Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za heri ya sikukuu ya Eid el Adh’haa kwa dua maalum akiwataka Watanzania kusherehekea kwa amani, umoja na upendo.
Ametuma salamu hizo leo Alhamisi Juni 29, 2023 kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii huku akiwahimiza Waislamu kutumia siku hii kuwakumbuka wale wote wenye uhitaji zaidi.
“Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid el Adh’haa. Tusheherekee siku hii njema kwa amani, umoja na upendo, tukiwakumbuka wale wote wenye uhitaji zaidi.
“Tutumie siku hii pia kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu azipokee ibada zetu, atusamehe makosa yetu, atuongoze katika mema, kweli na haki, tuendelee kuwa wamoja na atuepushe na yote yenye nia ya kutugawa. Eid el Adh’haa Mubarak,” ameandika Rais Samia.
Hajawakumbuka wenye uhitaji wa kujua mustakabal wa mkataba wa bandari zetu.