Ndio maana nikasema kwamba wewe unatumiwa na wakwepa ushuru wa bandarini, wapitisha madawa ya kulevya na wezi wa vifaa vya magari na vitu mbali mbali vilivyopo pale bandarini.
Haiwezekani mtu mwenye akili yako huru na ambayo haijawekwa mfukoni na mtu yoyote utoe tuhuma bila kuweka ushahidi wa kile unachokituhumu afu utegemee mtu mwenye akili timamu kama mimi nitaungana na wewe kupigania masilahi ya wajanja wachache niliowataja hapo juu.
Weka mkataba wote hapa tuangalia hayo uliyoyaandika hapa kama yana ukweli kwa faida ya wasomaji wote.
Mimi sio mtu wa kuandikiwa au kuambiwa tu vitu na mtu au mwanasiasa fulan na mimi nianze kupanua mdomo bila kuoneshwa ushahidi, kwa faida yake yeye na familia yake.
Weka huo mkataba hapa tuone haya uliyoyaandika na kama hauna basi nitaamini kuwa na wew ni miongoni mwa waliolishimwa matango pori na wanufaika wa bandarini.