Kila mtu atakubaliana na mimi kuwa nipo sahihi na mzalendo wa kweli.
Pesa za umma zinapotea hovyo, nidhamu serikalini imepotea. Deni la taifa linapaa kama Kunguru.
Mama apishe 2025 yakae majembe yatakayorudisha nidhamu ya kizalendo.
Nawakilisha Mimi Idu wa Igunga.
Halafu inawezekana ukawa mwana CCM wa kwanza uliyegizani usiyefahamu hata kanuni ya umakamu inatokana na vigezo gani!!!!!
Yaani kama Makonda anatenda vizuri kwa sasa kwenye ngazi za chini halafu unampeleka kuwa makamu wa rais utanufaika na kitu gani gani hapo kama kumpoteza?
Makamu wa rais ni kinyago tu cha kuwezesha muungano kuaminishwa kwa wananchi kwamba upo na una uhai.
Sikiliza Rais akitokea bara makamu anatokea visiwani na rais akitokea visiwani makamu anatokea bara.
Kwa pendekezo lako P.Mpango ni Mzanzibari au Mmbara na P.Makonda ni Mzanzibari au Mmbara?
Tunataka rais
1. Anayesema na kutenda kwa haki kwa wnanchi wote bila kuwakandamiza kwa njia yoyote
2. Tunataka rais asiyetumia vibaya madaraka yake kujinufaisha binafsi kwa kuuza, kugawa au kukodisha rasilimali za nchi (umma) bila kuzingatia maslahi ya wananchi ambao ndio wenye dhamana ya uendeshaji kupitia shughuli zao za kiuchumi
3. Tunataka rais mwenye maono ya kuondoa umaskini bila kuwalinda matajiri pekee kwenye biashara zao huku wakiwakandamiza wananchi kutokana na unyonge wao wa kutokuwa na rasilimali fedha, mali na maarifa
4. Tunataka rais anayechukia kwa vitendo maovu yanayotendwa na wananchi wa kawaida, viongozi, wafanya biashara na kutekeleza kutatua kero zao kwa dhati na wenye matendo ya ufisadi, rushwa, unyanyasaji,, dhuluma, ubadhirifu wa mali, matumizi mabaya ya fedha za miradi wanawajibishwa kwa mjibu wa sheria
5. Tunataka rais mpenda watu wa kila ngazi ya hadhi ya ubinadamu, anayewasikiliza moja kwa moja na kuonesha njia ya kutatua kero zao kisiasa na kitaalamu bila kumwonea mtu yeyote
6. Tunataka rais mwenye maono ya kuinua uchumi na kusimamia mapato kwa dhati, kusimamia shughuli za kiuchumi, kijamii, kiusalama, kimahusiano ya kimataifa mazuri na yenye tija kwa nchi, kwa njia ya kujitegemea kupitia rasilimali zilizopo nchini, kuongeza thamani ya mali ghafi zilipo nchini, kuwekeza mitaji kwa wageni na wazawa nchini kisha kuuza bidhaa zilizozalishwa zikiwa zimeongezwa tamani hivyo kupata dola
7. Tunataka rais asiyekwapua mali za umma kwa faida yake binafsi, rafiki zake nk
8. Tunataka rais mzalendo halisi na mwenye uchungu na rasilimali za nchi na hali duni ya wafanyakazi, wakulima, wafanya biashara wazawa, wanafunzi, watoto, watu wazima, wazee, wagonjwa nk na atatue kero na mapungufu hayo kiukweli sio kisiasa