bongolala wewe
Poa bongo lala! Unafikiri wote wageni nchi hii! USA inauhuru zaidi ya miaka 240 wewe unaleta upumbavu hapa! Viongozi lazima wawajibike kutetea wananchi! Unakabidhi shamba la mahindi kwa nyani!
 
Usimpambe, uwezo huo wa kufanya maamuzi yenye tija na sahihi kwa muda mfupi Samia hana! Magu ni namba nyingine, usijaribu kulinganisha na photocopy iliyoishiwa wino!
Photocopy imewaondoa wamachinga na sasa mitaa inafanyiwa usafi. Photocopy iliweza kuongoza vyema bunge maalum la katiba likamalizika kwa salama na amani kabisa.
 
Tabia ya magufuli ya kuhukumu hapohapo aliambukizwa Lukuvi kwenye kutatua migogoro ya ardhi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Wanadhani ni ujasiri kuamua pale pale kumbe ni kielelezo cha kiburi cha kiume ambacho kimeumiza dunia nzima.

Hitler, Mussolini na wengine wengi tu walidhani ni ujasiri kuamua pasipo kujiridhisha matokeo yake hasara waliyoitengeneza haina mfano.
 
Photocopy imewaondoa wamachinga na sasa mitaa inafanyiwa usafi. Photocopy iliweza kuongoza vyema bunge maalum la katiba likamalizika kwa salama na amani kabisa.
We naye🤷, kwani kuongoza bunge la katiba ni kazi!? Kama Ndugai ameweza kuliongoza bunge la JMT nani atashindwa kuwaongoza hao wabunge🤷 waliojaa unafiki zaidi kuliko uhalisia! Yeyote yule angeweza kufanya vizuri zaidi na sasa nchi ingekuwa na katiba mpya!
By the way, matokeo ya hilo bunge la katiba mnalolipigia upatu ni nini vile🤷, kama haukuwa mchezo wa kuigiza!
Mnampa sifa asizostahiri🤔!
 
Uwezo anao ndio maana anakuongoza wewe na mimi. Uliyemtaka awe kiongozi kashindwa kuliongoza taifa hili.
 
Uwezo anao ndio maana anakuongoza wewe na mimi. Uliyemtaka awe kiongozi kashindwa kuliongoza taifa hili.
Hujitambui ww! Sasa hivi tunaongozwa na vivuli vya nje na ndani, siyo huyo mama! Kiongozi tuliyemchagua aliyekuwa analiongoza taifa letu bila ya kuongozwa na vivuli mlimfanyia hiyana, Mungu akamtwaa! Ila Mungu hatalisahau taifa letu hili, Magu wengine tunapiga jalamba kuja kuiongoza nchi!
 

Toka lini kazi ya MUNGU ikafanyiwa hiyana na binadamu? Umetendwa wewe na conspiracy theories zenu nyie gang!!
 
Pole sana mkuu, Hizo imani za vivuli mtazeeka nazo na hazitawasaidia. Huyo aliyekuwa anaongoza yeye alileta kipi cha ajabu na cha maana kwa taifa hili?.
 
Usimpambe, uwezo huo wa kufanya maamuzi yenye tija na sahihi kwa muda mfupi Samia hana! Magu ni namba nyingine, usijaribu kulinganisha na photocopy iliyoishiwa wino!
Magu aliamua hapo hapo na maamuzi yakawa na madhara makubwa yaliyodumu miaka na miaka. Mama anabeba suala ili aende akalitazame suala kwa undani ili asije kumuumiza mtu au watu.
 
Magu aliamua hapo hapo na maamuzi yakawa na madhara makubwa yaliyodumu miaka na miaka. Mama anabeba suala ili aende akalitazame suala kwa undani ili asije kumuumiza mtu au watu.
Kwanza si kila jambo aliloletewa Magufuli alilitolea maamuzi papo kwa papo..Pili, mengi ya aliyokuwa anayatolea maamuzi yalitokana na uzembe au dalili za uonevu, tatu, mengi yalihusu viongozi chini yake kushindwa kuwajibika..wewe unaona maumivu ya maamuzi kwa mtu anayetajwa kuumiza wengine, mbona husemi maumivu ya wale wanaoshitaki wakati huo kwa Magufuli, mfano yule Mama wa Rukwa ambaye ng'ombe zake ziliibiwa miaka 9 anapigwa dana dana na wezi wanajulikana, inawezekana ndani ya muda huo alishindwa kusomesha watoto, pengine hata vifo vilitokea kwa kukosa matibabu stahiki kwa kukosa pesa nk hiyo gharama wewe unaiona si kitu..mambo mengine huhitaji kusema unalichukua wakati unaona dhuluma wazi wazi, acheni bwana..jambo haliko kwako bora unyamaze, wahanga wa mambo haya ndio wanajua gharama na maumivu yake! mfano jambo lilmepelekwa hadi kwa DC mtu hajapata msaada, sasa unalichukua halafu nani utampa alishughulikie km si DC huyo huyo ambae kama alishindwa hapo mwanzo, mara ya pili ndio ataweza??acheni ajenda mufilisi za kukosoa wakati hata familia yako tu huwezi kuwaongoza! Mtu mwenye hulka ya uvivu, uonevu, dhuluma, rushwa ndio anaweza kosoa maamuzi ya papo kwa papo, lakini kwa mkulima asiyejua hata kazi za DC ni nini, maamuzi ya aina hii yana faida na ahueni kubwa kwake..bora ukosee kuamua papo kwa papo kuliko kujipa muda kuamua halafu ukachelewa kuamua, au usiamue kabisa yaani funika kombe...au hata ukatoa maamuzi ya upendeleo. Na mara zote, zote kabisa Magufuli alikuwa haamui bila pande zote kuwasikiliza! kama una mfano wa mtu alitolewa maamuzi bila yeye kusikilizwa leta hapa huo mfano...! Kama kiongozi hana jicho la tatu kuona zaidi ya kile watu wengine wanaona, huyo si kiongozi! ukisoma mifano ya watawala kama mfalme Suleimani nyakati zile hakuna pahali unakutana na kauli ya ninalichukua nitashughulikia..viongozi wanaojua jamii wanayoiongoza huomba jicho la tatu ili iwasaidie kuamua papo kwa papo!
 
Tusaidie kujua pale kigamboni nani alikua anamiliki ile nyumba na ni nani alikua anafyonza yale mafuta,
Na nini kinaendelea?
Maana hakuna cha wandishi wa habali wala kiongozi anapasemea tena ispokuwa wameufyata tu.
Na kama ilikua halali yake kufyonza na hakukua na hasara kwa serikari basi tujibiwe tujue.
 
Umeandika mengi lakini naamini busara ni kujipa muda wa kufahamu pande zote zenye uhasama kuliko kuamua hapo hapo halafu madhara yake yakaendelea kuumiza jamii inayohusika.
 
Swala umelianzia katikati kama kila mtu analifahamu. Halafu .ukaongeza na hisia nyingine kwa ujumla tulia uandike upya na kwa kirefu.
 
Umeandika mengi lakini naamini busara ni kujipa muda wa kufahamu pande zote zenye uhasama kuliko kuamua hapo hapo halafu madhara yake yakaendelea kuumiza jamii inayohusika.
Hayo uliyoandika #1 na mengine yooote ukilinganisha na niliyoandika mimi yapi ni mengi?? wewe ni mjinga na mufilisi wa fikra unasifia sifia tu kama zuzu..wewe unapoumiza wenzio busara huwa iko chooni siyo..!ukiguswa ndio unaikumbuka busara, wahedi kabisa..kiongozi anayefanya homework yake vzr kuwatumikia watu hahitaji kujipa muda kuamua mambo yanayoleta maumivu kwa watu anaowaongoza, uhasama gani unaoongelea...??? watu wanalalamikia mradi wa maji kutokamilika huo ni uhasama? hivi unafikiri sawa sawa wewe! kwako jamii inayoumia ni ile inayoguswa na maamuzi ya papo kwa papo basi, vipi wale wanaoshitaki kwake wao ni halali kuumizwa..siyo! bora unyamaze. Mara nyingi wanyonge japo wanaumizwa huwezi sikia kelele za aina hii km za huyu mjinga..magenge ya wahuni, walafi, wabinafsi na wezi wanapoguswa kwa matendo yao kelele km hizi ndio wimbo wa kila siku, mara hakuna utawala wa sheria, mara oo demokrasia hakuna, mara oo maamuzi ya papo kwa papo ni mabaya..misemo miiiingi kisa tumbo! peleka kwenu huu ujinga!
 
Kuna mzee mmoja aliwahi kunambia Hitler ndo alichangia kuifanya Ujerumani ifikie hapa ilipo.

Ukiwa mtu wa kutembelea ofisi za umma na ukakutana na urasimu uliopo.... Utatamani umwage damu.

Sisi Watanzania tukishapata pakujishikiza tunadharau sana wengine...
 
Nakuona Mnyangara ukimpigia ndugu yako ingawa hayupo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…