PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ni wanachama hai, tembelea www.ccm.or.tz kwa taarifa zaidi kuhusu wanachama wa CCM
Yaani nitembelee tovuti ya wapika data? Mnagawa kadi kwa wanafunzi kwa lazima wakati hawana muda na nyie. Wanawachora na kuwalia hela zenu kwenye semina.Yaani wanafunzi wanawachukulia kama mashuga dadi wa kuwalia hela, lakini hawana vibe na nyie kabisa.
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
Nani anamchunguza aliyetoa order ya shoot to kill?

Akishamaliza kumchunguza watamshtaki wapi?

Hayo maigizo ni phase II tu wenye akili tunajua kuna policcm na usalamaccm wameandaliwa kama mbuzi wa kafara baada ya hapo ili wahusika wakuu wasafishwe.

Wajinga waliisha .
 
Kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwake ,waache waruke ruke tu ,Samia anataka kuwalinda wasaidizi wake IGP.GDIS ,CDF ila bila kuwatoa hao kafara ataingia yeye kitanzini.
Amewakaanga, kuua ni jinai. Kuiba au kuharibu ni madai. Tunataka kujua aliyeagiza kuua..

Yaani kitaeleweka. Kuna washenzi wanasema waliouawa waliharibu mali. Sheria za Tanzania hazisemi mtu akiharibu mali auawe..

Kupotea kwa watu, ni kichocheo cha maandamano. Tuwajue wanaoteka watu
 
Mapito ya waheshimiwa majaji

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Awadh Bawazir photo

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Mwenyekiti Rufani ya Zabuni za Umma PPAA: Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma PPAA ni chombo cha kisheria nchini Tanzania chenye jukumu la kusikiliza na kutatua malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya ununuzi wa umma na utupaji wa mali za umma. Inafanya kazi kama mhimili huru wa kisheria unaosimamia haki na usawa kwa wazabuni na taasisi zinazonunua .


Retired Judge Gad John Mjemmas
1779122374998.jpeg

Pichani ni Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Gad Mjemmas ​

The President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, has appointed Retired Retired Judge Gad John Mjemmas as the Chairperson of the Tax Revenue Appeals Tribunal (TRAT) 2025

Baraza la Rufaa la Mapato ya Ushuru (TRAT) nchini Tanzania ndilo chombo cha pili cha rufaa kwa migogoro ya kodi . Jukumu lake kuu ni kusikiliza na kuamua migogoro ya kodi ya kiraia kati ya walipa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hasa likifanya kazi kama chombo cha rufaa kwa maamuzi yaliyofanywa awali na Bodi ya Rufaa ya Mapato ya Ushuru (TRAB). [1, 2, 3]

19 October 2018
1779122519165.jpeg

Mhe. Jaji Kiongozi (katikati) akimkabidhi shada la maua, Jaji Mstaafu, Mhe. Jaji Gad Mjemmas ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kustaafu salama, anayeshuhudia (aliyesimama nyuma mwenye miwani) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kitengo cha Usuluhishi ‘Mediation’, Mhe. Rose Teemba na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Crencensia Makuru.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
​


Jaji Aishiel Nelson Sumari
1779120556729.jpeg

24 Juni 2014 Jaji Aishiel Nelson Sumari mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi Jaji Sumari majaribuni tena Moshi | JAMHURI MEDIA

MAAMUZI YA KESI MUHIMU KABLA YA MAJAJI KUSTAAFU :
..


​

Panafrican Energy T. Ltd vs Commissioner General Tra (Civil Appeal 121 of 2018) [2019] TZCA 170 (31 May 2019) - [2019] TZCA 170​

​
 
Yaani nitembelee tovuti ya wapika data? Mnagawa kadi kwa wanafunzi kwa lazima wakati hawana muda na nyie. Wanawachora na kuwalia hela zenu kwenye semina.Yaani wanafunzi wanawachukulia kama mashuga dadi wa kuwalia hela, lakini hawana vibe na nyie kabisa.
Acha propaganda mkuu, CCM ni chama makini na well ahead of time, kina wanachama na ofisi mpaka nje ya nchi kwa taarifa yako
 
Amewakaanga, kuua ni jinai. Kuiba au kuharibu ni madai. Tunataka kujua aliyeagiza kuua..

Yaani kitaeleweka. Kuna washenzi wanasema waliharibu mali. Sheria za Tanzania hazisemi mtu akiharibu malu auawe..
Haki itendeke ,kuua watu kisa madaraka moja kwa moja The Hague ,SSH hakuchaguliwa na wananchi bali amechaguliwa na TUME(Sisi tumeona kulikuwa hakuna uchaguzi na Hata Jaji warioba amesema wazi).

SSH kulinda heshima aachie ngazi ,mali alizochuma ni nyingi sana zinatosha kula wanae ,wajukuu na vitukuu ya nini kung'ang'ania madarka?
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
Tume ya pili inachunguza nini wakati tume ya kwanza ilisema wanaodaiwa kuwa ni polisi? Tume inakuja na maneno wanaodaiwa?

Walioua watu mitaani ni jeshi la polisi na wengi waliuawa siku ya tarehe 29 kuanzia saa 10 jioni na kuendelea usiku kucha na siku ya octoba 30 mimi binafsi nilishuhudia watu wakipigwa risasi na POLISI. Tena wakiwa kwenye gari ya POLISI na watu wenyewe walikua wamejikalia tu sehemu wanapiga story.
Watu wengi hawakujua kama polisi wanaua watu hovyo kutokana na kuzuiwa mitandao ya kusambaza tasrifa hivyo octoba 30 wengi hawakujua kinachoendelea mitaani wakawa wanajipitia tu hovyo kumbe ndiyo wanaenda kuuliwa.
 
wameuliwa Christians kwa wingi na hata wanajitapa kabisa kwamba hakuna muslims aliouliwa, halafu jaji kateuliwa ni muslim, na zilikuwa ni targeted killings, hizi sarakasi zote zina mwisho ...
 
Back
Top Bottom