econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, CCM baada ya kututawala kwa miaka 60 wanaonesha dhahiri jinsi akili zao zilivyofika mwisho wa kufikiri. Sasa wanashindwa hata jambo dogo tu la kutafuta sura mpya zenye weledi zije kufanya kazi ya wananchi licha ya wasomi wengi waliopo.
Ni aibu kwa taifa la watu zaidi ya milioni 60 kuongozwa na sura zile zile kila awamu, huu mchezo wa kurithishana madaraka unatengeneza taifa la watawala na watawaliwa. Nawashangaa zaidi wale jamaa zangu wanaoitwa ikulu wakaimbe mipasho wakati hata wao keki ya taifa haiwahusu, hawa ndio watumwa haswa.
Mimi nashangaa jinsi Mambo yalivyogeuka kwa Kasi. Leo makamba, Nape na Ridhiwan ni Mawaziri. Aisee nobody knows about tomorrow. Nape alifukuzwa kisa kufuatilia sakata la Makonda kuvamia clouds.