Rais Samia asisitiza kwa mara nyingine "hakuna kumuweka mtu mahabusu kama upelelezi haujakamikika"

Rais Samia asisitiza kwa mara nyingine "hakuna kumuweka mtu mahabusu kama upelelezi haujakamikika"

Nasema hivi mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Atakumbukwa na kutumika Kama Rejea wa mfano wa kiongozi Bora kuwahi kutokea kwa miaka ya hivi karibuni katika Bara la Afrika, Ni kiongozi mwenye hofu ya mungu na mwenye upendo wa dhati kwa wale awaongozao na kuwatumikia
 
Huyu mama nae aache siasa katika fani za watu

Mshitakiwa akiwa nje upelelezi unakuwa mgumu maana atakuwa na uwezo wa kuziba mianya yote muhimu katika kufanya upelelezi
 
Ukisikiliza hii clip utaona kuna mambo mengi yaliyozungumzwa yalipaswa kuwa katika vikao vya ndani na ma ofisa.

Mmh! Vikao vya ndani kwa sababu gani? Bila kuwa kwenye vikao vya ndani hao maofisa huwa hawaelewi ama ni nini?
 
Ukisikiliza hii clip utaona kuna mambo mengi yaliyozungumzwa yalipaswa kuwa katika vikao vya ndani na ma ofisa.

Halafu watu wengine wanacheka tu,ndiyomaana Sirro alikua anamtolea shit,mengine unawaambia maofisa tu,kazi inaisha.
 
Hawatatekeleza,mark my words.
Huyu mama nae aache siasa katika fani za watu

Mshitakiwa akiwa nje upelelezi unakuwa mgumu maana atakuwa na uwezo wa kuziba mianya yote muhimu katika kufanya upelelezi
 
Huyu mama nae aache siasa katika fani za watu

Mshitakiwa akiwa nje upelelezi unakuwa mgumu maana atakuwa na uwezo wa kuziba mianya yote muhimu katika kufanya upelelezi

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Inawezekana hujaelewa. Kinachosemwa ni kuwa at least kuwe na evidence. Watu wengi wanakamatwa tu bila ushahidi wowote wanawekwa tu ndani wanapotezewa muda kisha wanaachiwa bila kupelekwa mahakamani.

Hizo fani za watu ni pamoja na kufanya upelelezi bila kumpa mwanya mshukiwa wa kuharibu upelelezi. Hii inawezekana.
 
Sijajua lakini ni kama umetumwa.....

Kwanini nasema hivyoo...., ni kinana nani wamepitaa ..? Na walikuwa na roho mbaya gani??..... na kama umefikiria haya wewe! Mkuu we have a long way to go.

Tulijenge Taifa kwa hojaa tunduizi....
 
Bila executive order na kuitangaza kwenye gazeti la serikali au kubadilisha PGO - anachofanya kwa “kupiga marufuku” haina tofauti na wale wanazuia ushuru wa mazao huku barabara zote zina vizuizi wakisisitiza kukusanya ushuru kwa sababu halmashauri haijaondoa agizo hilo la kisheria!!

Kama kweli anakusudia kumaliza uonevu huu - atoe executive order au waziri wa mambo ya ndani apeleke mswada Bungeni ili iwe sheria baada ya Rais kuisaini.

Otherwise kilichofanyika hapa kutoa maneno yanayoonesha huruma tu. Amri ya Rais sio maneno tu jukwaani, kisheria!!
 
Uko sahihi, Mwendazake aliwahi sema hilo la Mazao lakini watu walitozwa kama Kawa na wanakutoza huku wakikwambia mfuate Ikulu ukamwambie au acha mazo yako hapa msubirie aje akulipie 😁😁
 
Kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti atende kwanza ndipo aseme
 
Nawasalimu kwa JMT..

Mnyonge hanyongwi na haki anapewa..

Rais SSH kwa mara nyingine amesisitiza kwa Polisi kwamba ni Marufuku kumuweka mtu ndani yaani Mahabusu Kama Upelelezi Haujakamikika..

Hii ni mara ya pili anaongea jambo hili na ameshaliweka kwenye sheria za Polisi..

Ni nadra Sana hapa Duniani kupata Kiongozi anayejali haki,wengi wa waliopo kwenye jamii mnajua ni makatili kama wale waliopita..

Hapa Chadomo hutowakuta ila angekuwa ka tweet yule Rais wa Twitter kutoka Zambia wangeshajaza nyuzi 😃😃..

Asante Sana Rais Samia 👇
Amesema nani ahakiki Hilo utimizwa? Au ni polisi kujiangalia menyewe kwa menyewe tu?
 
Nawasalimu kwa JMT..

Mnyonge hanyongwi na haki anapewa..

Rais SSH kwa mara nyingine amesisitiza kwa Polisi kwamba ni Marufuku kumuweka mtu ndani yaani Mahabusu Kama Upelelezi Haujakamikika..

Hii ni mara ya pili anaongea jambo hili na ameshaliweka kwenye sheria za Polisi..

Ni nadra Sana hapa Duniani kupata Kiongozi anayejali haki,wengi wa waliopo kwenye jamii mnajua ni makatili kama wale waliopita..

Hapa Chadomo hutowakuta ila angekuwa ka tweet yule Rais wa Twitter kutoka Zambia wangeshajaza nyuzi [emoji2][emoji2]..

Asante Sana Rais Samia [emoji116]
Unaandika huku unaiwaza CHADEMA !!
Hiyo mimba ya CHADEMA itoe itakuuwa...
 
Huyu mama nae aache siasa katika fani za watu

Mshitakiwa akiwa nje upelelezi unakuwa mgumu maana atakuwa na uwezo wa kuziba mianya yote muhimu katika kufanya upelelezi

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Siokweli......
Shida kubwa ni elimu...na ndio maana umeona limetengwa fungu kwa kazi hiyo.
 
Sasa kama polisi wanaweka mtu ndani bila kosa lolote, watafuatilia hilo kweli. Shida nyingine ni kua PT wengi (asilimia kubwa) hawajui sheria na wala hawataki kujifunza sheria walau kidogo.
Ndugu yangu inawezekana labda kule CCP siku hizi, pengine somo la GPO halifundishwi ipasavyo na ndo maana unakuta matatizo mengi ktk utendaji wa polisi huwa yanaanzia hapo ..... kazi kwelikweli...
 
Hapo shida inaanzia kwenye watunga sheria.
Wao hawajasema Makosa yote Kuna baadhi ya Makosa wameyaacha katika utaratibu wa zamani.
Mifumo hii tumeirithi kutoka Kwa wakoloni hata nchi za mabeberu nazo zimegawanyika katika mifumo tofauti tofauti Adversarial system na inquisitorial system.

Kwa Aina ya watu Wetu Adversarial system inatufaa zaidi kwasababu UKIFANYA utafiti mahakamani watuhumiwa walioruka dhamana ni zaidi ya asilimia 40 Kuna hatari haki za watu zikazidi kupotea zaidi.

Muhimu ni KUWASIMAMIA Polisi Wetu watende haki wasibambikize kesi.
Watuhumiwa wanaoonewa wabainike mapema ikiwezekana ndani ya masaa 24 kuwepo Pia check and balance ndani ya jeshi Hilo.
 
Nawasalimu kwa JMT..

Mnyonge hanyongwi na haki anapewa..

Rais SSH kwa mara nyingine amesisitiza kwa Polisi kwamba ni Marufuku kumuweka mtu ndani yaani Mahabusu Kama Upelelezi Haujakamikika..

Hii ni mara ya pili anaongea jambo hili na ameshaliweka kwenye sheria za Polisi..

Ni nadra Sana hapa Duniani kupata Kiongozi anayejali haki,wengi wa waliopo kwenye jamii mnajua ni makatili kama wale waliopita..

Hapa Chadomo hutowakuta ila angekuwa ka tweet yule Rais wa Twitter kutoka Zambia wangeshajaza nyuzi [emoji2][emoji2]..

Asante Sana Rais Samia [emoji116]
Rais hahitaji kusisitiza. Anahitaji kuchukua hatua kwa Mtanzania mwajiriwa wake ambaye hafuati maagizo yake. Msaidieni Rais wetu atimize wajibu wake.
 
Nimegundua huyu ni mtu na nusu na hapaswi kulaumiwa Kwa sababu zozote. Rais huyu ni wa pekee japo ni binadamu. Na sisi binadamu huwa ni vigumu kuridhika hata mtu angefanyaje. Kwa hulka yetu ukipewa wali nyama utaanzisha maandamano ya kudai mchuzi, na ukipewa mchuzi unaanzisha maandamano ya kudai kachumbari, na ukipewa kachumbari kuna maandamano ya kudai chumvi. Hiyo ni hulka yetu wanadamu hatujui neno Asante hata Kwa kile tunachopata.

Rais anaeleza vitu mpaka unamuona kabisa anaumia huyu !! Mahabusu magerezani wanakula ugali wa Serikali kwa kesi ambazo hazina ushahidi wowote

Nilijua ni Rais anaagiza watendewe hivyo kumbe hapana, mama yetu na yeye anaumia na hajui ni kwanini;
Nimegundua wasaidizi wa Rais ndio wanaoharibu taswira na Nia yake njema. Jamani tumheshimuni huyu mama kabla hajaondoka , huyu inaonekana atatuletea nafuu nyingi sana.

DPP anaweka mtu ndani mpaka miaka miwili na kesi haijulikani ni ipi..narudia Tena tumheshimu huyu malaika mungu katupa .mama huyu akiendelea hivi nawambieni tutapiga hatua kubwa sana. SAMIA SULUHU HASSANI sitakulaumu Tena .umenikuna na nimekunikaaa.

Sasa tuanze na Hawa waliojaza magereza na ushahidi hamna, watolewe kwanza mpaka ushahidi utakapo kamilika . Samia suluhu hoyeee !! Najua wavimba macho mtakuja kunichamba hapa ila mwambieni huyu mama Nina jogoo wake hapa kipatimo juu ,msigwa njoo umchukulie mama zawadi yake akachemshe supu Kwa kazi nzuri .. mwambieni Mimi nimekunika sanaaaaa !
 
Back
Top Bottom