Rais Samia anawezaje kujenga zahanati 564, Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68?

Hivi kweli tukae kimya,

Mtu anajenga Zahanati 500,

Mtu anajenga vituo vya afya 300

Mtu anajenga hospitali 70

Tukae kimya eti tukisema tunalipwa,


Shame on you,
 
Hikweli tukae kimya,

Mtu anajenga Zahanati 500,

Mtu anajenga vituo vya afya 300

Mtu anajenga hospitali 70

Tukae kimya eti tukisema tunalipwa,


Shame on you,
Samia analipwa mshahara kiasi gani.?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Kumbuka hii ni awamu ya sita,
 
Kwa mujibu wa hotuba, kuna mistari inasema 'kuendeleza ujenzi' kuna mstari unasema 'ujenzi ulianza 2019/2020'

Ushauri wangu, tumpongeze mama kwa jitihada zake ila pia tuache kuchonganisha kwa kubadilisha maelezo
 
Kumbuka hii ni awamu ya sita,
Mkoloni alijenga reli, shule, hospitali, barabara,masoko n.k mbona haupongezi?

Kuna vitu havina haja ya kusifia hizo ni huduma na ni jukumu la serikali kuzitoa kutokana na kodi za wananchi.
 
Mtazame Samia kama taasisi sio as an entity,
Jibu swali , kwani wewe ulivyokuja kupiga hapa tarumbeta na vigelegele hukuja kusifia "taasisi" bali an individual

Sasa nijibu swali usihamishe mada.

Samia analipwa kiasi gani?
 
Hivyo, vituo vilijengwa lini? Sio kwamba vilianza kujengwa miaka mingi iliyopita na kukamilika kwenye awamu hii ya Mama?
 
Kuna watu wanateseka bila kuteswaa,

Huyu Mama ni mpango wa Mungu tukubali tukatae,

Mambo anayoyafanya yanatetemesha,
Katiba mpya huenda ikawafungua watanzania ufahamu hata kuelewa wajibu viongozi na serikali kwa wananchi.

Tutapata fursa ya kuona mihimili ikiwajibika na kuwajibishwa. Tutaelewa kuwa miradi ya maendeleo sio kwa hisani ya mtu bali kodi za wananchi na misaada ya wahisani.

Leo tumejivua ufahamu na kuona ajabu pale mtu anapotenda kulingana na wajibu wake.

Watanzania bado hatujafanikiwa kumuondoa adui UJINGA....bado anatuandama
 
Ulipiga kura 2020? Ulimchagua? Kama ulimpa kura yako, huna sababu ya kuuliza ni lazima tu ulisoma Ilani yake. Kama hukumchagua huna sababu ya kuuliza kazi yako subiri 2030.

Ssikiliza hii:
 
Kwa mujibu wa hotuba, kuna mistari inasema 'kuendeleza ujenzi' kuna mstari unasema 'ujenzi ulianza 2019/2020'

Ushauri wangu, tumpongeze mama kwa jitihada zake ila pia tuache kuchonganisha kwa kubadilisha maelezo
Wapi maelezo yamebadilishwa?
 
Kumsema Rais vibaya au vizuri kunategemea mtazamo na uwezo wa kifikra wa anayesema.
Hata hivyo, orodha ya yaliyofanyika uliyoiweka yahitaji kujadiliwa kwa fikra pana zaidi ukizingatia yafuatayo;
1. Kuanzia wakati wa uhuru hadi leo, idadi ya watu wakiwemo wataalamu na wasomi wameongezeka sana hiyo Kasi ya maendeleo lazima iwe kubwa kwa ulinganifu.
2. Uzalishaji umeongezeka hasa kwa sekta binafsi hivyo kodi na mapato mengine ya serikali kuongezeka sana kwa kulinganisha.
 
Mleta mada kwenye uzi wake

Kaandika fedha zimetengwa ili " Kukamilisha".

Halafu anaweka kichwa cha habari kuwa mkamilishaji wa mradi alioukuta ndio kajenga.

Yaani ni sawa na kukamilisha ujenzi wa daraja la Tanzanite.

Awamu hii haijajenga bali inakamilisha ujenzi.

Mleta mada muongo muongo tu
 
Hivi kweli tukae kimya,

Mtu anajenga Zahanati 500,

Mtu anajenga vituo vya afya 300

Mtu anajenga hospitali 70

Tukae kimya eti tukisema tunalipwa,


Shame on you,
Anakamilisha kazi iliyoanza awamu ya tano.

Hakuna kipya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…