Kuna usemi kwamba "Ya kale ni dhahabu. Model ya Magufuli itakumbukwa daima" Mama alipochukuwa nchi alisema hataki watu kuonewa akawaachia huru mafisadi waliowekwa ndani na serikali ya Magufuli (japo ela za Plea Bargaining zilizokuwa kwenye subira ya mchakato wa kisheria kuliwa nyuma ya Magufuli kufariki).
CAG Assad alipumzishwa kwa ripoti kama hizi hizi za CAG Kichere. Sijajuwa kama Kichere ataendelea kuvumiliwa hadi lini.
Mama hata kama hapendi mafisadi walio kwenye ripoti ya Kichere kushughulikiwa (kuonewa) lakini tayari CCM kimeshindwa kuvumilia na kuagiza serikali kuwachukulia hatua wahusika wote.
Pasina kujali udhaifu wa Mhimili wa Mahakama yetu lijapo suala la rushwa katika kufanya maamuzi ya mashauri, ni dhahiri kwamba mama sasa ana kigugumizi cha ni kwa vipi nilitoa mafisadi jela alafu leo tena niwarudishe jela ama wale wale au hata kama ni mafisadi wapya!
Huu ni mfupa mgumu kwa mama na huenda hata kwa CCM kilichompa maagizo kuwachukulia hatua za kisheria.
Dondoo chache kwenye ripoti ya CAG 2022 - 2023:
1. TTCL imekopesha watu wasiojulikana 21 bl.
2. Mkurugenzi Mkuu na maafisa wengine waandamizi wa TPA ambao wote waliondolewa kazini kwa utendaji mbovu bado wanaendelea kuidhinisha malipo kwenye mfumo wa TPA.
3. Takriban V8 mpya 40 za serikali zilizoagizwa zimeyeyuka bandarini.
4. CAG hakusaini (alirukwa) baadhi ya mikataba ya manunuzi makubwa ya kimkakati ughaibuni kama sheria inavyotaka.
Kwa ripoti hii ya CAG Kichere nchi inaenda wapi wakati wapigakura wanakula mlo mmoja? Mchele mbovu (chenga 3,100/)
Tujadili kwa ustaarabu kwa kujifunza kitu siyo kwa kushindana maana nchi ni yetu sote.