Rais Samia Atoa milioni 100 kwa ajili ya Ukarabati kanisa la Katoliki Manyara

Tanzania ni nchi inayoongozwa na serikali isiyo na dini. Ikiwa kila mwenye taasisi yake ya dini atataka apewe fedha hii na rais, rais ataweza kutoa hela sawa kwa wote?

Kwa nini serikali inajiingiza kwenye mamo ya kufadhili makanisa,wakati kuna kazi nyingi za serikali zinahitaji pesa?
Serikali haina dini ila watu wake wana dini.
 
Endelea kuweka neno mkuu.
Rais Nyerere alijitambulisha kama Mkatoliki. Alipokuwa Dar es salaam, kila siku asubuhi alikuwa akisali kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay. Tuliokaa Oysterbay tulimuona. Si Jumapili tu, kila siku.

Alipewa shutuma kwamba anapendelea Wakatoliki.

Akasema serikali yake hata haijui mawaziri ni wa madhehebu gani, anajua tu wanavyoapa wanatumia kitabu gani. Alisema serikali haina haja ya kujihusisha na mambo ya dini. Alisema hata kwenye kuhesabu watu, serikali haikusanyi idadi ya watu gani ni wa dini gani, na kama mtu anatafuta habari hizo, aende kwenye taasisi za dini.

Nyerere hakuwahi kutoa hela za serikali hivi kwenye taasisi za dini, kwa sababu alielewa mipaka ya serikali na dini.

Nyerere hakuwahi hata kupanda mbele kwenye altare kanisani kusema neno kanisani kama rais.

Rais Mkapa naye alikuwa anakwenda kanisa la St. Immaculata Upanga, hakuwahi hata kupanda madhabahuni kutoa neno kama rais. Alielewa mipaka ya serikali na dini, separation of church and state/ religion.

Sasa hawa viongozi wetu wa sasa wanaosema wanamuenzi Nyerere, mbona tunawaona wanaondoka kwenye misingi ya Nyerere ya kukataa kuchanganya mambo ya serikali na dini?
 
Hii si sawa,

Halafu rais ni nini maana Rais ni ofisi.... maana yake ni fedha za umma zile.

Ndio maana hata afya yake na ulinzi wake ni sisi wananchi tunawajibika.

Kwa nini wasifanye mambo ambayo ni ya msingi kama umeme na maji.... na elimu badala ya hizi takrima ndogondogo
Saa 100 ni mfano wa rahisi asiyependa kuumiza kichwa kabisa na anaona njia ya rahisi yeye kujipatia ummarufu ni hiyo ya kugawa psa za wananchi hivyo hovyo Laiti kama angekuwa na uwezo wa kuzitafuta angeziheshimu
 
Tanzania ni nchi inayoongozwa na serikali isiyo na dini. Ikiwa kila mwenye taasisi yake ya dini atataka apewe fedha hii na rais, rais ataweza kutoa hela sawa kwa wote?

Kwa nini serikali inajiingiza kwenye mamo ya kufadhili makanisa,wakati kuna kazi nyingi za serikali zinahitaji pesa?
Politics...
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya zoezi la kutabaruku Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu, Babati mkoani Manyara ikiwa ni mchango wake kwa kanisa hilo.

Kwa niaba ya Rais, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa kauli hiyo katika Misa Maalum ya kumwombea Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Nyerere.

Hii ina ashiria Amani na Nuru ya maelewano baina ya Serikali Ya Dr. Samia na Kanisa Katoliki, na hii ni baada ya miezi iliyopita Baraza la Maaskofu la Kanisa hilo Kutoa Waraka uliokuwa unapinga mkataba wa Serikali.

Binafsi nasema kila la Kheri, Mungu alisimamie Taifa letu la Tanzania.
Maelewano gani kwani kulikuwa na kutoelewana kati ya Rais Samia na kanisa? Kupinga uuzwaji wa bandari haikumaanisha ugomvi wa kanisa na raisi

Sent from my Infinix X660C using JamiiForums mobile app
 
Rais Nyerere alijitambulisha kama Mkatoliki. Alipokuwa Dar es salaam, kila siku asubuhi alikuwa akisali kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay. Tuliokaa Oysterbay tulimuona. Si Jumapili tu, kila siku.

Alipewa shutuma kwamba anapendelea Wakatoliki.

Akasema serikali yake hata haijui mawaziri ni wa madhehebu gani, anajua tu wanavyoapa wanatumia kitabu gani. Alisema serikali haina haja ya kujihusisha na mambo ya dini. Alisema hata kwenye kuhesabu watu, serikali haikusanyi idadi ya watu gani ni wa dini gani, na kama mtu anatafuta habari hizo, aende kwenye taasisi za dini.

Nyerere hakuwahi kutoa hela za serikali hivi kwenye taasisi za dini, kwa sababu alielewa mipaka ya serikali na dini.

Nyerere hakuwahi hata kupanda mbele kwenye altare kanisani kusema neno kanisani kama rais.

Rais Mkapa naye alikuwa anakwenda kanisa la St. Immaculata Upanga, hakuwahi hata kupanda madhabahuni kutoa neno kama rais. Alielewa mipaka ya serikali na dini, separation of church and state/ religion.

Sasa hawa viongozi wetu wa sasa wanaosema wanamuenzi Nyerere, mbona tunawaona wanaondoka kwenye misingi ya Nyerere ya kukataa kuchanganya mambo ya serikali na dini?
Mgema ukimsifia sana pombe huitia maji.

Na kweli pombe imewekwa maji mkuu
 
Back
Top Bottom