Rais Samia Atoa milioni 100 kwa ajili ya Ukarabati kanisa la Katoliki Manyara

Hizo ni pesa zake binafsi vinginevyo angemuelekeza waziri wa fedha palepale atoe hizo pesa, ila serikali ilijenga msikiti wa Bakwata Kinondoni hili halina ubishi.
 
Alitakiwa akatoe ANGLICAN, LUTHERAN au MISIKITINI KATOLIKI sio wa level ya milioni 100 kwakweli ni kuwatania! Hili ni dhehebu tajiri!
Hawalazimishwi kupokea, wanaweza kuzikataa pamoja na kukataa kusamehewa ushuru wa forodha pale kwa DPW.
 
Katoa millioni 100 kutoka kwenye akaunti yake binafsi? Fafanua tafadhali.
 
Anawasaulisha😀😀
 
Ndio uzuri wa kuwa na Rais TAJIRI.
...Milioni mia!
Angekuwa masikini kama Nyerere sijui angetoa nini?
 
Mkuu hao viongozi wanaapa kwa kutumia biblia au quran

Serikali haina dini kivipi?Wakati wanaapisha wafanyakazi kwa viapo vya kidini na wanataja Muumba wa mbingu na nchi

Hata Marekani ,Viongozi wanatamka maneno ya kuomba msaada wa muumba mbingu na nchi wakati wa kuapa

Hakuna serikali ya kipagani katika dunia hii,Tawala nyingi zilipinduani kwa ukabila na udini

Udini na ukabila ndio silaha za kampeni mpaka ulaya na Marekani

Watu wanabaguliwa kwenye chaguzi za ulaya kwa dini zao na kabila zao

Huyo Samia kutoa pesa kanisani ni mambo yake binafsi na hakuna mahali wameonyesha vitabu vya ikulu vimekuwa Debited

Magufuli alitoa pesa barabarani na misikitini yalikuwa ni mambo yake binafsi na pesa zake ,Hakuna mahali wameonyesha vitabu vya ikulu vilikuwa debited
 
Wewe huelewi separation of church and state.

Na inawezekana huna uwezo wa kuelewa.
 
Hizo fedha ni zake binafsi au ni za walipa kodi? Tanzania haina dini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…