Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,914
- 3,386
Awamu ya tano kona kona zilikua nyingi na huu sio wakati wa kumlaumu yoyote, kila mtu anajua propaganda na uongo na maamuzi ya mtu mmoja yalitawala. Wanufaika wakatumia kila njia kuziba mifumo wananchi na kuwatisha kwa kila namna. Kama tukifatilia mienendo ya awamu ya tano ni Rais Samia na Majaliwa walio salama na rushwa na ufisadi wa kutisha uliofanyika.
Awamu ya sita Mama anataka tuishi kwenye ukweli yaani kama tumekosea anasema hapa tumekosea na suluhisho ni hili. Huyu ni Rais pekee ambaye anaenda kuleta maendeleo ya kweli sio uongo uongo kama wa jamaa. Tunaona mkakati wake wa sera ya mambo ya nje akitaka kuongezeka kwa mitaji kutokana na wawekezaji. Ili tupate kodi, ili tutengebeze Ajira, ili tukuze teknolojia, tuongeze uzalishaji na export business na kuleta maisha mazuri kwa wananchi.
Katika kipindi kifupi Rais Samia amefanikiwa sana na projection inaonesha atakua Rais wa kwanza kukuza uchumi kwa kasi zaidi ba kuongeza thamani ya shilingi ya Tanzania.
Nawaonya wanufaika wa awamu ilopita kuwa endeleeni kumpinga Rais na endeleeni kusambaza chuki za wazi wazi. Mmekuwepo serikakini na kwenye chama tunamengi tunayajua tukiamua kufukua makaburi hamtabaki salama. Hivyo kuweni wapole na Rais Samia yuko very powerful and smart anawacheki. Siku akiamua mtalia na kusaga meno, huu sio wakati wa kujenga nchi kwa uongo, uongo.
Ngoja niwambie hakuna awamu ambayo nchi hii itapata maendeleo kama awamu hii ya Rais Samia. Ni Rais pekee ambaye hutumii mihemko wala sifa kufanya maamuzi bali anatumia akili na maarifa.
Watanzania tuna imani kubwa na hakika nchi yetu inakwenda kupata uchumi wa kati wa ukweli kweli sio ule wa propaganda.
Watanzania tumpe muda Rais Samia.