Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Dar es Salaam wakati akielekea Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo, tarehe 16 Agosti 2022.
Rais Samia anaenda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Kujua safari zingine za Rais soma hapa.
Picha: Ikulu