PostGE2025 Rais Samia atangaza msamaha kwa washtakiwa wa kesi ya uhaini, “hasa kwa walioingia kwa kufuata mkumbo“

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kusamehe watu wasio na makosa hakuna tija. Hiyo ni danganya toto!

Tunataka yeye na majambazi wake wawajibike kwa massacre waliyofanya!
 
Hotuba ya Mama Leo imejaa Faraja na Matumaini Makubwa sana, She now speaks as Comforter in Chief

Mama tunaomba sana Uyaishi haya unayotuambia sisi tutakupa ushirikiano Mkubwa
 
Na waliouliwa wataweza kuwarudishia roho zao?

Pia angesema wote waliokamatwa kwa sababu ya maandamano waachiwe.
 
Wahaini wavaa madera bila shaka 😀😀😀! Na wauwaji vipi? Nani anawajibika?
 
Hotuba ya Mama Leo imejaa Faraja na Matumaini Makubwa sana, She now speaks as Comforter in Chief

Mama tunaomba sana Uyaishi haya unayotuambia sisi tutakupa ushirikiano Mkubwa
Ndio maana tunabanangwa kila siku, Kuwepo na mechanism za kumlazimisha kuyaishi anayoyasema sio tumuombe ayaishi.

Mechanism zitakazomlazimisha kila kiongozi kutenda wajibu wake na haki, tushaomba sana inatosha.

Halafu mmwambie vijana hawajafuata mkumbo.
 
Kesi ya uhaini haipo kwa hao vijana, wanatakiwa waachiwe wote waendelee na shughuli zao
 
Waliokamatwa kwa uhaini Waachiwe

Ninatambua kwamba vijana wengi waliokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya, navielekeza vyombo vya kisheria kuangalia kiwango cha makosa waliyofanya, na kwa wale ambao wanaonekana wamefata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wafutiwe makosa yao.

MY TAKE;

1. Watu mali zao zimeharibiwa, watu wamekufa. Tunahitaji kupewa miili ya ndugu zetu tukawazike.

2. Matendo ya kuua yamefanywa na Watendaji wa Serikali, uweje Wajichunguze?

3. Tunataka tume huru. Ili samia suluhu Hassan aache kuingilia mahakama.

4. Polisi na DPP wataficha wapi sura zao? Hadi samia kajua watu walibambikiwa kesi za uhaini. Bora hilo katambua kwamba polisi wanabambika kesi.
 
Ameanza kutii amri za geny z walizotoa kwenye barua yao!!

Sjui nani kwmshauri hili
 

Vijana: Tumekusikia lakini maombi yako tumeyakataa​

 
Reactions: naa
Kabisa hapo alipaswa kutoa msamaha tu kwa wote bila polisi kuhusishwa.
 
Mmmmmmmhhhhhh usitudanfanye..
Tutaendelea na agenda yetu
ICC
Uchaguzi ufutwe
Katiba Mpya
Polisi na ccm wooooooote jela inawahusu
Tume huru ya kikwelikweli
Achilia wafungwa wote wa kisiasa

Ndugu zetu wako wapi? Tuanzie hapa

Bunge haramu halina nafasi Tanganyika
Vinginevyo……
 
Katika ufunguzi wa bunge la 13 leo November 14, 2025 jijini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza msamaha kwa washtakiwa wote wa kesi ya uhaini walioingia kwa mkumbo.

Amesikika akisema "Nikiwa mama na mlezi wa taifa hili naagiza vyombo vya usalama na ulinzi kuangalia kiwango cha makosa ya walioshtakiwa kwa kesi ya uhaini hasa kwa walioingia kwa kufuata mkumbo waseme nao kisha wawaachie waende kwa wazazi wao"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…