adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Simba na Yanga kwa serikali ni muhimu sana kwani ni nyezo juu ya kutupumbaza watanzania ,bila kujadili Simba na Yanga wananchi wangewekeza nguvu zao kujadili ripoti ya CAG ,katiba mpya ,bunge ,halinya kiuchumi ,viongozi nk na kuibuka kwa upinzani hadi maandamano .Hizi pesa kama zipo kwanini zisipelekwe kwenye vituo vya kulelea watoto yatima angalau wawe wanakula chakula kizuri kila mara, badala ya kuwasubirisha mpaka siku za sikukuu ndio wapelekewe michele, mbuzi, na mafuta?
Kwasababu hizi Simba na Yanga kwasasa zina wadhamini wakutosha, zinajimudu kwenye mahitaji yao tofauti na miaka ya nyuma walipokuwa wakinywa chai na chapati asubuhi, hata kama serikali ni walezi, muhimu waangalie pazito zaidi kupeleka hayo malezi.
Katika kuneutralize hali Simba na Yanga inaupiga mwingi sana ,mfano leo pita vijiwe vingi ni Simba na Yanga tu na hiyo ni haki ya sikuzote hapo lazima serikali iziangalie hizi klabu kwa jicho la tatu .