Rais Samia athibitisha kuna uhaba wa Shilingi nchini. Bila ya kifo cha Mafuru tungelijua hili?

Rais Samia athibitisha kuna uhaba wa Shilingi nchini. Bila ya kifo cha Mafuru tungelijua hili?

K
True say hili Taifa lina vichwa shida ni moja mfumo haupendi vichwa ila ndio mzee ref to Prof Assad no comment ni genius ila check kilicho mkuta siasa ina nguvu kuliko wasomi
abisa kabisa ma-genius hawatakiwi Nchi hii !
Mwisho wake huwa ni kudhalilishwa tu !
Lakini Mungu alishawaona na ameshawafikia I hope so !
Majuto ni mjukuu Tunasemaga Wasukuma. 😱
 
Kwani aliongelea upungufu wa sarafu za shilingi au shilingi kama currency? Sasa, kama kuna uhaba wa shilingi na wingi wa dola, sio kuwa maanake shilingi ipo nje? Na kama ipo nje, je kwa sasa tuna trade kwa shilingi?!
 
Kazi ipo, kumbe mtu anaweza kujivua uraisi for minutes na katiba inaruhusu!
Hiyo ndiyo leadership. The process of enabling a group of people to work together to achieve a common goal.

This definition emphasizes the importance of collaboration and teamwork in leadership
 
GPA haifanyi kazi bali ni utashi wa mtu binafsi tu. Huyo Mchechu mwenyewe akiwa UDSM ame graduate na karai (C)
Sema unatania kuhusu Mchechu😀! Inabidi nicheke kidogo manake nakumbuka nimewahi kufanya kazi na jamaa mmoja hivi! Mkuu, kwanza yule jamaa ukiambiwa amesoma vyuo vya TZ, tena wala sio UDSM unaweza kukataa!Na hata ukiamini alisoma Bongo utakuwa ni kama sie wengine ambao tulikuwa tunaamini hawa ni wale wa GPA ya 4.5+. Sasa siku moja nikamuuliza kwanini aliishia under grad peke yake akaniambia aliomba kusoma Masters UDSM lakini kwa kozi ambayo aliomba wakamtakalia kwa kigezo kwamba alitakiwa awe na angalau GPA ya 3.5! Sikutaka kumchimba manake ilitosha kujua jamaa huenda alikuwa Gent Pass aka Karai au Second Lower! Lakini ndo kama alivyosema TumainiEl hapo juu, Taifa lina aleji na real big brains kwa sababu hata yule jamaa alipigwa jungu hadi akaacha kazi! Mwezi uliopita nimekutana nae Dodoma yaani hana mbele wala nyuma lakini ana project yake kwenye PC, na akikudadavulia hapo unaiona potential yake ingawaje kwa project kama ile hata serikali yenyewe haina ubavu wa kuifanya ingawaje mwenyewe anaamini inawezekana, na ipo siku ataifanya😀😀! Sasa sijui ndo keshadata kwa kutokuwa na kazi wala shughuli yoyote kwa muda mrefu; so sad!
 
Hiyo ndiyo leadership. The process of enabling a group of people to work together to achieve a common goal.

This definition emphasizes the importance of collaboration and teamwork in leadership
Umekariri definition za CIVICS, kweli uko vizuri we CHAWA.

Fom Foo ulipata divisheni ngapi?
 
Jamani, na usomi wote huu mimi nashindwaje kuelewa ‘uhaba wa shillingi’? , ndio kitu gani hiki?
Mkuu kwa uelewa wangu naona kweli uhaba wa shilingi upo, hapa nilipo mfukoni sina shilingi napiga mahesabu nile nini ili nipige pasi ndefu hadi usiku
 
Wakuu,

Kumbe nchi ina uhaba wa sarafu za Shilingi na hatuambiwi?

Siku ya Leo akiwa msibani kwa Lawrence Mafuru Rais Samia alikumbushia amekumbushia kipindi ambacho kulikuwa na uhaba wa Shilingi na Mafuru alivyohusika katika kusaidia taifa kupita katika kipindi hiko.

"Badala ya kulalamika Nchi haina dola nimesikia juzi Wazalishaji wanalalmika Nchi haina shilingi, sasa mpango wa kurudisha shilingi

Ndugu yetu ameondoka nitawatumia waliokuwepo, la pili tulikumbwa na changamoto ya miradi katika sekta ya ujenzi na nikaita mkutano pale Zanzibar katika kikao kile tulijadili mengi mwisho nikawaambia katika hali kama hii tuliyofika kati yenu mmoja angekuwa Rais mngeamuaje na nikasema leo najivua Urais sasa hivi nampa Mafuru

Mafuru nyanyuka wewe sasa ndio Rais kwenye hali kama hii ungefanyaje?"


Rais Samia aliendelea kwa kusema:

"Alisimama kwa unyeyekevu mkubwa akaniambia Mheshimiwa Mimi si Rais na Urais uko mbali nami lakini katika hali kama hii akatoa mchango wake ambazo hakika ulitutoa pal tulipo tukaweza kusonga mbele"

View attachment 3152488
Tulizaga uelewe vizuri alichozungumzia mh. Rais
 
Sasa mbona watu wanajisifia kwa kazi wanayofanya wengine? Wahusi wanasifiwa wakati wameaga dunia, ni sawa kweli?
 
hii nchi inaharibiwa na tundu lissu na lema badala ya kujadili mambo ya maana kama haya kilasiku media zinajadili uchaguzi
 
Wakati mwingine wanasiasa wanakuwaga na mbwembwe kibao kumbe Kazi inafanywa na Watu wengine kabisa

Sijawahi kumsikia Mafuru akisema hadharani nimefanya hivi na vile Nasi tuliamini mambo Yote yalifanywa na Mawaziri wa Fedha na yule wa Uchumi

Ukimya nao ni mzuri

RIP Mafuru
Waziri ni political figure tu hafanyi chochote, kwenye wizara watendaji ni makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara katika wizara na team zao. Waziri anamezeashwa tu MA report akatapike kwenye public
 
Wakati mwingine wanasiasa wanakuwaga na mbwembwe kibao kumbe Kazi inafanywa na Watu wengine kabisa

Sijawahi kumsikia Mafuru akisema hadharani nimefanya hivi na vile Nasi tuliamini mambo Yote yalifanywa na Mawaziri wa Fedha na yule wa Uchumi

Ukimya nao ni mzuri

RIP Mafuru
Shida ipo kwa wanasiasa, hasa Wabunge...kumpa sifa Rais hata kwa majukumu ambayo yaliwahusu wao wenyewe!
 
Huyu mama yenu analalamika wakati yeye ni smooth leadership
 
Nchi hii wenye uwezo kichwani wengi wako kando halafu vilazaa wengi the so called waheshimiwa ndio wanaotuongoza, hatutatoboa ng'ooo!!!.
Mfano mavuvuzela kama Makondakta na Chalamila, makelele mengiii huku output hakuna.
 
Back
Top Bottom