Rais Samia asisitiza kwa mara nyingine "hakuna kumuweka mtu mahabusu kama upelelezi haujakamikika"

Rais Samia asisitiza kwa mara nyingine "hakuna kumuweka mtu mahabusu kama upelelezi haujakamikika"

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Nawasalimu kwa JMT,

Mnyonge hanyongwi na haki anapewa.

Rais SSH kwa mara nyingine amesisitiza kwa Polisi kwamba ni Marufuku kumuweka mtu ndani yaani Mahabusu Kama Upelelezi Haujakamikika. Hii ni mara ya pili anaongea jambo hili na ameshaliweka kwenye sheria za Polisi.

Ni nadra sana hapa duniani kupata kiongozi anayejali haki, wengi wa waliopo kwenye jamii mnajua ni makatili kama wale waliopita. Hapa chadomo hutowakuta ila angekuwa ka tweet yule Rais wa Twitter kutoka Zambia wangeshajaza nyuzi 😃😃.

Asante sana Rais Samia 👇

Screenshot_20220830-162011.png
 
Angeongeza kuwa atakaemweka ndani mtu ikabainika basi yeye ndio afungwe
Kama ni Sheria na iwe hivyo maana tunaona hawaelewi
 
Hilo ni jambo jema, lakini je, ni kweli sheria hiyo itafuatwa!? Au kauli za mama jeshi linachukulia poa tu! The same as anaimba taarabu za mipasho.
 
Sasa kama polisi wanaweka mtu ndani bila kosa lolote, watafuatilia hilo kweli. Shida nyingine ni kua PT wengi (asilimia kubwa) hawajui sheria na wala hawataki kujifunza sheria walau kidogo.
 
Kauli zake kama hizi,watendaji wangegeuza yaani ziwe zinazikika kama za JPM,hakika hakuna ambaye angewekwa mahabusu.Yaani ingekua laivu JPM anaongea,tena kwa msisitizo,aisee ni saluti tu zingekua zinamwagika kutoka kwa IGP,kuonyesha haitatokea mtu kuwekwa mahabusu kabla ya upelelezi kukamilika.R.I.P Mzee.
 
Haibadirishi kitu hii tutaendelea kuminywa kende na kesi kutokamilika uchunguzi hadi kiama
 
Kwani wanamuogopa? Kaongea mangapi hadi sasa?
Wewe unayajua mangapi aliyoagiza hadi sasa na hayajatekelezwa?

Mwisho kama jambo linakiuka sheria hakuna atakayeyekeleza kwa sababu liko kwenye sheria hadi wabadili sheria.
 
Back
Top Bottom