Rais Samia aongea na Wazee wa Dar: Aahidi kutojali vyama katika teuzi zake. Serikali kutunza Haki, Demokrasia, Uhuru wa Habari

Rais Samia aongea na Wazee wa Dar: Aahidi kutojali vyama katika teuzi zake. Serikali kutunza Haki, Demokrasia, Uhuru wa Habari

Wazee wanazidi kuongezeka. Mwaka 2012 kulikuwa na Wazee milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 na hivi sasa wameshafika milioni 2.52.
Atakua anamsema Pole pole

IMG_20210501_071254.jpg
 
Mama atangaze kuhusu wamachinga walioanza kufukuzwa waachwe watafute riziki zao.

Pia ujambazi wa mapanga umerudi Dsm nao auzungumzie amuachie Sirro maagizo na awe mkali kidogo.
Hili hataliweza, namwona si mtu wa kutoa matamko makali kama Mwendazake
 
Leo nimesoma mtandaoni kwamba Dar kuna Watu wanajaribu kupima kina cha Maji, Viujambazi vimeanza kuja juu - Naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha Maji. IGP upo hapa, Mitandaoni wanamtaja Afande mmoja alikomesha ujambazi wanasema Mama turudishie, kaliangalie hilo
 
"Katika suala la kujenga uchumi wa nchi yetu, tutamchukua mtu yeyote hata kama wa vyama vingine mradi tu ana weledi katika uchumi tutamtumia kujenga nchi yetu"
 
"Tutakwenda pia kufanya mabadiliko ya kisera, uongozi na kitaasisi kwa lengo la kuongeza uwajibikaji kwa dhamira ya kuiletea nchi yetu maendeleo"
 
Busara yaelekeza Ukiwa mpangaji mpya Nenda kajitambulisha, Nimekwenda Uganda na nitakwenda na kwingine kutunza ujirani wetu na majirani zetu.
 
Anaongea na wazee wa MKOA wa Dar es Salaam sio jiji mkuu
Kuna mwaka Mkwere naye alisema anaongea na wazee wa dar kumbe aliwasomba na malori toka Bagamoyo
 
wakuu nipo mbali sana,vipi wazee wa Darisalama wameomba katiba mpya+tume huru ya uchaguzi?
 
Promising sio zile ahadi za kila kitu atanya as if budget sio limiting factor, mama sasa anaanza kuongea kama raisi.
 
Back
Top Bottom