Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Ally Hapi ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kwenye wilaya za mkoa wa Tabora. Jumatatu na jumanne alikuwa anajitambulisha wilaya ya Kaliua, jumatano na alhamisi alikuwa wilaya ya Urambo, ijumaa amehamishwa mkoa.

Sijui kama alishamaliza kujitambulisha Tabora. Kazi Iendelee.
Labda hata shule za watoto alikuwa hajapata

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae
View attachment 1814796
Tunasafisha nyumba au ghala hadi pale itakapo kuwa safi.

Tunaondoa masalia yoote na bado wengine inabidi wajiandae.
 
Mlevi Chalamila amefanya kosa gani huko?
Chalamila alikuwa mpenda sifa muonevu na mbwabaj. Kinacho furahisha kwa mama SSH hata wajaribu kumpenyezea majina ya watu hovyo atajitahidi kutumia vyombo vyake kufanya tathmini ya kina kubaini ukweli.

Mama hakosei ni makini sana. Sifa kubwa ya akina mama hawapendi aibu na fedheha ndiyo maana utakuta nyumba nyingi zilizokuwa na mama ni safi ndani na zinangaa. Ndiko huko tunako elekea taifa la Tanazania kutoka kwenye uigizaji kurudi kwenye uhalisia.

Nilikuwa naona aibu sana kuwa na viongozi kama kina: Ole Sabaya, Paul Makonda, etc ilikuwa ni aibu kwa taifa. Maombi yangu kwa mama ukimaliza na RCs, DCs, DEDs geukia kwenye Mashirika ya Umma na Taasisi za Elimu ya juu (hapa ifanyike ukaguzi maalum). Nina uhakika ukipitia sehemu zote nyumba itakuwa safi.

RC alikuwa RC kweli nikumbuka enzi za kina: Mashishanga, Mzindakaya, Mwambungu, Wasira, Meck Sadiq, Lukuvi, ole Kone, Rehema Nchimbi, Mwanri, Ndikilo, etc basi na muombea mama yetu mwenyezi Mungu amtangulie awapate kama hawa. Kiongozi wa umma ni kioo cha maadili mema na inatakiwa kuwa hivyo.
 
Ally Hapi ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kwenye wilaya za mkoa wa Tabora. Jumatatu na jumanne alikuwa anajitambulisha wilaya ya Kaliua, jumatano na alhamisi alikuwa wilaya ya Urambo, ijumaa amehamishwa mkoa.

Sijui kama alishamaliza kujitambulisha Tabora. Kazi Iendelee.
Huyo aanze naye kupaki mabegi yake
 
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
Hapi muda wake unakuja soon
 
Hon. Chalamila pitia hapa Mtwara nikupe tendo la ndoa bureee.... upunguze stress, vinginevyo wewe Mnyalu unaweza kujinyonga. Onyo! Usije na hung over ya BALIMI ya Kanda ya Ziwa.

KARAMA imekurudia, Sugu anakusubiri mkanywe ulanzi[emoji846][emoji846][emoji846]
Ngoja nije mimi unipe kwa niaba yake😊
 
Tuliandika humu kapelekwa kwenye lango la kutokea asipotuliza akili... wapambe wake wakatubeza Dar na Mwanza ni viatu vikubwa kwa "wenye miguu midogo..." waliokuwa wakimshangilia kwa hizo walizozisifia kuwa ni "akili" nadhani sasa wameelewa "...kwanini ilisemwa pombe kitovu cha uzembe!!" Ati ni comedian.... pole yake twamkaribisha uraiani ambako asipojichunga "wakalimani" watatafuna masurufu na mafao akija tahamaki....
Aione Phillipo Bukililo
Yesu Kristo aligeuza maji kuwa divai.
 
Hapi kapelekwa Mara Ili akatumbuliwa,hawa jiwe toxin zaidi ya kumsifia na kumtukuza mwendazake hawana sifa za kuwa watendaji
 
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?

Hahaaa Ally Happy inabidi ajitafakari next change anakaa benchi....Kwahiyo Bango limemuondoa Chalamila ,sasa inabidi polisi waanze naye kwa ile kesi aiyosema ya kuua kwa kumpiga risasi mtu.
 
Back
Top Bottom