Rais Samia aongea na Wazee wa Dar: Aahidi kutojali vyama katika teuzi zake. Serikali kutunza Haki, Demokrasia, Uhuru wa Habari

Wazee wamemkomalia bi mkubwa et vijana hatuwaachii siti kwenye daladala. Aaa kwani sisi vijana tunapanda bure hizo daladala! wazee tumieni pension zenu kununua usafiri na mkiona tunawakera bakini nyumbani mcheze na wajukuu zenu. Hii si awamu ya wanyonge.
 
Amesema wazi kuwa leo hana jambo zito la kuzungumza na wazee kwa maana wazee ndio wamemuomba.
 
"Sisi pia tunakuja huko (uzeeni), hivyo tusipoandaa mazingira nasi pia yatatukuta
 
Kitendo cha Rais kuvaa barakoa ni cha kupongezwa sana utakuwa ni mfano mzuri hasa kwa wale wabishi wa kujikinga na hiki kirusi hatari ambacho kimesababisha maafa makubwa na ya kutisha dunia yote.
usikuze mambo rais katoa sababu kwa nini barakoa zimevaliwa

Rais Samia Suluhu Hassan
Naomba niwaombe radhi kwamba mtindo wa maisha umebadilika. Tumekuja na vikaba midomo ninyi pamoja na sisi

Kwasababu mkusanyiko huu ni mkubwa na Wazee ni rahisi kupata haya maambukizi, hatuwezi kujua nani anayo na nani hana. Sisi wenzenu tunazunguka sana
 
Mama swali ni hilo: na wazee wa umri mkubwa watasimama kuitwa kwa Mungu ili faida ikipatikana wagawiwe?
Kwani wazee hawana ndugu, watoto au wajukuu? Wanafaidika indirect.....
 

Itoshe kusema ukishafika umri wa uzee ni bora ukakae nje ya mji shambani kula upepo tulivu,ukija mjini njoo na Cruiser V8 kutembelea wajukuu.
 
Kwasababu mkusanyiko huu ni mkubwa na Wazee ni rahisi kupata haya maambukizi, hatuwezi kujua nani anayo na nani hana. Sisi wenzenu tunazunguka sana
Ndio Siasa zenyewe hizi ili kuwapoza Mazezeta wa Mwendazake
 
"Ugumu wa maisha sio sababu ya mtu kuwa mwizi, kuna sababu nyingine nyingine huko. Nimesikia hapa, Dar es Salaam watu wameanza kujaribu kina cha maji, wizi na uporaji Umeanza. Nasema wasijaribu na Mkuu wa Jeshi la Polisi kalishughulikie hilo"
 
View attachment 1776541
Jamani, barakoa tele! Maendeleo hayo?
Analeta desturi za Kenya (na za dunia....)?
Ila zinasaidia kiasi tu wakati watu wanabanana ndani ya ukumbi . . .
usipotoshe siyo hivyo rais katoa sababu

Rais Samia Suluhu Hassan
Naomba niwaombe radhi kwamba mtindo wa maisha umebadilika. Tumekuja na vikaba midomo ninyi pamoja na sisi

Kwasababu mkusanyiko huu ni mkubwa na Wazee ni rahisi kupata haya maambukizi, hatuwezi kujua nani anayo na nani hana. Sisi wenzenu tunazunguka sana
 
Wazee wanaoweza kuketi na Rais lazima ni wazee wenye uwezo, hawawezi kuwa wa kiwango cha kuomba msaada kuboreshewa kambi za wazee
 
Ulitegemea asema kuwa nimebadirika kuhusu barakoa? Lazima aseme hivyo ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…