Rais Samia atoa TZS 300BL kukamilisha majengo ya Serikali Jijini Dodoma

Yaani hizi taarifa zina ukakasi mnoo. Kwani hela za maendeleo hutolewa na rais au huidhinishwa na bunge?? Mna tuletea mambo ya mwenda kuzimu hapa??
 
Ni kukosa akili au uelewa mdogo kusema kuwa Rais ametoa hela.

Ukisikia tu kiongozi anasema Rais ametoa hela, huyo mtu:

1) Huenda ana akili ndogo kiasi cha kutotambua kuwa Rais hana hela ya kuendesha Serikali wala ya kutekeleza miradi ya umma.

2) Huenda huyo mtu hana weledi, na kwa sababu hana kitu chochote kichwani wala kiutendaji cha Mh. Rais kuendelea kumwamini, anaamua kuwa mnafiki na kuamua kumvika Rais mamlaka na uwezo ambao hana.

Kama viongpzi wetu wangekuwa na hekima, pale wanaposikia sifa za kijinga au wanapoona watu wanawavika mamlaka au utukufu ambao, kama Rais, hawezi kuwa nao, walistahili kuwafukuza kazi watu hao mara moja.
 
Tanzania na Samia,

1.Uchumi Juu,

2. Uwekezaji juu

3. Diplomasia juu

4. Amani & Upendo juu

5. Maendeleo juu

6. Demokrasia juu
 
Rais ni taasisi
 
safi sana, wacha jiji la Dodoma lijengwe.
 
Acha tuhamie DODOMA naona Ajira zimeshamiri sasa
 
Sipendi kabisa lugha hii ya "Rais Samia ametoa pesa" Pesa inatolewa na serikali na si Rais.
 
Haya Mambo kwa kikwete mkapa mwinyi na nyerere hayapo.cjui kwann hizi awamu wameanzisha eti hela ya Samia hela ya magu.hela ni ya serikali.
 
Sipendi kabisa lugha hii ya "Rais Samia ametoa pesa" Pesa inatolewa na serikali na si Rais.
Lugha hii ya Rais ametoa, mara nyingi hutumiwa na watu wanafiki kwaajili ya kuwapumbaza wajinga, na kumlewesha Rais kwa maneno ya hila.
 
Mama nakupongeza Kwa hili,safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…