Rais Samia atetemesha, apongezwa kila kona kwa uzalendo wake wa kutanguliza mbele taifa

Rais Samia atetemesha, apongezwa kila kona kwa uzalendo wake wa kutanguliza mbele taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Rais Samia Ameendelea Kudhihirisha kwanini anapendwaa na kukubalika na watanzania,Amethibitisha sababu za mamilioni ya watanzania Kuendelea kumwamini na kumuunga mkono katika juhudi zake za kulijenga Taifa,Amethibitisha sababu za Tanzania Kuendelea kuwa yenye Amani,utulivu , mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.

Rais Samia Amethibitisha uzalendo na upendo wake kwa Taifa hili, Ameonyesha namna Taifa Hili lilivyokaa katika kifua chake, ameonyesha namna anavyoipenda Tanzania,Ameonyesha kuwa yupo madarakani kwa ajili ya Tanzania na watanzania,Ametoa Funzo kwa watu,kwa viongozi na kwa watanzania wenye ndoto ya kuwa viongozi kuwa uongozi Ni utumishi kwa watu na siyo mahali pa kuhitaji kuabudiwa na kusujudiwa,Ameonyesha kwa matendo na kauli kuwa Mwenyezi Mungu alimuinua na kumweka hapo ili kuwatumikia watu na siyo kutumikiwa na watu. Ameonyesha yupo hapo Alipo na anatenda yote atendayo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Rais Samia Ameendelea kuonyesha unyenyekevu wake,usikivu wake Na ucha Mungu wake. Anaendelea kuwafundisha watu kuwa hata ukiwa kiongozi wa ngazi ya juu bado wewe Ni mwanadamu unayepaswa kuwa mnyenyekevu na mwenye hofu ya Mungu huku ukijuwa kuwa vyeo na Madaraka Ni vya kupita na vyote hutoka kwa Mwenyezi Mungu muumba wa Mbingu Na Dunia.

Rais Samia Hataki kutumikiwa yeye Kama yeye Bali anataka kila mmoja wetu alitumikie na kulipigania Taifa letu.Anataka watanzania Tuendelee kulipenda Taifa letu.Rais Samia Ni Mzalendo wa dhati mwenye moyo wa upendo kwa Taifa letu tunayepaswa kumuunga mkono kwa nguvu zetu zote

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kwa kuwa Ameendelea kuonyesha namna anavyoipenda Tanzania na watanzania. Ndio sababu ya kuona akihangaika huku na kule katika juhudi za kulijenga Taifa letu.

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
 
Mlishaambiwa acheni haya mambo ya kumpaka rangi hujasikia?

Namba ya simu nani akupigie wewe chawa?[emoji1787]
 
Sasa hivi umekuwa mjanja kuweka namba, itakuwa rahisi kukufikia wakishakusikia.
 
Hasafishiki hata kwa dodoki la bati. Amefeli hadi aibu.

Anatamani leo ingekwa June 2025 abwage manyanga
 
Sikiliza badala ya kua lijinga Kila siku kuandika maujinga.

Andika makala za maana, zakuleta hoja, za kutatua .

Andika masuala yatakayofanya uonekane una kitu kichwan kwako !!!.

Wakikuona una kitu, utachaguliwa

Huuu upupu wako ni ujuha tu
 
Hata wewe waweza andika hayo unayoona kuwa ni Bora kuliko yangu ili nami nijifunze kutoka kwako
 
Wazungu wanasema rubbish, Waswahili tunasema takataka, Waitaliano wanasema la spazzatura, Wafaransa wanasema l' ordures, Wahispaniola wanasema la basura, Wajerumani wanasema der müll, Wareno wanasema o lixo, Waarabu wanasema زُبالة, na Wajapani wanasema ごみ(gomi). Sijui wewe kwa kilugha chenu mnaitaje "takataka" malizia mwenyewe....,...
 
Kwa kizungu kilichotulia tunasema "wiinya"!😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom