Nimegundua huyu ni mtu na nusu na hapaswi kulaumiwa Kwa sababu zozote. Rais huyu ni wa pekee japo ni binadamu. Na sisi binadamu huwa ni vigumu kuridhika hata mtu angefanyaje. Kwa hulka yetu ukipewa wali nyama utaanzisha maandamano ya kudai mchuzi, na ukipewa mchuzi unaanzisha maandamano ya kudai kachumbari, na ukipewa kachumbari kuna maandamano ya kudai chumvi. Hiyo ni hulka yetu wanadamu hatujui neno Asante hata Kwa kile tunachopata.
Rais anaeleza vitu mpaka unamuona kabisa anaumia huyu !! Mahabusu magerezani wanakula ugali wa Serikali kwa kesi ambazo hazina ushahidi wowote
Nilijua ni Rais anaagiza watendewe hivyo kumbe hapana, mama yetu na yeye anaumia na hajui ni kwanini;
Nimegundua wasaidizi wa Rais ndio wanaoharibu taswira na Nia yake njema. Jamani tumheshimuni huyu mama kabla hajaondoka , huyu inaonekana atatuletea nafuu nyingi sana.
DPP anaweka mtu ndani mpaka miaka miwili na kesi haijulikani ni ipi..narudia Tena tumheshimu huyu malaika mungu katupa .mama huyu akiendelea hivi nawambieni tutapiga hatua kubwa sana. SAMIA SULUHU HASSANI sitakulaumu Tena .umenikuna na nimekunikaaa.
Sasa tuanze na Hawa waliojaza magereza na ushahidi hamna, watolewe kwanza mpaka ushahidi utakapo kamilika . Samia suluhu hoyeee !! Najua wavimba macho mtakuja kunichamba hapa ila mwambieni huyu mama Nina jogoo wake hapa kipatimo juu ,msigwa njoo umchukulie mama zawadi yake akachemshe supu Kwa kazi nzuri .. mwambieni Mimi nimekunika sanaaaaa !