The right option ni status quo.
CHADEMA washiriki uchaguzi kama utakavyokuwa kama hapo awali.
Manufaa ya CDM kushiriki:
1. CCM, serikali na vyombo vya dola watasota kuiba uchaguzi, kukimbizana na masanduku ya kura, kupiga wananchi virungu, na kukesha kufuatilia nyendo za wagombea, viongozi, na wafuasi wa CDM. Watashuhudiwa na umma wa Watanzania na wadau duniani.
2. CCM wataendelea kuipata saikolojia ya kuzidiwa kura na CDM kwa kushuhudia kura halisi vs matokeo ya mchongo wanayotangaza. Wao ndio huwa wanaoiona hesabu halisi ya kura.
3. CDM pamoja na kudhulumiwa, nafasi yao katika siasa na upinzani wa kulazimishwa itakuwa juu tu: watapata wabunge wengi, madiwani, etc. Hii ni pamoja na kufaidika kiuchumi kwa chama na wanaoshinda uchaguzi (individuals). Uhai wa chama ni muhimu.
Hasara za CDM kushiriki:
1. Wananchi kuibiwa uchaguzi wao (hata bila ya ushiriki wa CDM). 2. Vipigo, Majeruhi na hata vifo kuongezeka kutokana na jazba ya CCM na vyombo vya dola kukamia kuzuia umaarufu na ushindi wa CDM. 3. Matumizi ya kutisha ya pesa za umma kununua wagombea na viongozi wa CHADEMA kutafuta kupunguza au kuondoa ushindani; kuhonga wapiga kura pesa, nguo, chakula, pombe, usafiri, n.k.; ufisadi mkubwa kwa wanaoshika hizo pesa.
CHADEMA wameshafanya kazi kubwa kuwapigania Watanzania haki zao. Kama wananchi hawaamki na kuunga mkono mapambano basi wao CDM waendelee kuithibitisha nafasi yao katika jamii na kujikusanyia chao toka kwenye keki ya taifa ili wasife. Kila mtu ajijue kivyake hadi siku watu watakaporejewa na fahamu kuwa nchi inaelekea kuzimu.
CDM wasiposhiriki kwa jinsi nchi hii ilivyo watapotea kabisa! Na ndio lengo kuu la CCM. CCM inafanya mapambano ya attrition (kuwakatisha tamaa na kuwachosha wapinzani wa kweli hadi waachane na mapambano). Rejea kilichomtokea Halima Mdee na Covid 19, Nasari, etc. Wamelegezwa bila kutaka! Sad!
CCM wamefanikiwa kuwachosha Watanzania hadi political apathy imetamalaki. Sasa hivi nguvu zote zinaelekezwa CHADEMA. Ndilo changamoto kuu lililobakia. Na inaaminika Mbowe ndio tatizo kubwa kuliko hata Lissu katika kuvunja will ya CDM. Fuatilia kelele za JF.