kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nilimsikia Rais wetu Samia Suluhu akithamanisha uwepo wake kama Rais Mwanamke katika kuvutia vitega uchumi toka nje. Hiki ni kiinimacho tusije ruhusu uwekezaji usio na tija kwa maendeleo ya nchi.
Lengo letu sio kua na wawekezaji wengi tu. Samia asije legeza kamba akaanza kutoka kwenye misingi ya uwekezaji iliyowekwa na awamu ya tano.
Uwekezaji uwe ule wenye manufaa na nchi na mwekezaji 50/50 na isiwe kudumaza maendeleo ya wenyeji huku ukitajirisha wageni kwa mali asili au ghafi ya nchi yetu.
Wawekezaji potential wanaosifu mabadiliko ya rais huku wakimpiga vijembe mtangulizi wake ajue ni wale wenye kutaka masharti laini yenye kuwapendelea. Pia hawapendi uongozi imara wa nchi wenye kulinda maslahi ya wananchi wake.
Mzee ruksa alisema awamu yake alisimamia uchumi toka kuendeshwa na dola kwenda kutegemea sekta binafsi. Kwa hivyo milango ilipofunguliwa kwa uwekezaji binafsi waliingia pia wadudu wabaya akiwa na maana waliyotuumiza kiuchumi na wababaishaji.
Tulishapita huko saa hizi tumefikia mahali tunakaribisha wawekezaji wenye tija kwa maendeleo ya nchi na watu wetu.
Rais wetu awe makini asije yumba.