Rais Samia atakuja kushinda tuzo ya Kiongozi Bora ya Mo Ibrahim

Rais Samia atakuja kushinda tuzo ya Kiongozi Bora ya Mo Ibrahim

Mo Ibrahim Leadership Prize ni tunzo anayopewa kiongozi msataafu aliyetumikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi miongoni mwa nchi za Kiafrika, na katika uongozi wake aliheshimu na kuruhusu demokrasia, akasimamia utawala bora na kuondoka madarakani kwa kuheshimu mihula ya kiuongozi na kukabidhi madaraka kwa anayemfuatia.

Mpaka Sasa, Rais Samia ni miongoni mwa marais wachache katika Afrika ambaye ameweza kuweka mizania nzuri ya kusimamia mabadiliko ya kiuchumi, demokrasia, utawala bora na uimrishaji wa huduma za jamii. Kama ataendelea hivi na kuruhusu uchaguzi huru na wa haki hapo 2025 na akaondoka madarakani kwa misingi hiyo, bila shaka atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashabiki na Kati kutwaa tuzo hiyo.

Hapana ubishi kuwa kasi ya Samia katika ujenzi na uimarishaji wa huduma za kijamii hususan elimu, maji na afya haina mfanowe kwa Sasa. Maudhui ya taarifa za habari hususan ITV katika kipindi takribani mwaka Sasa, ni juu ya utekelezaji au uzinduzi wa miradi mbalimbali ya elimu, afya na maji.

Chapa Kazi mama, kazi iendelee.
Atashinda tu na hilo liko wazi, labda wafanye figisu ila tayari ameishashinda mtake msitake. Rs zake zinampa Ushindi mnono
 
I don't think so. Ile tuzo wanapewa rais madarakani maskini. Rais Samia ni filthy rich--- with all those Arab friends.
 
..Ccm hata akiteuliwa mwenye akili na maadili yasiyo na shaka mfumo wao wa utawala utamharibu tu.

..Mwenyekiti wa Ccm ni Amiri Jeshi Mkuu mwenye madaraka ya ki-mungu mtu.

..Madaraka hayo makubwa kupita kiasi kwa za humlevya mwenyekiti wa Ccm, na pili huwafanya wa chini yake wamtii bila kumhoji.
Sasa tatizo linakuwa kubwa sana pale ambapo viongozi walioteuliwa kuongoza vyombo vya dola wanakuwa wale wa kushikiwa fikra.
Kama wangekuwa watu wenye akili na fikra huru wangemshauri kiongozi mkuu kwa faida na mustakabali mwema wa taifa.
 
..tatizo ni liko kwenye KATIBA.

..viongozi wa vyombo vya dola wanateuliwa na Mwenyekiti wa Ccm ambaye ni Raisi.

..lakini nafasi za viongozi hao hazina kinga yoyote ya kikatiba kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila kuingiliwa na Mwenyekiti wa Ccm / Raisi.
 
Mo Ibrahim Leadership Prize ni tunzo anayopewa kiongozi msataafu aliyetumikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi miongoni mwa nchi za Kiafrika, na katika uongozi wake aliheshimu na kuruhusu demokrasia, akasimamia utawala bora na kuondoka madarakani kwa kuheshimu mihula ya kiuongozi na kukabidhi madaraka kwa anayemfuatia.

Mpaka Sasa, Rais Samia ni miongoni mwa marais wachache katika Afrika ambaye ameweza kuweka mizania nzuri ya kusimamia mabadiliko ya kiuchumi, demokrasia, utawala bora na uimrishaji wa huduma za jamii. Kama ataendelea hivi na kuruhusu uchaguzi huru na wa haki hapo 2025 na akaondoka madarakani kwa misingi hiyo, bila shaka atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashabiki na Kati kutwaa tuzo hiyo.

Hapana ubishi kuwa kasi ya Samia katika ujenzi na uimarishaji wa huduma za kijamii hususan elimu, maji na afya haina mfanowe kwa Sasa. Maudhui ya taarifa za habari hususan ITV katika kipindi takribani mwaka Sasa, ni juu ya utekelezaji au uzinduzi wa miradi mbalimbali ya elimu, afya na maji.

Chapa Kazi mama, kazi iendelee.
Hawezi kuipata kwa sababu kadhaa za kiuchumi, hasa kutokana na ongezeko la watanzania walioingia kwenye dimbwi la umaskini.
 
Madam akiweka Katiba tu atavuta pesa ndefu badala ya kuendelea na temporary glory ya kutaka eti chama fulani Kibaki mahali fulani

Katiba ni takwa linaloheshimika duniani

Nafasi hiyo anayo labda ashindwe mwenyewe nadhani hata wale jamaa wa visima kule pembeni watashukuru sana kuwa mama yao kutendea haki nafasi aliyopewa

Sukuma gang wamekwama kabisa kuipata hii na imepita hairudi
Pesa ndefu kutoka wapi? PRIMITIVE MINDSET, , yaan mpewe pesa kisa kutimiza agenda za kuwapendeza wamagharibi? Hizi akili za kupewa pewa mmejazwa na hao viongozi wenu wapumbavu ambao waasisi wa mataifa ya afrika na wapigania uhuru walikataa huo upumbavu.

Nikajua mtasema rais awaunganishe wanasiasa ili wajenge uchumi pamoja bila kubaguana kumbe mijitu inapambana kuipamba demokrasia ili mupate sifa za mabwana zenu.

Kwa akili kama hizi tusitegemee Africa kuja kuendelea hususan kwa black race, maana ujinga na upumbavu bado uko akilini mwa wengi.

Amkeni enyi wapumbavu
 
Hiyo Tuzo haina faida kwa Taifa labda kwa huyo kibaraka wao anaefuata kanuni za hao wagawa mikopo.

Kila nchi ina tamaduni na kanuni zake za uongozi, mnapoforce taifa fulan litumie kanuni za taifa lingine kiuongozi hapo ndipo mnapokosea, huyo mamaenu hata akitimiza hayo mapambio yenu, kama taifa halitopata lolote zaid ya umasikini kuongezeka, pambaneni kuwasomesha watoto zenu waelimike wasijekufuata akili zenu na za hawa viongozi wetu wa kisiasa na vyama vyote vya kipuuzi puuzi.

Ubora wa kiongozi haupimwi kwa kuifurahisha jamii za mbali ama kanuni za mataifa mengine...

Wake up guys
 
Hawezi kuipata kwa sababu kadhaa za kiuchumi, hasa kutokana na ongezeko la watanzania walioingia kwenye dimbwi la umaskini.
Unapoondoa watu makazini, unapofunga biashara zao, unapochukua pesa kwenye akaunti zao, unapowanyang'anya mazao yao unatarajia nini kitatokea kwenye uchumi? Tena tuna bahati angekuwepo mwenye sera hizo hali ya umaskni ingekuwa mbovu Zaidi. Samia hawezi kuhukumiwa kwa janga lililoasisiwa na mtangulizi wake.
 
Back
Top Bottom