Rais Samia aongeza dau, kutoa Tsh. Milioni 10 kwa kila Goli kwa Yanga na Simba (CAFF na CAFCL)

Rais Samia aongeza dau, kutoa Tsh. Milioni 10 kwa kila Goli kwa Yanga na Simba (CAFF na CAFCL)

Hizi pesa kama zipo kwanini zisipelekwe kwenye vituo vya kulelea watoto yatima angalau wawe wanakula chakula kizuri kila mara, badala ya kuwasubirisha mpaka siku za sikukuu ndio wapelekewe michele, mbuzi, na mafuta?

Kwasababu hizi Simba na Yanga kwasasa zina wadhamini wakutosha, zinajimudu kwenye mahitaji yao tofauti na miaka ya nyuma walipokuwa wakinywa chai na chapati asubuhi, hata kama serikali ni walezi, muhimu waangalie pazito zaidi kupeleka hayo malezi.
Simba na Yanga kwa serikali ni muhimu sana kwani ni nyezo juu ya kutupumbaza watanzania ,bila kujadili Simba na Yanga wananchi wangewekeza nguvu zao kujadili ripoti ya CAG ,katiba mpya ,bunge ,halinya kiuchumi ,viongozi nk na kuibuka kwa upinzani hadi maandamano .

Katika kuneutralize hali Simba na Yanga inaupiga mwingi sana ,mfano leo pita vijiwe vingi ni Simba na Yanga tu na hiyo ni haki ya sikuzote hapo lazima serikali iziangalie hizi klabu kwa jicho la tatu .
 
reet.jpg
 
Hapana napinga hii tabia. Michuano ya Simba ni mikubwa inayoshirikisha teams kubwa pekee. Ni ngumu sana kufunga CL kuliko CC. Nadhani kwa Simba ingekuwa 15m na kwa Yanga iwe hiyo 10m
 
Kaona hela zake zitaisha akilipia magoli ya penati 😂😂😂
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi milioni 5 hadi milioni 10 kwa kila goli endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, magoli yatakayolipiwa motisha hiyo (shilingi milioni 10 kila goli) ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.

Rais Samia amezitakia kila la kheri timu hizo na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo yao ya robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali ambapo kila goli litakuwa shilingi milioni 10.

Simba inacheza mchezo wa marudiano leo dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco ikiwa na mtaji wa ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano siku ya Jumapili (kesho kutwa) dhidi ya Rivers United ya Nigeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwa na mtaji wa ushindi wa 2-0 ilioupata ugenini huko nchini Nigeria.

USSR
 
Hizi fedha zinatoka kwenye mfuko gani WA serikali?
 
Kila mwezi ungekuwa unatoa 10mil kwa wanafunzi na graduate wa engineering watakaobuni vitu ambavyo vinaweza kuwa msaada kwenye jamii.
 
Huyu Rais hayupo Sahihi Kabisa
Kwanini hizo pesa asiwasaidie watoto Yatima?
 
Maza amejua makolo safar yao mwisho leo... Kwahiyo ameona Yanga Wananchi waendelee kula m10 kilaini hadi fainali...
 
Back
Top Bottom