Rais Samia atakuja kushinda tuzo ya Kiongozi Bora ya Mo Ibrahim

Atashinda tu na hilo liko wazi, labda wafanye figisu ila tayari ameishashinda mtake msitake. Rs zake zinampa Ushindi mnono
 
I don't think so. Ile tuzo wanapewa rais madarakani maskini. Rais Samia ni filthy rich--- with all those Arab friends.
 
Sasa tatizo linakuwa kubwa sana pale ambapo viongozi walioteuliwa kuongoza vyombo vya dola wanakuwa wale wa kushikiwa fikra.
Kama wangekuwa watu wenye akili na fikra huru wangemshauri kiongozi mkuu kwa faida na mustakabali mwema wa taifa.
 
Sasa tatizo linakuwa kubwa sana pale ambapo viongozi walioteuliwa kuongoza vyombo vya dola wanakuwa wale wa kushikiwa fikra.
Kama wangekuwa watu wenye akili na fikra huru wangemshauri kiongozi mkuu kwa faida na mustakabali mwema wa taifa.

..tatizo ni liko kwenye KATIBA.

..viongozi wa vyombo vya dola wanateuliwa na Mwenyekiti wa Ccm ambaye ni Raisi.

..lakini nafasi za viongozi hao hazina kinga yoyote ya kikatiba kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila kuingiliwa na Mwenyekiti wa Ccm / Raisi.
 
Hawezi kuipata kwa sababu kadhaa za kiuchumi, hasa kutokana na ongezeko la watanzania walioingia kwenye dimbwi la umaskini.
 
Pesa ndefu kutoka wapi? PRIMITIVE MINDSET, , yaan mpewe pesa kisa kutimiza agenda za kuwapendeza wamagharibi? Hizi akili za kupewa pewa mmejazwa na hao viongozi wenu wapumbavu ambao waasisi wa mataifa ya afrika na wapigania uhuru walikataa huo upumbavu.

Nikajua mtasema rais awaunganishe wanasiasa ili wajenge uchumi pamoja bila kubaguana kumbe mijitu inapambana kuipamba demokrasia ili mupate sifa za mabwana zenu.

Kwa akili kama hizi tusitegemee Africa kuja kuendelea hususan kwa black race, maana ujinga na upumbavu bado uko akilini mwa wengi.

Amkeni enyi wapumbavu
 
Hiyo Tuzo haina faida kwa Taifa labda kwa huyo kibaraka wao anaefuata kanuni za hao wagawa mikopo.

Kila nchi ina tamaduni na kanuni zake za uongozi, mnapoforce taifa fulan litumie kanuni za taifa lingine kiuongozi hapo ndipo mnapokosea, huyo mamaenu hata akitimiza hayo mapambio yenu, kama taifa halitopata lolote zaid ya umasikini kuongezeka, pambaneni kuwasomesha watoto zenu waelimike wasijekufuata akili zenu na za hawa viongozi wetu wa kisiasa na vyama vyote vya kipuuzi puuzi.

Ubora wa kiongozi haupimwi kwa kuifurahisha jamii za mbali ama kanuni za mataifa mengine...

Wake up guys
 
Hawezi kuipata kwa sababu kadhaa za kiuchumi, hasa kutokana na ongezeko la watanzania walioingia kwenye dimbwi la umaskini.
Unapoondoa watu makazini, unapofunga biashara zao, unapochukua pesa kwenye akaunti zao, unapowanyang'anya mazao yao unatarajia nini kitatokea kwenye uchumi? Tena tuna bahati angekuwepo mwenye sera hizo hali ya umaskni ingekuwa mbovu Zaidi. Samia hawezi kuhukumiwa kwa janga lililoasisiwa na mtangulizi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…