BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi Milioni 5 hadi Shilingi Milioni 10 endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Simba ambayo ina uongozi wa 1-0 kutoka mchezo wa kwanza leo Aprili 28 inarudiana na Wydad Casablanca ya nchini Morocco wakati Yanga yenye uongozi wa 2-0 ikitarajiwa kurudiana na Rivers United ya Nigeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam siku ya Jumapili.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais dkt. Samia Suluhu Hassan anazitakia kila la kheri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya kukamilisha robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali ambapo kila goli litakuwa shilingi Milioni 10.
Aidha, Msigwa amesema magoli yatakayolipiwa shilingi Milioni 10 ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.
Pia soma: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF