Rais Samia atangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
Muda wowote baraza jipya....... stay tuned

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua @Nnauye_Nape kuwa Waziri wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua @HusseinBashe kuwa Waziri wa Kilimo na @AnthonyMavunde kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amembadilisha @ummymwalimu kuwa Waziri wa Afya akitoka @OR_TAMISEMI

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Mhandisi Hamad Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi na @ridhiwankikwete kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemhamisha George Simbachawene kwenda Wizara ya Katiba na Sheria

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Mhandisi Hamad Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Profesa Adolf Mkenda kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akichukua nafasi ya Profesa Joyce Ndalichako.

Rais Samia Suluhu amemteua Prof Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu





#MabadilikoBarazaLaMawaziri
Lengo lake la kumridhisha kikwete limetimia
 
Masauni ni wa znz pia
naona huu mwaka spika nae atoke tu znz
Waziri mkuu nae znz!

Hivi akina Kabudi, Mkuvi na wengine hata Majaliwa
si wajitoe ccm?
Kweli hii nchi imekuwa genge sasa!

Upinzani hii ndiyo nafasi pekee ya kuingia Ikulu
huenda Mungu amejibu maombi yenu
Cha msingi mleteni mtu sahihi!
 
Nilisema jana kwamba samia hana option ya kupata mawaziri nje ya type ya mawaziri anaofanyanao kazi sasa.

Wote ni type moja tu.
mwisho wa siku ni kurudia teuzi zilezile.

Ukimtosa ndugulile utarudi kumwibua kigwangala.

Ukimtosa simbachawene utajikuta umemrejesha mavunde & etc

Circle ni ileile.naona pindi chana amerejea tena.

Nakumbuka jakaya, ndani ya awamu yake alijikuta ameteua mawaziri takribani 90+ kama sio 100.
 
Muda mfupi ujao Mabadiliko ya Baraza la mawaziri yanatarajiwa kutangazwa kutoka Ikulu Jijini Dar es salaam.

======

Rais Samia amebadilisha muundo wa Wizara Tatu, Ameunganisha Wizara ya Uwekezaji iliyokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa Wizara Moja ambayo itaitwa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya mwisho aliyoifanyia mabadiliko ni Wizara ya Afya

Uteuzi (Mawaziri Wapya):

Nape Moses Nnauye - Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hamad Masauni - Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi

Dkt. Pindi Chana - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Dkt. Angelina Mabula - Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hussein Bashe - Waziri wa Kilimo

Manaibu:
Anthony Mavunde - Kilimo

Jumanne Abdallah Sagini - Mambo ya Ndani

Dr. Lemomo Ole Kiruswa - Madini

Ridhiwani Kikwete - Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Atupele Mwakibete - Ujenzi na Uchukuzi (Upande wa Uchukuzi)


Mabadiliko ya Mawaziri:

Jenista Mhagama - Utawala Bora

Ummy Mwalimu - Afya

George Simbachawene - Katiba na Sheria

Profesa Joyce Ndalichako - Waziri wa Kazi

Innocent Lugha Bashungwa - TAMISEMI

Profesa Adolf Mkenda - Wizara ya Elimu

Dkt. Dorothy Gwajima - Wanawake, Jinsia na Makundi Maalum

Mohammed Mchengerwa - Utamaduni na Michezo

Dkt. Ashatu Kijaji - Uwekezaji


Mawaziri Walioachwa

Palamagamba Kabudi - Alikuwa Wizara ya Katiba na Sheria

William Lukuvi - Alikuwa wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi

Kitila Mkumbo - Alikuwa Wizara ya Viwanda na Biashara

Geoffrey Mwambe - Alikuwa Wizara ya Uwekezaji

=====

Kwa Ufupi;

Ikulu

Mkuchika

Utumishi
Mhagama
Ndejembi

Tamaisemi
Bashungwa
Silinde
Festo

Makamu wa Rais
Jafo
Hamis Hamis


Sera Bunge
Pindi Chana
Nderiananga

Ajira na kazi
Ndalichako
Katambi

Fedha
Mwigulu
Chande

Ulinzi
Tax

Ndani
Masauni
Sagini

Katiba
Simbachawene
Pinda

Mambo ya Nje
Mulamula
Mbaruku

Kilimo
Bashe
Mavunde


Mifugo
Mashimba
Ulega

Ardhi
Mabula
Kikwete

Maliasili
Ndumbaro
Masanja

Nishati
Makamba
Byabato

Madini
Biteko
Kiluswa

Ujenzi
Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya

Viwanda
Kijaji
Kigahe

Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel


Elimu
Mkenda
Kipanga

Maendeleo ya kamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis

Maji
Jumaa aweso
Mahundi

Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

Habari Mawasiliano
Nape Nnauye
Kundo Mathew
Marwa Waitara yule Mlevi yu wapi?
 
Kiukweli nadhani kwa miaka ya hivi karibuni nchi hii haukuwahi kuwa na Waziri wa ardhi aliyeimudu Wizara Ile kwa kiasi chake kama Lukuvi. Kiukweli tumepata pigo. Yule mzee kidogo alikuwa na utu katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Ndio hivi yaani manaa anaacha mawaziri wa maana anateua watu wao hivyo wa kuturudisha nyyuma .2025 atakuwa na wakati mgumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duhh ngoja kwanza niko hapa mlingotini nasoma upepo nitawaletea taarifa kamili muda si mrefu.

Kwani hawawezi kusubiri kidogo??

Yes ipo live sasa.
Ndugu yako Ridhiwani ameula sasa.

Naiona Yanga ya mwaka huu ikiwa bingwa maana kila idara wamejazana
 
Huwa najiuliza sijui Kikwete huwa anaifikiria familia yake kwamba ataiachaje siku akienda au anafikiri ataishi milele? Hakuna Familia inayochukiwa Tanzania kama hiyo na kila siku chuki inazidi.

Haya Spika Ndugai yuko wapi ?
 
Back
Top Bottom